Ukweli wa Erick Kabendera ndio huu

Ukweli wa Erick Kabendera ndio huu

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
18,833
Reaction score
23,276
Kwanza kabisa niwape pole familia ya Kabendera, wengi wanaogopa kusema ukweli na makosa ya Kabendera kwa upande wake,kwa kuwa wataonekana hawana ubinaadamu.

Lakini kama nchi, Kabendera aliikosea sana akaangalia maslahi yake akamtukana Rais atakavyo akainanga serikali atakavyo eti leo hii kuna watu ni watetezi wake na bado Jeshi la Polisi lilitoa sababu kwanini lilimkamata kwa kumvamia kwa kuwa alikaidi wito,je hapo hatuoni makosa ya Kabendera.

Kwanini alikuwa hataki kuitikia wito kama huna kosa polisi ni rafiki na kwenda polisi sio kwamba umefungwa tayari ni mahojiano.

Kabendera alikuwa anaonyesha jeuri kuwa nyuma yake kuna ubalozi wa mmarekani na uingereza.

Ndio maana alikuwa anakaidi,bwana huyo anaonekana ana mambo mengi mabaya ana tuhuma za kukwepa kodi na kutakatisha fedha bado kuna watu wanatetea je mnaujua undani wake ilihali wengine wanakamatwa italy kwa kwa kusafirisha madawa.

Tuwache kupiga mayowe waachwe jeshi la polisi,mahakama wafanye kazi yao ndio watakaotoa maamuzi ya haki na sheria.

Angalizo hawezi kuwa mfungwa bila ya kutiwa hatiani na mahakama!
 
Hv huu upuuzi mnaondikaga hapa kisa buku saba una uhakika ametakatisha fedha? Unapompa kesi ya kumnyima dhamana si umemfunga tu hapo leo rugemalila ana miaka mingapi jela jinga kabisa ww na mtu akishikwa na madawa ya kulevya inatuhusu nini sisi hio ni personal interest zake
 
Kwani Mkuu kwanini sasa tunadangaywa kuwa Uhujumu uchumi kumbe hilo siyo tatizo kubwa, maana content nzima ya Andiko lako ni Kumchafua Mfalme wenu.
Halafu Kabendera anafanya biashara gani mpaka aingie Kukwepa Kodi na kuhujmu Uchumi? Hata haingii akilini hata Kidogo.
 
Nchi zilizoendelea raisi anachanwa lakini hakuna mtu anakamatwa, sisi tumebaki na tabia zetu za kizamani. Kama muandishi anaamua kuandika uharo mwache aandike, hakuna litakalo haribika. Mambo mengine tunajitakia wenyewe, kwani raisi amepungukiwa kitu gani kutokana na hayo maandishi. Tatizo letu wantanzania ego imetuzidi, mtu akiwa kiongozi basi anakua mungu mtu, hata yesu alitukanwa itakuja kuwa magufuli. Haki yao wazungu watuseme.
 
Taarifa ya awali kutoka kwa polisi na uhamiaji walisema kuwa alikamatwa kwa sababu ya kwenda kuhojiwa uraia wake, hayo makosa yaliojitokeza baadae ni makosa ya kutafutiwa kituoni baada ya kosa la kwanza kukosa mshiko.
 
Mie nikafikiri una ukweli sawa na kichwa cha habari, kumbe ni wale wale.
Mbona sasa hajashitakiwa kwa kosa la kumtukana rais kama unavyodai ?
 
Utangulizi tu umechemka.
Sheria zipo wazi namna ya kumfungulia mtu mashitaka na kumkamata.Acha mbwembwe binafsi nakuona huna hoja ya msingi.
 
Mm nilidhan unaandika cha maana pumbavu Sana ww!!! Ngojea utekwe ndio akili zitakurudia
 
Back
Top Bottom