Ukweli wa kimahesabu katika kuwekeza kwenye ufugaji wa kware

Ukweli wa kimahesabu katika kuwekeza kwenye ufugaji wa kware

Tumainiandy

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2014
Posts
430
Reaction score
91
Nashukuru kuwa ufugaji wa kware unaendelea kupata wapenzi wengi kutokana na faida kama chakula bora kwa ndege huyu ila kumekuwa na taarifa nyingi na hasa faida ya kifedha ambayo inaweza kupatikana kutokana na kufuga ndege huyu na vilevile bei ya bidhaa hii imeendelea kuwa juu sana kiasi kwamba hivi kweli bei hizi za bidhaa hii zina uhalisia kiasi gani. Na kwa kuwa ni kitu kipya katika jamii yetu na mara nyingi watu wanataka kuchukua nafasi ambayo itakuwa rahisi na kuleta hela nyingi kwa mara moja lakini ukweli kuhusu utajiri unabaki pale pale kuwa inachukuwa muda na katika kuchukua muda watu wengi wanaachwa wakishangaa na wengine kuona kama aina fulani ya utapeli.

Leo nimeamua kuweka number kama unataka kufanya ufugaji huu kwa muda mrefu lazima kwanza uangalie uhalisia wake kwa kina na kuona kama bado unahitaji kujiuliza hivi kama bei za bidhaa hizi zitashuka zaidi ya nusu utaweza kuendelea kuwa na faida na kwa kiasi gani unaweza kuhimili kuwekeza katika biashara hii kama hakutakuwa na nini malengo na makusudio yako ukichaweka na kujua hilo ndio uingie kwenye shughuli hii. Kwa hiyo kwa kukusaidia nimejaribu kuweka mahesabu hayo kwenye excel sheet ambayo itaweza kukuonyesha faida unayoweza kupata na kwa mahesabu ya kware 500 unaweza kupata faida ya wastani wa Tshs millioni moja kwa mwezi kwa hiyo unaweza kushusha kutokana na kiasi unachoweza ingawa unavyoenda chini inaweza kuwa chini zaidi lakini kwa kware 100 inaweza kukupa kati ya laki moja hivi kwa mwezi .

angalia mahesabu hapo chini na kama unaswali unaweza kuniuliza na kama uengependa kujipatia kware na bidhaa zake unaweza kutupigia 0788-318671 au tembelea page yetu @ www.ulimwenguwakware.blogspot.com

MCHANGANUO WA GHARAMA YA KUFUGA KWARE
[TABLE="class: grid, width: 800, align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Description/ Maelezo[/TD]
[TD]IDADI (Quantity)[/TD]
[TD]KIASI (Amount)[/TD]
[TD]JUMLA (Total)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1
[/TD]
[TD]Gharama ya kununua kware 300 wa wiki moja[/TD]
[TD] 520 [/TD]
[TD] 3,500 [/TD]
[TD] 1,820,000 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2[/TD]
[TD]Chakula kwa muda wa miaka miwili na nusu9 Kware hula gram 30 kwa siku kware 500 hula kilo 15[/TD]
[TD] 13,800 [/TD]
[TD] 160 [/TD]
[TD] 2,208,000 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3[/TD]
[TD]Madawa na utaalamu matumizi ya wiki[/TD]
[TD] 130 [/TD]
[TD] 10,000 [/TD]
[TD] 1,300,000 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5[/TD]
[TD]Ujenzi wa banda la kukaa ngazi tatu mita 3 kwa 1.5[/TD]
[TD] 1 [/TD]
[TD] 750,000 [/TD]
[TD] 750,000 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6[/TD]
[TD]Gharama za usimazi na wafanyakazi kwa miezi 30[/TD]
[TD] 30 [/TD]
[TD] 500,000 [/TD]
[TD] 15,000,000 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]7[/TD]
[TD]Dharura na mengineyo na gharama ya masoko 20% ya gharama zote juu[/TD]
[TD] 1 [/TD]
[TD] 1,215,600 [/TD]
[TD] 1,215,600 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Jumla ya matumizi[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD] 22,293,600 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Mapato[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Kware huanza kutanga vyema baada ya wiki nane na utakuwa na kware 400 wanaotaga 100 vijogoo na wanataga kwa siku 215 to 250 kwa mwaka kwa miaka miwili na nusu kware mmoja atatupa mayai (215*2.5=538) kwa kware wetu 400*538[/TD]
[TD] 215,000 [/TD]
[TD] 250 [/TD]
[TD] 53,750,000 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Baada ya miaka miwili uza kware wako wote [/TD]
[TD] 450 [/TD]
[TD] 3,000 [/TD]
[TD] 1,350,000 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Ukipata mahali pa kuuza mbolea vile vile itakuwa sawa ila kwenye hili sitaiweka[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Jumla ya mapato[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD] 55,100,000 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Faida tarajiwa kwa miaka miwili[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD] 32,806,400 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Faida kwa mwezi[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD] 1,093,547 [/TD]
[/TR]
[/TABLE]


