Ulaji wa nyani Tanzania watishia utalii Morogoro

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
VITENDO vya ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa iliyopo Morogoro hususani uwindaji wa nyani wa kitoweo, unaweza kupunguza mapato yatokanayo na shughuli za utalii.

Kwa miaka mingi watalii na baadhi ya watafiti wamekuwa wakitembelea hifadhi hiyo kwa ajili ya kufanya utafiti na kujionea makundi 11 ya nyani wa aina mbalimbali wakiwamo pekee aina ya Sanje Mangebay na Iringa Colabus wanaopatikana hifadhini humo.

Hayo yalisemwa juzi na Muikolojia Msaidizi wa Hifadhi ya Udzungwa, Christine Kibwe alipokuwa akizungumza kupitia makala za utalii zinazoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kurushwa na Kituo cha televisheni ya Taifa (TBC) juzi.

Alisema wanaendelea kukabiliana na changamoto ya kuwahifadhi nyani hao adimu kutokana na baadhi ya watu wanaowatumia kama kitoweo.

“Nyani hawa wa kipekee kabisa wanastahili kutunzwa na kulindwa vizuri kwa ajili ya kuliingizia taifa kipato zaidi,” alisema Kibwe na kuongeza:

“Jamii inayotuzunguka imekuwa ikiwatumia nyani kama kitoweo kwa hali hiyo kama hatutaweza kufuatilia kwa karibu basi wanaweza kusababisha kutoweka kwao,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Hifadhi hiyo, Hassan Nguluma alisema kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakipokea watalii kutoka nje badala ya wananchi waishio nchini.

“Watanzania hawana mwamko wa kutembelea na kujionea rasilimali walizojaaliwa na Mwenyezi Mungu, kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukipokea watalii kutoka nje ya nchi badala ya watalii wa ndani wazawa,” alisema.

Nguluma alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna aina mbili za nyani ambao hawapatikani sehemu nyingine duniani ambao ni Sanje Mangebay na Iringa Colabus.
ULAJI NYAMA YA NYANI WATISHIA UTALII
 
Huu sasa ni uwindaji haramu na hatari kwa utalii. Yaani hawana hamu tena na nyama ya swara.
 
mulisaaa njoo hapa uone venye nyani kitoeo huko bongo😀😀😀😀Mimi nasema wabongo hangaikeni na kwenyu kablaje mtwambie ya kwetu😀😀😀😀😀
 
Huyo mwenye nywele nyekundu ndio Iringa Colabus na huyo mwingine ndio Sanje Mangebay ,only in Tanzania..
 
Mbona hawaleti appetite buana? 😀
Hakuna MTU anakula hao nyani ila ukweli ni ujuma za baadhi ya viongozi na wageni wana wateka na kuwauza nchi za ulaya kisha wanasingizia wananchi
 
Hakuna MTU anakula hao nyani ila ukweli ni ujuma za baadhi ya viongozi na wageni wana wateka na kuwauza nchi za ulaya kisha wanasingizia wananchi
Dah masikini mwananchi hana mtetezi.
 
Dah masikini mwananchi hana mtetezi.
Wanaleta porojo za kusingizia wananchi kula nyani ili magufuli asiwatumbue kwa hizo biashara chafu wanazo fanya kawaida wazungu huwa wa kwanza kutengeneza video za wanyama poli wanaopotea duniani Kwa kuliwa na wanadamu huko vijijini
 
kumbe hawa pia wanamwaga mate wanapomwona nyani mtini😀😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…