Nakumbuka bagia tu kati ya hizo, kijijini kwetu Ice-cream ilikuwa haijafika wakati huo, kwetu ilikuwa bakuli la kunde, muda wa mapumziko kulikuwa na wamama wanauza bakuli la kunde na togwa. Hahahahahha, CCM inataka turudi tena huko?
Mkuu hapo naona umesahau, Ufuta Mabumunda Sambusa za viazi, Half keki, Kashata, Mihogo ya kukaanga aka misuba Kaukau, Ubuyu, Ubuyu wa unga. Mabungo, Mengine nimesahau nitaongezea nikikumbuka.