*Angalizo mahesabu haya yamewekwa yakiassume kuwa kware asilimia 4 tu ndio watakufa na inawezekana kwenye hali halisi ikawa tofauti
 

Attachments

Maelezo mazuri japokuwa mimi naingiza over 2.4mil kila mwezi kwa uuzaji wa mayai ya kwale, nina kwale 360 majike 300 na madume 60 nilinunua wakiwa na week tano kutoka Kwale Bora Ltd, Kama unahitaji kwale wasiliana na KWALE BORA LTD hawa jamaa ni wazalishaji bora wa vifaranga wa kwale, na wanatoa mafunzo ya ufugaji pamoja na majarida ya ufugaji kwale bure.

KWALE BORA LTD
TEL : 0654 163 784
EMAIL: kwalebora@gmail.com
 
Tatizo kila mtu anataka kufuga kwale sasa, sijui nani atakuwa mnunuzi sasa
 
Tanzania hata leo wakisema maboga yanamaliza ukimwi kila mtu atataka lima maboga. Watanzamia kwa kuvamia na kuiga biashara we wasikie tu
 
Yamoto band wameanzisha band, sasa kuna vikundi takribani vinne vimeanzisha band na vinaimba ka Yamoto band, hii ndo Tanzania.
 
Bora kufuga kuku wa kienyeji kwani hapa Dodoma Walaji ni wengi kuliko hayo
hiyo biashara ningepata mjuzi ningefurahi zaidi ya mayai ya Kwale
nasikia vifaranga vinatoka Mtwara kwa bei ya 1,500/ x 100 sawa na 150,000/
baada ya miezi 6 tayari kuku wanapatikana kwa ajili ya kula/kuchoma kwa bei ya 10,000 x vifaranga 100 sawa na 1,000,000
chakula na matibabu kwa mwezi 100,000/
mfanyakazi mpe 50,000/
Hujosi 700,000/ kwa mwezi
Naomba mwenye mawasiliano na hawa jamaa wa vifaranga wanijuze kwani mabanda tayari ninayoNingeweza kuwaingiza Kwale lakini Link za hawa jamaa hazifunguki na sina soko la mayai ya Kwale
 
Bora kufuga kuku wa kienyeji kwani hapa Dodoma Walaji ni wengi kuliko hayo
hiyo biashara ningepata mjuzi ningefurahi zaidi ya mayai ya Kwale
nasikia vifaranga vinatoka Mtwara kwa bei ya 1,500/ x 100 sawa na 150,000/
baada ya miezi 6 tayari kuku wanapatikana kwa ajili ya kula/kuchoma kwa bei ya 10,000 x vifaranga 100 sawa na 1,000,000
chakula na matibabu kwa mwezi 100,000/
mfanyakazi mpe 50,000/
Hujosi 700,000/ kwa mwezi
Naomba mwenye mawasiliano na hawa jamaa wa vifaranga wanijuze kwani mabanda tayari ninayoNingeweza kuwaingiza Kwale lakini Link za hawa jamaa hazifunguki na sina soko la mayai ya Kwale



Ukiwauza kwa 10000
Unapata hiyo Milioni Moja.

