Ulaji wa Udongo, Sabuni na Karatasi wakati wa ujauzito

Ulaji wa Udongo, Sabuni na Karatasi wakati wa ujauzito

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Pengine umewahi kuwaza kwa nini baadhi ya wanawake wajawazito hupenda sana kula udongo, barafu, magodoro, nguo, sabuni, karatasi au vitu vingine visivyo chakula? Kitendo hiki kitaalamu huitwa Pica.

Husababishwa na uwepo wa upungufu mkubwa wa madini ya chuma ambayo hupelekea kutokea kwa tatizo la upungufu wa damu.

Tatizo hili linaweza pia kusababishwa na upungufu wa madini ya zinc, aina mbalimbali za vitamini B au hata changamoto zingine zinazohitaji uchunguzi wa haraka wa daktari.

Wajawazito hushauriwa kutumia mlo bora pamoja na kupata virutubisho vyenye utajiri wa madini ya chuma na asidi za foliki (FEFO), zinc pamoja na aina mbalimbali za vitamini B ili kujikinga na changamoto hii.

Aidha, ni muhimu kufika hospitalini mapema kwa uchunguzi na ushauri ili kupata msaada wa haraka ikiwa tatizo hili litakuwa limesababishwa na mambo mengine yenye kuashiria uwepo wa hatari kubwa kwa afya.

Chanzo: Healthline
 
Mimi sina mimba lakini nakula sana udongo yani nakula kama mkate hakuna siku sijalal je nifanyeje niweze kuacha nimechoshwa na hii hali Kila nikijaribu kuacha nashindwa 😔.
 
Nilikua nakula sana sabuni adi mdomo unawasha ila siwezi kukaa bila kula kumbe ni upungufu wa madini
 
Back
Top Bottom