CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,872
- 9,263
Tatizo la watanzania ni ujinga. Siyo wakulima tu ila hata wafanyakazi wa aina zote. Hawajitambui.Ukiangalia maandamano ya Wakulima Ulaya yana fikirisha sana na kujikuta nawaza kama tuna lima huku Africa au tuna tania tu.
Ulaya wakulima wana nguvu mno, kaisi kwamba sisi tunaonekana tuna cheza tu, na Wakulima sio tu wana nguvu pia wanaogopewa sana na sio Ulaya tu hata Asia nchi kama India mwaka jana au juzi kulikuwa na movement moja ya Wakulima wa India, ile movement ilifanya Serikali ya India inyoshe mikono juu.
Ulaya pia EU inaelekea kusalimu amri kwa wakulima, wakulima wanauwezi wa kuangusha Serikali.
Tanganyika hii ni haiwezekani, hatuwezi hata robo ya movement za wakulima Wazungu huko nje na haitakaa itokee hata kufikia robo ya nguvu zao.
View attachment 2893729
Tatizo la watanzania ni ujinga. Siyo wakulima tu ila hata wafanyakazi wa aina zote. Hawajitambui.
Narudia na nitarudia. Tatizo ni letu watanzania. Kwa nini? Mfumo ni nani anauweka? Kwa nini wananchi kwa ujumla tusikatae huo mfumo? Tuache hao wakulima vijijini. Tanzania sasa hivi ina vijana wengi sana waliomaliza sekondari na vyuo. Kwa nini wasidai mabadiliko? Kuna kitu ambacho tunakiwa kukijua. Hata hiyo mifumo huko majuu haikujileta yenyewe. Ni kazi ya wananchi. Waliwakalia viongozi kooni. Kwanza nimekosea kusema ''waliwakalia''. Mpaka sasa hivi wanawakalia kooni. Ni kwa sababu haitangazwi tu lakini migomo ni kitu cha kawaida majuu.Tatizo ni MIFUMO ya kinchi
Hivi mwalimu wa msingi anayelipwa 400k au babu yako kule kijijini anayekuwa limited kulima eka mbili kwa jembe la mkono ni mjinga mkuu
Nchi kama USA ina wakulima 10% tu dhidi ya 80% kazi zingine wakati nchi zetu wakulima ni 80% ya wananchi wote
Ajabu ni kwamba 10% ya wakulima wa USA wanawalisha 90% wanashiba na kusaza hadi tunaletewa sisi misaada
Wakati huku kwetu 80% inashindwa kujilisha na iashindwa kulisha 20% ya wafanyakazi zingine hadi tununue kutoka kwa 10% ya wakulima wa USA
Hapa tatizo ni MFUMO
Mkulima wa USA anahitaji wafanyakazi 20 kulima ekari 100,000 wakati mkuliwa wa Tz anahitaji vibarua 200 kulima ekari 10 tu
Hakika🤣🤣🤣🤣🎶🎶Mkulima wa Tanzania hafaidiki, anayefaidika ni Dalali
Narudia na nitarudia. Tatizo ni letu watanzania. Kwa nini? Mfumo ni nani anauweka? Kwa nini wananchi kwa ujumla tusikatae huo mfumo? Tuache hao wakulima vijijini. Tanzania sasa hivi ina vijana wengi sana waliomaliza sekondari na vyuo. Kwa nini wasidai mabadiliko? Kuna kitu ambacho tunakiwa kukijua. Hata hiyo mifumo huko majuu haikujileta yenyewe. Ni kazi ya wananchi. Waliwakalia viongozi kooni. Kwanza nimekosea kusema ''waliwakalia''. Mpaka sasa hivi wanawakalia kooni. Ni kwa sababu haitangazwi tu lakini migomo ni kitu cha kawaida majuu.