Ulaji wa chips umetajwa kuwa hatari kwa afya ya binadamu

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,267
Reaction score
29,917
Kama unapenda kula chips tafadhali soma hapa:-

Ulaji wa chips umetajwa kuwa hatari kwa afya ya binadamu, kwani husababisha maradhi mengi yasiyo ya kuambukiza hasa figo, moyo , shinikizo la damu,kisukari na saratani za aina zote.

Sahani moja ya chips kavu huwa na mafuta yanayokaribia nusu kikombe cha chai ambayo ni sawa na ujazo wa mililita 250.

Kwahiyo walaji wengi wa chips wapo katika hatari ya kutengeneza sumu kwenye miili yao bila kujua.

Utafiti unaonyesha watu wengi hupendelea kula chips mayai, kuku, soseji au hata kwa mishikaki maana yake ni kwamba kiwango hicho cha mafuta huzidi kwa sababu na vyenyewe huwa vumekaangwa.

Jambo la kusikitisha ni kwamba wafanyabiashara wengi wamekuwa hawazingatii umuhimu wa kutumia mafuta mara moja katika kukaanga vitu hivyo.

Wengi huwa wanapikia mafuta kwa zaidi ya mara mbili na hivyo kuzidisha hatari zaidi.

“wanazidisha hatari kwa sababu… kawaida mafuta yanapaswa kupikiwa mara moja. Kadri unavyounguza mafuta ndivyo ambavyo ule mfumo wa mafuta masafi ambayo yanatakiwa kwa mwili wa mwanadamu unabadilika na kuwa machafu, maana yake ni kwamba unapopikia mafuta zaidi ya mara mbili tayari yanakuwa yametengeneza sumu ambayo haitakiwi mwilini ,”


Mafuta ambayo yametumika kukaangia vyakula zaidi ya mara mbili hubadilika na kutengeneza utando mweupe ambao huweza kuonekana iwapo mtu atayatazama kwa macho yake.

Ule utando mweupe utakaouona unatoa ishara kwamba mafuta hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu, lakini watu wanataka kufanya biashara hivyo huendelea kuyatumia bila kujali au pengine kutokujua kwamba wanaziweka afya za walaji katika hatari ya kupata magonjwa .”

Pamoja na kiwango hicho cha mafuta ambacho huingia mwilini kwa ulaji wa sahani moja pekee ya chipsi kavu, mlaji hula chumvi nyingi iliyopo ndani ya nyanya maalumu iliyosagwa (tomato).

Tomato sauce jinsi ilivyotengenezwa ina chumvi nyingi, sasa umekula mafuta mengi jumlisha na hiyo chumvi nyingi na ninavyofahamu walaji wengi wa chipsi hupendelea kushushia na kinywaji chenye sukari nyingi maana yake unakuwa umetengeneza sumu ndani ya mwili wako.

Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wagonjwa wanaougua magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza nchini inaongezeka.hatari hii inaweza kuepukwa iwapo watu watazingatia ulaji unaofaa.

Wengi hatuzingatii ulaji wa chakula bora, tunakula mradi tule na hatuzingatii kupima afya zetu.wakati umefika tunapaswa tubadilike kwa sababu wagonjwa wanaongezeka.

Utafiti unaonyesha kati ya watu 100 wenye umri wa kati ya miaka 25 na kuendelea,tisa kati yao tayari wanaugua ugonjwa wa kisukari huku wawili wakiwa hawajijui kuwa wana maradhi hayo.

Kila mwaka duniani watu milioni 12 hugundulika kuwa wana saratani ,na asilimia 60% ya magonjwa ya saratani yanasababishwa na mfumo mbovu wa maisha hasa ulaji usiofaa.

Wenzetu wazungu ni wajanja sio kwamba hawali chips, wanakula lakini wanazingatia ‘menu’ ya sahani wanayokula.kwamba inakuwa na viazi kidogo, mbogamboga nyingi na matunda .sisi kwetu ni kinyume kabisa watu wanapenda tomato sauce kwa wingi.

Ulaji wa mbogamboga ni jambo la msingi kwani huenda kusaidia kurahisisha mfumo wa umeng’enywaji wa chakula tumboni.


Take Care
 
Sahani moja ya chips ina mafuta 250ml hayo mafuta ndio yale wanakaangia kwa chips vumbi zetu huwa wanakaanga gunia kadhaa za viazi kwa siku na mafuta haya huwa wnaweza kuyatumia siku kadhaa bila kubadilisha.

Sasa anajiuliza iwapo kila sahani ingekuwa inatoka na nusu kikombe si wangekuwa wanatumia pipa zima? imagine kuna sahani ngapi za chips (kipimo cha wanaume wa Dar) kwenye gunia moja?
 
Ndiyo maana siku hizi mtu mnaweza kuwa naye,baadaye ukasikia amefariki,nadhani ni aina ya vyakula pia na mitindo ya maisha yetu ila kwa chipsi wengi wataathirika maana hata mgonjwa ambaye hana apapetaiti chipsi huwa hazikatai
 
Tuanze kula chips za kuchoma wakuu tuepukane na madhara ya mafuta
 
Umenena vema, na umetaja vitu vya msingi sana kwa afya zetu. Kuna matatizo kadhaa pale unapoleta hoja kama hii yako, unaposema tafiti nyingi au takwimu zinaonyesha bila kuzitaja hizo tafiti au chanzo cha takwimu unazozitamka kirahisirahisi inanipa shida kuamini kama unachokiandika unakielewa au unababaisha.

Please onyesha ushahidi wa tafiti na takwimu unazozitaja (Ni zipi, za lini na zilifanyika wapi?) hapo ndipo hoja inakuwa na nguvu na yeyote anaweza kurejea akajiridhisha. Mfano unaposema ulaji wa chips kama chanzo cha saratani zote ingefaa uweke rejea (source ya hicho ulichokisema) vinginevyo hoja yako ni nyepesi kama hoja ya kijiweni tu.
 




Wanaume wa dar mpooooo hahhhhhaahahah cos ndo vyakula vyenu ndo ivoooo mliowengiii but all in all thenx for reminding us brooh jah bless you!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…