Ukweli wa hii habari ni kweli ndalichako kakanusha

chedyrichie

Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
7
Reaction score
7
WIZARA YA ELIMU YAKANUSHA TAARIFA ZILIZOSAMBAA KUWA HAITOAJIRI TENA WALIMU WA ARTS


Akitoa ufafanuzi juu ya ajira mpya za walimu zilizotangazwa na waziri wa elimu kuwa wamezfuta ajira za walimu wa sanaa amesema hivi

"Sijui hizi habari hawa wanahabari wanazipokea vipi na kuzipeleka vipi kwa wananchi, mliorecord maongezi yangu ya Jana Nendeni mkasikilize vizuri kama nilisema nimezifuta ajira za walimu wa Sanaa ila Leo asubuhi kuna gazeti flani limeandika front page hivi "NDALICHAKO AFUTA AJIRA ZA WALIMU WA ARTS"

Nilichokisema tumeanza ajira za walimu na tumetoa tangazo kwa walimu wa sayansi na hesabati watume vyeti vyao kwanza maana shule nyingi hazina walimu wa Sayansi na hesabati. Ktk elimu kuna matatizo mengi moja wapo kubwa ni ukosefu wa walimu wa masomo ya sayansi na hesabati nchi nzima.

Bado mchakato unaendelea sasa mbona mnawapa pressure hawa walimu?

Nimepata taarifa sehemu mbalimbali wengine wamezimia wengine wamemeza vidonge wengine hata kula wameshindwa kutokana na taarifa hii.

Sharia ya habari na mawasiliano tayari mh raisi ameisign nafkiri hawa wanaopotosha umma kwa maslahi yao wenyewe itawachukulia hatua kali.

Mh raisi anawapenda wote na anataka mrudishe hela zake mlizokopeshwa ndo maana anaikarabati vizuri wizara hii mda ukifika tutaangalia sasa tuwapeleke wapi kulingana na uhitaji wa sehemu husika.

Ila nitoe ombi langu kwa walimu msikae bure kusubiri ajira, jishughulisheni na shughuli mbalimbali mwenye kaeneo alime mbogamboga, mwenye kamtaji afungue biashara ndogondogon.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…