Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,925
Nimeona niiweke hii kwa kuwa kulikuwa na maswali yaliulizwa hapa kuhusu nini hasa maana ya mtaala na madhumuni yake.
Na Profesa Hermes Mosha
Ukweli wa kuwepo, kutokuwepo mitalaa nchini - Makala - mwananchi.co.tz
Katika kikao cha Bunge kilichopita, kulizuka mjadala kama sekta ya elimu nchini ina mtalaa au la.
Kwa vile moshi kuhusu mjadala huu bado unaendelea kufuka, nimeona ni vyema nitoe ufafanuzi wa kitaalamu ili kuwaridhisha wote wenye dukuduku kuhusu ukweli wa jambo hilo.
Ili kuweza kuelewa vizuri mtalaa ni nini, ni lazima tuelewe tofauti zilizopo kati ya dira na falsafa ya taifa, sera ya elimu, mitalaa, mihtasari ya masomo, mpango wa kazi, na andalizi la somo, kwani dhana hizi zote zinarandana.
Dira ya Taifa hujumuisha matamshi ya kina kuhusu matarajio ya maono ya taifa, kuwa tunataka taifa la aina gani, tuseme ifikapo mwaka 2015. Pia inatamka bayana falsafa ya Taifa ni nini.
Mtu akichunguza kwa karibu Dira ya Taifa hadi kufikia mwaka 2025, ataona inatamka bayana kuwa falsafa ya Tanzania ni kuwa taifa ambalo wananchi wake wote wana maisha bora, kuna amani, utulivu, umoja, utawala bora, watu walioelimika na wanaoendelea kujielimisha, uchumi shindani unaoweza kuchochea ukuaji wa haraka na wa kudumu kwa manufaa ya wote.
Tanzania pia ina kusudio la kuwa taifa la watu wabunifu na lenye kutoa elimu bora kwa idadi kubwa ya watu wake, ili waweze kuwa na uwezo wa kuyatatua matatizo yanayoikabili nchi yao, kuwaletea maendeleo ya haraka na kuwa na uwezo wa ushindani barani Afrika na duniani.
Sambamba na Dira ya Taifa, sera ya elimu ya mwaka 1995, inatoa mwongozo wa jinsi elimu inavyoweza kuwa kichocheo cha kutekeleza dira hiyo, kwa kuoanisha na kubainisha mfumo wa elimu, mipango na utekelezaji wake kwa kuhakikisha kuna ongezekao la udahili, usawa, uwiano na ubora wa elimu inayotolewa kwa kila ngazi ya elimu.
Mtalaa ni nini?
Mara nyingi mitalaa hutokana na sera ya elimu. Neno mtalaa, linatokana na neno la Kilatini Currere au kukimbia. Katika taaluma ya elimu, neno hilo linamaanisha mpango wa mafunzo ambayo mwanafunzi anapaswa kupata ili awe mkamilifu katika ngazi fulani.
Hata kabla ya elimu hii ya shuleni, elimu yetu ya jadi ilikuwa na mtalaa wake katika ngazi mbalimbali kuhusu maarifa, stadi, maadili, maono na ujuzi ambayo anayepita mtalaa huo anapaswa awe amepata amalizapo mafunzo yale, ili aweze kuwa mtu anayejiamini, anayejituma na anayetoa mchango mkubwa katika sehemu ya kazi ama anapoishi.
Kwa ufupi, mtalaa unajumuisha yale yote ambayo mwanafunzi anapaswa kujifunza na kuyafahamu katika ngazi mbalimbali za elimu. Wataalamu wa elimu wameweza kubainisha aina tano muhimu za mitalaa.
Moja, mtalaa rasmi. Huu ni ule mtalaa unaoandaliwa na Wizara au vyuo vikuu kuhusu aina ya mafunzo yanayopaswa kutolewa katika ngazi husika. Viongozi, walimu wa shule, vyuo na taasisi wanapaswa, wayazingatie na wanafunzi wajifunze.