Matumizi
Chakula 100,000 kwa miezi 6 inakuwa 600,000
Mfanyakazi 50,000 kwa miezi 6 inakuwa 300,000
Hapo utapata 100,000 tu mwisho wa miezi 6.
Ukiondoa hela za kununua vifaranga unajikuta umeenda na negative 50,000 yaani hujapata faida. Na pia hao Vifaranga hawajatoto hivyo itabidi ununue wengine tena Negative 200000 jumla so kila siku utapata hasara. Bora ufugie huko uje kuuza Dar
 
Ukiwauza kwa 10000
Unapata hiyo Milioni Moja.
Matumizi
Chakula 100,000 kwa miezi 6 inakuwa 600,000
Mfanyakazi 50,000 kwa miezi 6 inakuwa 300,000

Hapo utapata 100,000 tu mwisho wa miezi 6.
Bora ufugie huko uje kuuza Dar
Mkuu nimekuelewa na asante sana kwa ufafanuzi
Lengo langu sio kuwa na kuku 100 tu mpaka wakue na kuwauza
Hata km ni Duka utafilisika, ni lazima niwe na batch km 6 au 4 kila mwezi naingiza mzigo kwenye Banda jipya
Hapo kwenye RED
ni kwambahicho chakula ni cha mizunguko kwa wote na huyo mfanyakazi atafanya kazi ya kuku 600

Nijirudi mkuu nitakuja na hayoa mahesabu ili unisaidie na soko huko Dar maana wanasema River sude Ubungo wanakula sana kuku wetu wa Dodoma na Singida

Nimepata msaada hapa:-
https://www.jamiiforums.com/ujasiri...wongozo-kwa-wafugaji-wa-kuku-wa-kienyeji.html
https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/400316-zijue-mbinu-zangu-ufugaji-kuku-wa-kienyeji.html
https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/835515-vifaranga-vya-kuku-wa-kienyeji-wauzwa.html
https://www.jamiiforums.com/ujasiri...ugaji-wa-kuku-wa-kienyeji-na-masoko-yake.html
 
ufugaji sio mbaya ila napenda kila anayefuga aielewe biashara hiyo kwa undani ili aweze kwenda kwa muda mrefu na ajiandae na kama itakuwa sio nzuri

Tatizo kila mtu anataka kufuga kwale sasa, sijui nani atakuwa mnunuzi sasa
 
Mbona TFDA wamesem mayia ya kwale hayana protini yoyote kama inavyodaiwa na sisi tunaofuga kwale?
 
Kitu ambacho TFDA wamekaataa na mimi naungana nao mkono ni kuyaita mayai ya kware kuwa ni dawa(potency) yaani kama mtu uumwe kitu ule mayai ya kware kama kitu cha kuponyesha mayai ya kware ni chakula ila kina nutrients nyingi sio dawa kwa mtu yeyote anayejua process ya kitu kuwa dawa huwezi kumweleza kuwa hii ni dawa ila ni chakula full stop.

Mbona TFDA wamesem mayia ya kwale hayana protini yoyote kama inavyodaiwa na sisi tunaofuga kwale?
 
Hivi jamani mayai ya kware huatamiwa kwa muda gani na unaweza kumwekea kuku na kuyatotoa na mwisho huwa wanazoea kama kuku au kanga
 
Mayai ya kware yanatamiwa kwa siku 18 ila tumia machine ukiwapa kuku basi hakikisha
hawatoki nje maana huruka kama ndege

Hivi jamani mayai ya kware huatamiwa kwa muda gani na unaweza kumwekea kuku na kuyatotoa na mwisho huwa wanazoea kama kuku au kanga
 
Back
Top Bottom