Ulaya wanashindwaje kuezeka viwanja vyao?

Ulaya wanashindwaje kuezeka viwanja vyao?

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Nipo naangalia fainali ya capital one cup kati ya Chelsea na Tottenham na mvua imeanza kunyesha kipindi cha pili huku mashabiki wakiloana.. Naona manager wa Tottenham anahangaika kujifuta maji ya mvua kila mara. So mara ya kwanza kuona mvua ikinyesha uwanjani na wakati mwingine hadi mechi kulazimika kuahirishwa. Sasa najiuliza hawa wazungu pamoja na technology yote walionayo wanashindwaje kuezeka uwanja ili watazamaji uwanjani na makocha wasiloane? Au ni sheria ya FIFA?
 
mimi nahisi wakiezeka yafuatayo yatatokea.
joto litakua jingi na itabidi zitumike a.c ambazo zinaweza kuleta madhara kwa wachezaji (kibiologia) kwa sababu ule natural upepo haupatikani
hata kama kuna viwanja vimezibwa juu lakini plan yake tang mwanzo ilikua ni kuziba, sasa hatujui pengine kiwanja kikifungwa paa kuna space zinakuwepo kwa ajili ya kuruhusu hewa kupita.
sauti ya mashabiki itakua ni kubwa kupita kiasi ndani ya uwanja na tukianglia kuna baadhi ya viwanja vina space ndogo.
ni hayo tu kama wapo macivil engineer waje watueleze
 
Hamna cha Uconservative wala nini ni maswala ya fwedha tu! Hao Jamaa sasa hivi ni choka mbaya!

Kuweka roof sio kwasababu ya hela,ni design tu. Wembley ndio uwanja wa soccer namba moja duniani kwa gharama na uzuri lakini hauna complete roof,millennium stadium Cardiff ni wa gharama nafuu kuliko wembley na una complete roof!

http://www.therichest.com/sports/top-10-most-expensive-sports-stadiums-in-the-world/10/
 
Hivi kama wakizeeka kutakuwa na tofauti gani kati ya mpira wa indoor na wa nje?
 
si kama hawana uwezo ila hawaja amua tu wanaweza kutumia vitu ambavyo ni transparent just kuzuia tu mvua isipite kwa wakati ule mpira unapochezwa na wanaweza kutumia njia nyengine kwa ajili ya kupeleka hewa inside kwa mfano kuna hizi underground za treni zimechimbwa chini kwa chini na watu wanaongia ni wengi na hewa inapita kwa kutumia bomba zao special kwa ajili ya kupitisha hewa na hii ikifika mda itakua inawasumbua watalitafutia ufumbuzi kama walivyolitafutia ufumbuzi goal tecnology
 
Millennium stadium Cardiff unafunga roof,Wembley unafunga partially...its all about design

Wembley ndo unaoongelewa na mleta mada...unafunga partially hadi wapi kama juzi mpaka sehemu ya makocha na benchi walikuwa wanaloana mkuu?
 
Hamna cha Uconservative wala nini ni maswala ya fwedha tu! Hao Jamaa sasa hivi ni choka mbaya!


Vipi umetokea kijiji gani apa tanganyika?na baada ya kuja mjini mpira unaangalizia kwenye kibanda umiza kipi?

Uingereza na hispania ndo zina timu tajiri zaidi na zenye mapato makubwa zaisi duniani,man U,chelsea,arsenal.etc na kila siku unasikia wanavunja record za bids na mishahara minono kwa wachezaji...ni vipi wanashindwa kufunika viwanja vyao ka wakiamua? Unajua serikali ya uingereza inaingiza mapato kiasi gani from football?uo uchoka mbaya we unaongelea upi?ka uingereza ni choka mbaya unahisi uholanzi wana hali gani(ajax wana kilichofunikwa)

Hii sio sehemu ya kuleta story za vijiweni sisizo na mashiko wala evidences
 
Wembley ndo unaoongelewa na mleta mada...unafunga partially hadi wapi kama juzi mpaka sehemu ya makocha na benchi walikuwa wanaloana mkuu?

hadi wapi?? nenda kasome details za uwanja utajua.....nilichojibu hapa kuweka roof au kutoweka si pesa ni maamuzi tu kwasababu wembley umetengenezwa kwa pesa nyingi kuliko viwanja vyenye roof! kama wangetaka kuweka roof wasingeshindwa eti hawana pesa.
 
Patrickn ...
kuna Michezo ya aina mbili indoor games na outdoor games, Michezo ya indoor ni michezo ambayo inachezwa kwenye viwanja vilivyozibwa juu! Nadhani unaijua michezo hiyo. Soccer ni mojawapo ya outdoor game kama rugby. Na outdoor games ni michezo inayochezwa kwenye viwanja wazi "open air" ila washabiki wanaweza wakawa na kivuli ila sio kwenye pitch. Hata Qatar walitaka wajenge indoor stadia kwa ajili ya ku regulate joto, wakaambiwa haitakuwa football. Kwa uelewa wangu Amsterdam Arena ndio indoor stadium
 
Last edited by a moderator:
Kwa sababu mashabiki huwa hawaondoki wakati mvua inanyesha basi hawana sababu ya kuweka roof
 
Back
Top Bottom