Ulanzi hauwezi kutumika kuendeshea magari?

Ulanzi hauwezi kutumika kuendeshea magari?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wakuu nchi kama Brazil sehemu kubwa ya magari yake yanatumia pombe kama nishati. Mengine yanatumia mchanganyiko wa mafuta na pombe. Wamarekani nao hawako nyuma, hawa pombe yao inatokana na mahindi. Pombe huko Brazili inatokana na miwa.

Na kiukweli future ya nishati ya magari ni pombe. Kuna utafiti unaendelea wa kutengeneza pombe kutokana na cellulose. Cellulose ndiyo inaunda miti, majani, yaani sehemu kubwa ya mimea ni cellulose. Sasa hapa maana yake mmea wote unageuzwa pombe! Inatoka pombe nyingi sana. Lakini utafiti kuhusu hili bado unaendelea.

Sasa huku kwetu Mungu katubariki, ni mianzi ya Africa pekee ndiyo inatoa pombe. Je, hatuwezi kutumia pombe hiyo kwa kuifanyia distillation ili tuendeshee magari?

Pombe ya mahindi au miwa ni hadi mazao yakomae na uvune, ila pombe ya ulanzi unapata kila siku wakati wa majira ya mvua. Ukipiga hesabu kwa mwaka unaweza kuta ekari ya ulanzi inazalisha pombe nyingi kuliko ekari ya mahindi au miwa.

Suala la kuendesha magari kwa ulanzi linawezekana? Changamoto gani unaziona?
 
Back
Top Bottom