Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,745
- 11,267
Nikupe mfano, muagize mtu wa "kawaida" ambaye muonekano wake ni wa kawaida yaani asiwe kama ofisa flani hivi aende duka maarufu hapa Mwanza linanoitwa Mwanza Huduma: wanauza vifaa vya ujenzi anunue sementi, mabati, nk pale kuna mbinu mpya. Unapewa risiti halali kabisa ya TRA na unaambiwa ni ya kusafirishia mzigo ukiirudisha unapewa kiasi fulani cha pesa!. Risiti hiyo atatumia mtu mwingine kusafirishia mzigo (upo uwezekano hata hiyo risiti ameirudisha mteja mwingine) Nimemtaja Mwanza Huduma kama sampuli tu, maduka makubwa karibu yote hapo Mwanza wanazo mbinu zao!
Zipo mbinu nyingine tatu ila kwa kuanza ngoja tukupime wewe Waziri wa Fedha na TRA kama mtaweza hii nitakutajia nyingine ambazo TRA wao ndio "operators" wake" Watanzania tunapenda sana kulipa kodi ila majambazi wa serikali wanatukatisha tamaa.
Ijumaa Njema Waziri!