Kaifanyie service maeneo yote muhimu yanayorelate na ulaji wa mafuta.
1.Badili tairi kama zimekwisha na uweke upepo kwa usahihi.
2. Badili plugs zote nne. Weka mpya. Soma user manual ya hiyo gari utaona kiwango cha umeme pendekezwa cha aina ya plug ya kuweka.
3. Badili air cleaner weka mpya kama ya zamani inaonesha kuwa haipo kwenye hali nzuri.
4. Tazama kama MAF sensor ipo sawa. Tazama na sensor nyingine kama zipo sawa kama oxygen sensor.
5. Weka engine oil sahihi ya engine ya hiyo gari. Tazama user manual utaona wameandika.
6. Unapokuwa unaendesha gari kuwa makini na uchocheaji wako wa mafuta. Kuna ile unaondoka sehemu unakanyaga kwa nguvu ili gari ikimbie hiyo sio sawa. Unatakiwa ukanyage taratibu gari itakuwa inakwambia yenyewe uongeze kukanyaga kulinagana na power inavyoongezeka katika engine na gear zinavyopanda.