Ulega Azindua AZAM SEA TAXI, Awataka Wavuvi Kutotupa Nyavu Hovyo

Ulega Azindua AZAM SEA TAXI, Awataka Wavuvi Kutotupa Nyavu Hovyo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amewataka wananchi wanaojishughulisha na uvuvi maeneo ya Kigamboni kutunza mazingira na kutotupa nyavu katika njia inayopita vivuko ili viweze kutoa huduma ya kuvusha wananchi kwa ufanisi na ubora.

WhatsApp Image 2025-01-23 at 17.32.10.jpeg
Ulega ametoa agizo hilo leo Januari 23,2025 jijini Dar es Salaam wakati akikagua na kuzindua vivuko viwili vitakavyofanya safari za Magogoni - Kigamboni vinavyomilikiwa na Kampuni ya Azam ambavyo vitapunguza adha ya usafiri kwa wakazi Dar es Salaam hususan wananchi wa maeneo ya Kigamboni.

“Naomba niwasisitize ambao wanatumia maeneo haya kufanya shughuli zao za uvuvi, ni vizuri tuwe na utaratibu wa kutazama maeneo haya [Kigamboni] ili shughuli zingine zisiingiliane na njia za vivuko kwa sababu vimekuwa vikipata changamoto na kuharibika”- amesema Ulega.

WhatsApp Image 2025-01-23 at 17.32.11.jpeg
Aidha Ulega amesema vivuko hivyo vitapunguza adha kwa wananchi wanaosubiria kivuko kwa zaidi ya saa moja na badala yake sasa watatumia dakika tano kuvuka huku kivuko kimoja kikiwa na uwezo wa kubeba abiria 200 - 250 kwa wakati mmoja.

“Mtanzania wa hapa Kigamboni aliyekuwa anakaa saa nzima akisubiri kivuko, historia inaandikwa hatatumia muda huo tena atakuwa yeye anasubiriwa na kivuko, kivuko kimoja kitakwenda kubeba mpaka watu 2500 kwa saa moja”- ameongeza Ulega.

Ulega amewahakikishia wananchi kuwa vivuko hivyo ni salama, vimekaguliwa na kupata Ithibati ya kuwasafirisha abiria na kuwataka TEMESA, TASAC na AZAM MARINE kuendelea kushirikiana kuhakikisha usalama wa wananchi wanaotumia vivuko unazingatiwa wakati wote.

WhatsApp Image 2025-01-23 at 17.32.13.jpeg
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso ameipongeza Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi katika kutoa huduma kwa wananchi, na kuiomba Kampuni ya Azam Marine kuwekeza katika maeneo mingine ikiwemo Ziwa Victoria ili waweze kupata wigo mpana wa kutoa huduma kwa wananchi.

“Ni vema Azam Marine waangalie na uwezekano wa uwekezaji ndani ya ziwa Victoria na tunahitaji kuwakuza hawa wawekezaji wa ndani na nikuombe Mheshimiwa Waziri tuhakikishe tunapopata fursa tutumie wakandarasi wa ndani kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yetu”.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema vivuko hivyo vitasaidia kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Kigamboni - Magogoni na jambo la kusingizia muda linakwenda kuisha.

WhatsApp Image 2025-01-23 at 17.32.13 (1).jpeg
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro Kilahala amesema kwa sasa Mv Kigamboni na Mv Magogoni vipo kwenye matengenezo makubwa hivyo kituo kimebaki na kivuko cha Mv Kazi ambapo katika kukabiliana na changamoto hiyo serikali imeingia ubia na Kampuni ya Azam Marine ili kutoa huduma ya kusafirisha abiria Magogoni - Kigamboni.

Ushirikiano wa TEMESA na AZAM Marine ambao unatarajiwa kuwa na Sea Taxi 8 utaboresha huduma katika eneo hilo ambalo huvusha takribani abiria 70,000 kwa siku.


WhatsApp Image 2025-01-23 at 17.32.15.jpeg
WhatsApp Image 2025-01-23 at 17.33.06.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-01-23 at 17.32.14.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-23 at 17.32.14.jpeg
    466.1 KB · Views: 5
23 Januari 2025

ADHA YA KUVUKA KIGAMBONI FERRY YAPATIWA UFUMBUZI, SEKTA BINAFSI YASHIRIKI KUWEKEZA


View: https://m.youtube.com/watch?v=1WsPIvt4m9c
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amewataka wananchi wanaojishughulisha na uvuvi maeneo ya Kigamboni kutunza mazingira na kutotupa nyavu katika njia inayopita vivuko ili viweze kutoa huduma ya kuvusha wananchi kwa ufanisi na ubora.

Waziri Ulega ametoa agizo hilo leo Januari 23,2025 jijini Dar es Salaam wakati akikagua na kuzindua vivuko viwili vitakavyofanya safari za Magogoni - Kigamboni vinavyomilikiwa na Kampuni ya Azam ambavyo vitapunguza adha ya usafiri kwa wakazi Dar es Salaam hususan wananchi wa maeneo ya Kigamboni.
 
Back
Top Bottom