Ulaji wa maini!

leipzig

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
2,766
Reaction score
1,708
Naona hapa ndio nitapata muafaka,nimepata kusikia utumiaji wa maini ya wanyama kama mlo una madhara kwa binadamu,je hii ni kweli? Huko nyuma ilikuwa ukimuwekea mpenzi wako order ya maini buchani ndio unaonekana kwa mpenzi wako umetimia.
 
Hakuna ukweli ni ya white bear. Wale polar bear ndo sumu ya vitamin A ya hatari unakufa hapo hapo
 
maini yanafaida nyingi sana tena sana hasa kwa waliopungukiwa damu inachohoea erthropoiesis.. kula maini kwa afya yako..
 
Naona hapa ndio nitapata muafaka,nimepata kusikia utumiaji wa maini ya wanyama kama mlo una madhara kwa binadamu,je hii ni kweli? Huko nyuma ilikuwa ukimuwekea mpenzi wako order ya maini buchani ndio unaonekana kwa mpenzi wako umetimia.

Mimi nikiwa shule kidato cha pili, nilifundishwa na mwalimu wa biology kwamba ukila maini ya mnyama /ng'ombe alieathiriwa na wadudu waitwao ''Liver flukes" unahatari ya kupata maambukizo ya ugonjwa wa ini iwapo maini hayo hayajapikwa vizuri......ngoja wataalam waje kutuhabarisha...
 
Naona hapa ndio nitapata muafaka,nimepata kusikia utumiaji wa maini ya wanyama kama mlo una madhara kwa binadamu,je hii ni kweli? Huko nyuma ilikuwa ukimuwekea mpenzi wako order ya maini buchani ndio unaonekana kwa mpenzi wako umetimia.

Maini yanakuwa na madhara endapo Ng'ombe,mbuzi au mnyama yeyote unayekula maini yake alikuwa na ugonjwa na ni kwasababu mara nyingi mnyama akiumwa maini yake huwa yanaharibika kiurahisi.

ILA kama huyo mnyama haumwi....Hakuna sehemu nzuri ya ng'ombe tamu na healthy kama maini na moyo.
 
ILA kama huyo mnyama haumwi....Hakuna sehemu nzuri ya ng'ombe tamu na healthy kama maini na moyo.

Kwenye utamu ni kweli...tena ukiongezea na figo, acha kabisa.

Ila kuhusu afya ngoja wadau waendelee kufunguka japo hata wanyama wa porini wanaokula nyama huwa naona wakifanikisha windo huwa wanaanza na vitu vya tumboni...

Inawezekana kweli vikawa na afya maana wanyama huwa hawa bahatishi na kula kwa tamaa kama sie.... kila wanachokula kina umuhimu na sio sombasomba tu ili kujaza tumbo kama yule mp wetu wa kule ziwani mpakani.
 
maini yanafaida nyingi sana tena sana hasa kwa waliopungukiwa damu inachohoea erthropoiesis.. kula maini kwa afya yako..

Mkuu nahisi kuna kitu cha muhimu unataka kufunguka ila umesema kwa uchache. Unaonaje ukiongeza maelezo kama hutajali

Maana mimi niliacha kula maini baada ya kuambiwa si salama kwa afya zetu
 
Shida wanyama tunaouziwa mjini si wote wana afya njema. Hivyo ulaji wa maini nao unaweza usiwe salama haswa utakapoishia kula mnyama aliyekuwa akiumwa na kupewa madawa makali kumtibu. Tukumbuke wanyama pia hutibiwa na dawa ambazo ni kali na zenye madhara zinapoingia kwenye miili ya binadamu
 
Navyopenda chapati maini duh sijui kama naweza yaacha kuyala
 
Mkuu nahisi kuna kitu cha muhimu unataka kufunguka ila umesema kwa uchache. Unaonaje ukiongeza maelezo kama hutajali

Maana mimi niliacha kula maini baada ya kuambiwa si salama kwa afya zetu

Sawa kuna mengi ila nilikua na haraka... iko hivi,,
Maini ndipo sehemu ambapo Iron toka kwenye breakdown ya Red blood cell hutuzwa hivo, maini ni chanzo kikubwa cha iron ambayo husaidia katika uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu.
Maini pia ni chanzo kikubwa cha folate, Maini ni chanzo kizuri sana cha Protein kwa mwili wako, Maini pia yana Vitamini A kwa kiwaango kikubwa sana pia fat soluble Vitaminis, Maini ni chanzo cha Vitamini B12 na nyinginezo.. Maini pia yana madini kama Zinc na Copper..
MAINI YANA MADHARA KAMA MNYAMA ALIKUA AMEATHIRIKA NA FLUKES NA HAYAKUPIKWA NA KUIVA IPASAVYO...

ILA,, ni vema kupata mlo wa Maini walau mara moja kwa wiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…