Mbili, mtalaa unaotundisha. Huu ni ule ambao mwalimu mmoja mmoja anaufundisha, ukizingatia changamoto za mazingira, ubora wa elimu yake, mtazamo juu ya wanafunzi na uhusiano wa kila siku.
Tatu, mtalaa anaojifunza mwanafunzi. Huu unatokana na jinsi wanafunzi wanavyoandaliwa na walimu ili waweze kujenga ari ya kuwa wasikivu, kuuliza au kutokuuliza maswali, kujifunza kuheshimiana au kutokuheshimiana. Hivyo mtaala anaojifunza mwanafunzi ni mpana zaidi wa yale anayofunzwa.
Nne, mtalaa unaotathminiwa. Hii ni sehemu ndogo tu ya mtalaa rasmi ambapo maswali yanatungwa kufuatana na ujuzi wa kutunga mitihani ya yule anayetahini. Japokuwa walimu na Baraza la Mitihani wanaweza kuhakikisha maswali yanatokana na vipengele mbalimbali na kutumia aina mbalimbali za maswali, mara nyingi ni sehemu ndogo tu ya mtalaa inayotahiniwa katika kuainisha ubora halisi wa mwanafunzi.
Tano,mtalaa usio bayana. Kuna mambo mengi muhimu ambayo mwanafunzi anajifunza shuleni ambayo hayako bayana kwenye mtalaa rasmi. Mwalimu Nyerere kwa mfano alisisitiza mambo ya utii, nidhamu, kujifumza na kujenga moyo wa kushirikiana. Haya ni mambo mema yanayokamilisha maisha ya mwanadamu, hayafundishwi lakini shule nzuri huyawekea mkazo.
Aidha, mtalaa wowote mzuri una sehemu kuu nne. Mosi, malengo ya elimu katika ngazi husika. Malengo haya yanatokana na sera ya elimu na kurudiwa kwenye mitalaa na mihtasari ya masomo.
Pili, idadi ya masomo na yapi yanapaswa kufundishwa katika ngazi mbalimbali. Mara nyingi hii hubainishwa na miongozo mbalimbali inayotoka kwa Kamishna wa Elimu kila kunapotokea uamuzi wa kuongeza au kupunguza masomo.
Suala kubwa hapa ni kwa nini tuwe na masomo kadhaa tangu darasa la kwanza, wakati huko nyuma miaka miwili ya mwanzoni ilitilia sana mkazo kwenye misingi ya K tatu yaani kusoma, kuandika na kuhesabu? Hapa ndipo tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu linapotokea.
Tatu ni mbinu za kufundishia ambazo zinaweza zikawa zinamtegemea mwalimu (teacher based) au zile zinazomlenga mwanafunzi (student based). Hizi hutenganisha au kuunganisha nadharia na vitendo.
Nne ni namna ya kutathmini, iwe kwa kutumia mtihani wa mwisho au kufikiria jumuisho la mazoezi, tabia na mitihani ya mwisho. Kila mbinu ina matatizo yake. Vitu vyote hivi vimebainishwa katika sekula mbalimbali na katika ngazi ya chuo kikuu, vipo katika kalenda za vyuo.
Kimsingi, mambo haya ndiyo yanawaongoza watunga mihtasari mbalimbali na watunga mitihani katika kazi zao.
Sambamba na mitalaa kuna mihtasari ya masomo. Hii huandaliwa kwa kila somo litakalofundishwa kama ilivyobainishwa kwenye mtalaa. Hupambanua mada muhimu, kiwango cha uwezo, malengo yanayotarajia kufikiwa, mada kuu na mada ndogo, mbinu zitakazotumika kufundishia, zana kufundishia, mbinu za kutathimini na idadi ya vipindi.
Mpango kazi. Ni mkakati wa kutekeleza mtalaa. Mara nyingi huandaliwa kwa mwaka mmoja, muhula au semista moja. Mpango kazi unapaswa uainishe malengo, mada, kazi na majukumu ya mwalimu na ya wanafunzi, zana za kufundishia na namna ya kupima kiwango cha uelewa. Hata hivyo, ufundishaji wa siku hadi siku unaongozwa na andalizi la somo.
Inaendelea chini