Ukweli usemwe. Hii inakera sana

Kipenseli

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2020
Posts
825
Reaction score
1,074
Habari zenu wakuu?

Nisiwachoshe sana maana najua wengine mnaendelea na majukumu yenu muda huu alafu inawezekana umekereka Sana[emoji16]

*Inakera sana unakuta majirani na watu kibao wanaokuzunguka ambao huwa hawashiriki pamoja na wewe (uwe mchango wa hali au Mali) katika masomo yako lakini the way wanavyoulizia matokeo yako utadhani kulikuwa na msaada wao mkubwa mpaka wewe ukafanya mtihani ila fresh ngoja nivunge[emoji41]

*Haya unakuta umepanda zako daladala anaingia mtu na kamzigo kake anakuomba umshikie kale kamzigo bila kuzingatia jinsi ulivyo au aina ya mzigo anaokupa...(Hapa tuliopakwa shombo la samaki Kama papa,nguru n.k mtakuwa mshaelewa[emoji23]). Au unapewa kafurushi hivi mpaka status yako inashuka ghafla[emoji16] ila tuachane na hiyo maana Ni msaada wa lazima[emoji3]. Mungu tujaalie tuwe na vbox vyetu au tuwe na uwezo wa kukodi hata taxi tunapoenda makazini.

*Hii ndo itanifanya nije kumlamba mtu makofi[emoji3] unakuta jitu linaamini kitu fulani lakini linataka likuaminishe kuwa kile anachokiamini ni sahihi kuliko wewe unavyoamini hapa hilo limtu halizingatii uelewa wako au kiwango chako Cha elimu (Inshort wewe unakua juu kielimu kuliko yeye na kile mnachobishania kuaminishana usikute wewe ndo course yako[emoji18] na yeye kaishia la tatu C huko.

*Hii ya kutoa Siri za faragha kwa wapenzi[emoji533] au wana ndoa nayo inanikera ila kwa kuwa Mimi sio kungwi wala somo yake[emoji16] ngoja ninyamaze[emoji850]
 
Bro jukumu la kulipa ada si lao ila kujua matokeo ni kutaka kujua tu maendeleo yako
 
Bro jukumu la kulipa ada si lao ila kujua matokeo ni kutaka kujua tu maendeleo yako
Maendeleo kwenye results tu!? Ila kipindi Cha masomo hawatakiwi kujua maendeleo yako??
 
Kuna mtu aliniuliza matokeo form four kipindi hicho nipo teenager ndo najiandaa kuingia form five.Nikamuambia daraja na points.Akaniuliza na shule uliyochaguliwa? Nikamwambia.

Baadaye nikakuta wanajadiliana na mwanaye;"Huyu naye anajipitisha pitisha kwangu ili tujue amefaulu na kwenda shule nzuri".Waliponiona wakajidai kunipongeza.

Sasa mtu sikumtuma aniulize,na njia niliyokutana naye ni barabarani kabisa wala hakuna aliyejipitisha kwa mwenzie,tukigeuziana mgongo anaanza kunipepeta kwa watu.

Ya form six yametoka,kaja home kuniuliza,nikamjibu sijui. Mbona yametangazwa yametoka? Sijaangalia.Hatukuongeleshana tena hadi nahama nyumbani.

Umasikini ni uchawi tu.
 
Sijui kwann wabongo[emoji16].
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…