ukweli wa kisayansi kuhusu mambo yaliyoandikwa katika biblia

ukweli wa kisayansi kuhusu mambo yaliyoandikwa katika biblia

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,278
Reaction score
956
Mathew Fontaine Maury kwa wale waliosoma mambo ya history of marine Navigation Mnaweza mkawa mlimsoma , kwani ndiye Mtu wa kwanza akugundua " path of the sea current " yaani Mikondo ya bahari

Bahari kwa kawaida ina mikondo yake au kwa lugha nyingine baharini kuna njia ikifuatwa na meli vizuri unafika salama .

Mathew Fontaine Maury, alifikia ugunduzi huu kwa kusoma biblia zaburi ya 8:8 inasema " ndege wa angani na samaki wa baharini na kila kipitacho njia za baharini"

Baada ya kusoma biblia alitaka kujua hiyo njia za baharini ni zipi haswa. Alivyopata ajira yake katika america navy vessel, meli za jeshi la America alianza utafiti wake.

Alifanya utafiti kuhusu hiyo njia baharini kwa kuchunguza mawimbi yote ya bahari na pepo ( oceans sea current)

Mathew Fontaine Maury aliendelea na tafiti zake hata akakutana na neno la biblia Muhubiri 1:6 inasema " upepo huvuma kusi , hugeuka kuwa kaskazi, hugeuka daima katika mwendo wake , na upepo huyarudia mazunguko yake"

Mathew Maury baada ya kuona ukweli wa biblia umekuwa sawa sawa na tafiti yake , alizidi kusonga mbele hata kutengeneza charts ya mawimbi ya bahari , ambayo imekuwa ni Msaada mkubwa sana kwa mabaharia wengi ( marine navigator).

Meli zote duniani huwa zinafuata michoro yake mpaka Leo ingawa kuna maboresho tangu mwaka 1836. Ametoa chapisho la utafiti wake aliloliita " Theoretical and practical treatise of Navigation" na kikosi cha navy walichukua andiko lake kama andiko bora sana katika navigation system.

Ninachoweza kumaanisha katika article hii ni kuwa Mathew Maury aligundua haya kupitia neno la Mungu ( biblia) akafanyia kazi na hii ndiyo VISION (maono) . kama pioneer wa oceanography alisema bahari ni kitu kinachozunguka katika Mfumo Fulani , maana yake Yale ambayo wanasayansi wanayagundua , yalijulikana na Mungu tangu awali. Soma 1 nyakati 16:8-9

Leo wanasayansi wanatuambia kasi ya mwanga duniani inafifia siku kwa siku . ule mvutano wa dunian ( Magnetic field) unapungua badala ya kubaki palepale au kuongezeka . Dunia inashindwa kukaa kukaa katika muhimili wako ( NASA ame centre report).. Ozone layer angani inapungua ambayo inazuia mionzi ya jua isitudhuru sana .

Ukisoma zaburi ya 102:25-26. , utagundua Mungu anasema dunia itachakaa kama nguo , na kuchakaa kila mtu anakujua .

Watumishi wa Mungu wanaposema hizi ni nyakati za Mwisho wanamaanisha , na kwa kuwa ukombozi wa Mwanadamu ni hatua , Mimi nakubali with no doubt this is the end time.

Sayansi imeanza kukamata kile Mungu anasema kwa kasi ya ajabu .

Biblia siyo kitabu cha kisayansi ila ni ujumbe Mungu ametupa na sayansi hiyo ikielezewa humo na vyote vilivyomo duniani vimeelezewa kama cosmology maswala ya anga , thermodynamic , kuganda kwa damu kwa watoto biblia inasisitiza watoto watahiriwe ndani ya siku 8 mwanzo 17:12, wanasayansi wamebaini ndani ya kipindi hicho damu ya watoto inawahi kuganda na kupona kidonda kwa haraka..ukisoma Yona 2:6 yona alivyoshushwa baharini , ni kweli baharini kuna Milima proof ni visiwa vya Ravillagigedos.

NASA(ame research centre) wamethibitisha ni kweli Mwanadamu anatokana na udongo , element nyingi za Mwanadamu zipo katika udongo pia.

Walawi 17:11 damu ni chanzo cha uhai , wanasayansi wamekubali andiko hili.

Mawingu yote yanafanywa na ocean evaporation muhubiri 1:7

Hydrological cycle Amos 9:6 ayoub 36:27-28.

Proof za kisayansi ni nyingi kuhusu maandiko ya biblia na zinaendelea be connected
 
Aseeh... Na kuna mengine wanasayansi bado hawajagundua... Ya Mungu mengi
 
Back
Top Bottom