Ukweli usemwe tu

Hadrianus

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2020
Posts
2,112
Reaction score
5,229
Katija dirisha kubwa la Usajili, Simba iliwasajili wachezaji

1. David Kameta "Duchu"
2. Charles Ilanfya
3. Chris Mugalu "The Animal"
4. Rally Bwalya "Magician"
5. Benard Morrison "mkuki wa sumu"
6. Joash Onyango "Babu"
7. Ibrahim Ame

Katika wachezaji hao 7 waliosajiliwa ni Joash Onyango ndiye amechaza mechi nyingi zaidi akifuatiwa na Bwalya, Morrison.

Chris Mugalu amekua akitokea sana benchi na ameanza mechi 1 tu mechi zingine amezikosa kutokana na majeraha ya mara kwa mara ambayo anayapatia huko mazoezini (gari la mkaa, umri)

Rally Bwalya ameaminiwa mara kadhaa ika ukweli huyu dogo hana maajabu yoyote zaidi ya kucheza na jukwaa sawa na Morrison.

Ikumbukwe Simba walitamba wanafanya usajili kwa ajili ya kujiimarisha na CAF CHAMPIONS LEAGUE, ila tumeona wachezaji 99% wamechemsha na wameonesha uwezo mdogo sana kuliko matarajio.

Naweza kusema JOASH ACHIENG ONYANGO peke yake ndiye sajili iliyo lipa kutokana na anavocheza lakini pia ameonekana kuaminiwa haraka na kocha Mbelgiji SVEN.

Bwalya tulitegemea uwezo wake uwe kariba ya CHOTA CHAMA, ila akiwa uwanjani anaruka ruka tu kama maharage.

Mugalu tulitegemea awe anahatari kuliko Kagere ama Bocco ila kwa mechi chache alizocheza tumeona kabisa jamaa alivo mzito japo ni mzuri kwa umaliziaji lakini nathubutu kusema MUGALU hajafika uwezo hata 40% ya MEDDIE KAGERE (MK14).

Duchu yupo kujifunza kwa Kapombe, kocha ajaribu kumpa uzoefu asisubiri Kapombe aumie kabisa ndiyo aanze kumpanga, dogo ataharibu kwa presha. Japo kipaji anacho.

Ibrahim Ame huyu nadhani alisajiliwa kwa mihemko ya Upande wa pili (Utopoloni)

Charlse Ilanfya sijui hata alisajiliwa kwa sababu zipi, ameanza mechi 1 na aliishia kukimbia kimbia hadi ameomba arudi KMC kwa mkopo.

Benard Morrison ni mchezaji anayecheza na jukwaa sana, nadhani nafasi yake ni bora zaidi kumchezesha FRANCIS KAHATA NYAMBURA (kijiko).
Usajili wake nathubutu kusema ni usajili wa "kipumbavu kabisa".

Mechi ya Jumamosi 06/12/2021 wachezaji 11 walio anza (Starting XI) ni Simba ile ile isipo kua LUIS MIQUESSON tu ndiye hakuepo katika kikosi kilichotinga robo fainali wakati wa kocha PATRICK AUSSEMS "Uchebe". Waliokua benchi kulikua na maingizo mawili tu AME na MORRISON, wengine walikua jukwaani.

Kwa maana hiyo wachezaji wa 3 wapya ndiyo walioshiriki mchezo huo na wawili pekee wakicheza.

Simba Sc Tanzania katika suala la Usajili bado sana, mwendelezo mbovu wa kusajili unaendelea baada ya kuchemsha kwa WILKER DA SILVA, TAIRONE, KENNEDY, HARUNA SHAMTE, MIRAJI ATHUMAN.


Msimu huu wa 2020/2021 Simba Sc Tanzania imesajili wachezaji wasio na tija na faida yoyote na hawana impact katika michuano ya CAF CL wala Ligi kuu.

Flops
 
Simba wanasajili bila kuangalia mahitaji ya timu, tuna viungo wengi washambuliaji, tuna tatizo la kiungo mkabaji muda mrefu, Mugalu ana historia ya majeruhi toka alipotoka.

Kwa aina ya wachezaji tuliokuwa nao msimu uliopita tulitakiwa tusisajili zaidi ya wachezaji watano ila usajili wa kukomoa na bila kufikiria ndio matokeo yake.

Zaidi ya yote Simba haina kocha zaidi ya mzungu mwenye vyeti vya ukocha.
 
Kwahiyo sisi tufayeje sasa? Au kuna pesa yako ulichangia kwenye hizo sajili inayokuuma tukurudishie.
 
Hatujafika vipi level za kupambania champions league wakati Hilo kombe hakuna mwenye haki miliki nalo?
Hata Simba tunaweza kulichukua Hilo kombe.
Hatujafika levo ya kupambania champions league,ni kwa ajili ya uhitaji wa league ya ndani tuu,pale utopoloni wachezaji wengi wapya wanatumia nguvu tuu,akili ya mpira hakuna."Ligi yetu,kivyetu vyetu"
 
Ndiyo ukomo wa kufikiri kwako?
co uwezo wa kufikir hayo ni ya kawaida kwenye soka kumbuka wanaosajiliwa ni 30 ila wanaotakiwa kucheza ni 11 haiwezekaniwote wakapata nafac unaweza ukaona hana kitu akaja kocha mpya akawa ctaa
 
co uwezo wa kufikir hayo ni ya kawaida kwenye soka kumbuka wanaosajiliwa ni 30 ila wanaotakiwa kucheza ni 11 haiwezekaniwote wakapata nafac unaweza ukaona hana kitu akaja kocha mpya akawa ctaa
Uwezo wa hao wachezaji wapya hata aje nani, hawawezi kubadilika.
 
Kama kweli wewe ni mwana Simba upo vizuri kuichambua timu yako na umeongea vema sana
 
Wamatopeni Fc Mbona Mapema Mnaanza Kulalamika Subirini Safari Mbona Bado!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…