Mimi sio mtaalamu ila nakumbuka hata mini kabla sijazoea kula asali mara ya kwanza kula nilisikia tumbo linaniuma ila baada ya kuzoea na siku hizi ndio kama kilaji changu cha kila siku najisikia niko vizuri.
Wataalamu wanashauri kwa kuwa asali ni dawa ya vitu vingi ni vyema mtu akajizoesha kula asali kila siku asubuhi vijiko viwili na maji ya kunywa ya moto kabla hujala kitu chochote hii inasaidi tumbo lako kufanya(digestion) kazi vizuri. Kitu ambacho hata mimi nakubaliana nacho.
Hivyo nafikiria mtu kama hujazoea kula asali na mara unapoanza kula ukasikia maumivu ya tumbo pengine inaweza ikawa ni viashiria kuwa tumbo lako haliko safi kutokana na kula vitu vingi hivyo unaweza ukawa una uchafu tumboni, minyoo n.k. hivyo ile asali inavyoshuka kwa kuwa ni dawa inaenda kutibua hivyo vilivyokuwa vimelala kwa sababu kama mtu unajifuatilia mwenye yale maumivu ya tumbo huwa yanachukua muda mfupi then yanaacha ila utakapoendelea kula asali kila siku hiyo hali ya maumivu utakuta imetoweka ndio kusema kama ni uchafu umesafishwa. na then utajikuta unakuwa ni rafiki mkubwa wa asali hutamani siku ipite hujaonja hata kijiko kimoja.
Jamani haya ni mafikirio yangu tu ila pengine kuna sababu nyingine wajuzi watujuvye.