GE2025 Ukweli usioufahamu kuhusu wanaosema wataandamana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
 
Tatizo jingine kuna mkakati wa kuandamana? Wakishaandamana hatma yake nini? Mfano ukiandamana Dar unafanikisha nini? Kila kitu sasa ni Dodoma. Pale wagogo hawawezi kuandamana maana hawana huo mwamko. Pale ndipo pana kila kitu. Dar utavunja tu biashara za watu, then what?
 
Maandamano ambayo yangekuwa ya maana ni kugoma kwenda kupiga kura Watanganyika wote wangekuwa wanajielewa wangeamua kubaki majumbani mwao siku hiyo 29 October lakini walivyo mazuzu watakwenda kuchomwa na jua kupanga foleni kushiriki najisi hii.
 
Maandamano ambayo yangekuwa ya maana ni kugoma kwenda kupiga kura Watanganyika wote wangekuwa wanajielewa wangeamua kubaki majumbani mwao siku hiyo 29 October lakini walivyo mazuzu watakwenda kuchomwa na jua kupanga foleni kushiriki najisi hii.
Kuna namna kadhaa uchaguzi utakuwa wa fujo
 
Mi najua maandamano hayawezekana kwa sababu moja tu
Haya maandamano yanahamasishwa mitandaoni tu ila mtaani watu wengi hawajui na wala hawana habar za mitandaoni na apo ndo shida inaanzia

Ata ukifuatilia kundi la vijana hawa mnaowaita gen z weng hawako mitandaoni na walioko mitandaoni akili yao kubwa ni mapenzi, betting na kufuatilia habar za wasanii
Kwa ufupi gen z wa Tanzania hawajapevuka, bado hawayajayajua maisha bado weng ni kula kulala na akipata pesa ya vocha,kuonga na pesa ya bata bas maisha yake yamekamilika hawawazi zaidi ya apo

Tz tuko nyuma sana ktk masuala ya mitandao nani ngumu sana kufanya kitu kwa kutegemea mtandao

Ata hawa wasanii wetu wanaoshinda tuzo za m tv, BET Wengi hushinda sabu hupigiwa kula na wakenya ila sio watanzania maana watanzania weng atujui kutumia mitandao
 
Kuna namna kadhaa uchaguzi utakuwa wa fujo
Fujo hazitakuwepo ila ninachojua INEC watapika takwimu kwa sababu wote wenye kujitambua hawatapoteza muda wao kushiriki hii najisi sasa ili kuficha aibu yao watasema waliopiga kura ni m39 lakini ukweli watakaopiga kura hawatazidi m12.
 
Sio kuwa watu wote wanaweza kuandamana.

Wakitoka watu laki 2 tu, wakaandaman hata wiki tu, kwisha.

Serikali ya kijuha ambayo mpaka inamuogopa Sativa au Chaula mchoraji unadhani ina uwezo wa kushindana na watu elfu 50???
 
NGOJA NIWAAMBIE WATU KUWA UKIWA NA TOR BROWSER UNAWEZA kuAccess Jamii forumsπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mie nahisi maandamano haya yatafeli, ila CCM wajiangalie mwisho wao upo karibu kama wasipobadilika, raia zimechoka, ni vile zinategeana nani atamfunga paka kengele.
 
Hakuna wa kuandamana bwana tarehe 29.
HAKUNA asilimia 96 watu wanaoongea humu mitandaoni ni kuhamasisha ila huwa hawajitokezi.
Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na wanasiasa wanaofanya upinzani kama Ajira
 
Maandamano hayapangiwi tarehe raia wakichoka huwa wanatoka wenyewe bila kuambiwa, hii ya kupanga tarehe na kumjaza mtu mizuka ya uongo na kweli siyo rahisi kufanikiwa
Huku Familia za wahamasishaji zikiwa US na Canada salama salimini. Siku ya maandamano wanajituliza kwenye masofa simu zikiwa na bundles huku pembeni popcorn kama za 230,000/= zikiwasindikiza kutazama nyumbu zinavyoshughulikiwa. Kimsingi wahamasishaji wamekosa kabisa uhalali wa kusema watu waandamane.
 
Gen z wa bongo
Waliopo mitandaoni ni
Kubet
Mademu
Umbea.
Ukiona anaandika kuhusu wakina Lissu ni kutafuta umaarufu.

Waliopo mtaani ambao ni kizazi cha nyumba kidogo wako busy kuhustle hawajui hata yanayoendelea mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…