Ule ni usaliti, kukata tamaa kwa wanachadema au kupuuzwa kwa uongozi wa juu wa CHADEMA na mipango yao mibovu kuhusu maandamano?

Ule ni usaliti, kukata tamaa kwa wanachadema au kupuuzwa kwa uongozi wa juu wa CHADEMA na mipango yao mibovu kuhusu maandamano?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Maana,
bilashaka yoyote, kwa umoja na uzalendo ule wa kiwango cha juu sana walionyesha wanaChadema, mashabiki wake na wananchi wasio na vyama, kugoma na kutokuthubutu kuitikia wito wa Chadema wa kuandamana, ni ishara ya wanachama wa chama hicho kuanza kuususia na kupuuzia mipango, maamuzi na matamko ya chama hicho yasiyo na tija yoyote kwa jamii.

wanachama wa Chadema wamekataa kabisa kuburuzwa na viongozi wasio na mawazo mapya na fikra mbdala, hasa kwenye mambo yenye viashiria vya fujo na uvunjifu wa amani.

Tangu asubuhi ya siku ya maandamano, jiji la Dar es salaam na viunga vyake lilikua shwari na tulivu sana.

Wafanyakazi, wanafunzi, wafanyabiashara na wenye pilika pilika mbalimbali za kila siku mjini, wakiendelea na shughuli zao kama kawaaida, kwa uhuru bila taharuki au kitisho chochote cha kiusalama.

Na, kwakua ulinzi ulikua umeimarishwa vizuri sana kila kona ya jiji, kila mwanainchi alikua na amani ya uhakika na usalama wa alikokua anakwenda au alichokua ana kifanya.

waTanzani walionyesha uzalendo na utiifu wa kiwango cha juu sana kwa Taifa na Jeshi la polisi nchini, na kuwapuuza waliokusudia kuchochea chuki, kuvuruga na kuhatarisha umoja, amani na utulivu wa wananchi.

Hata hivyo,
Licha ya usaliti huo wa kiwango cha juu sana wa kujielewa, wanachadema kwa umoja wao waliungana kikamilifu katika kupuuzia wito wa viongozi wao wa kuwalazimisha kushiriki maandamano yaliyopigwa marufuku na polisi..

Pamoja na hayo yote, ni dhahiri bado kunaonekana lipo fukuto la uhasama na mashindano ya chini kwa chini, baina ya viongozi waandamizi wa juu wa Chama hicho..

Kwa mfano,
chairman na vice chairman Taifa, bilashaka yoyote hawako sawa. Mathalani, Mwenyekiti akitokea kwenye medias na social medias kwajili ya kueleza au kutoa mrejesho wa jambo fulani la kichama, hazipiti siku3, makamu mwenyekiti nae anakuja na jambo jingine jipya kuzima trending na kukipoteza alichoibua chairman wake kwa makusudi kabisa..

kwa hali hii, chadema wanaweza kuambulia chochote kweli kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Kwa sasa CHADEMA wamechoka kabisa kuburuzwa na kulaghaiwa na sinema za Mbowe. Ndio maana waliamua kupuuza wito wake wa kuwataka waandamane.
 
Back
Top Bottom