Ulianza anzaje kumiliki Chombo cha usafiri?

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Kwa wale wenye usafiri mtupe mbinu, je mlianza anzaje kumiliki chombo chako cha usafiri?

Siku ya kwanza kumiliki ulijisikiaje?
 
Kwa wale wenye usafiri mtupe mbinu, je mlianza anzaje kumiliki chombo chako cha usafiri?

Siku ya kwanza kumiliki ulijisikiaje?
Nilirithi mkuu.Sikutoa hata jasho.Na kwa sababu nilijua kuendesha tangu kitambo nikajisikia poa tu.
 
Gari ni kitu rahisi sana kuwa nacho. Ni hela tu. Na siku hizi kununua si gharama, na spare parts zipo nyingi. Ila pia badala ya gari, wekeza kwanza kwa kiwanja na mjengo. Kama hauna assets nyingine za maana, gari itakurudisha nyuma tu.

Binafsi nilienda abroad nikiwa 18 years old. Nikanunua gari ya kwanza wakati hata kuendesha sijui vizuri. Nilijifunza siku moja tu kabla ya hapo.

Unajisikia vizuri kama wiki ya kwanza tu. Baada ya hapo gari unaichoka na haikupi raha kivile zaidi ya kuwa chombo cha usafiri tu.
 
Nilipita sehemu nikakuta wanauza vibaiskeli vingi,nikawaza hivi na hii corona nikinunua kibaiskeli, si nitakuwa nimeondokana na misongamano ya kwenye daladala kwenye trip fupifupi za mjini lakini nitakuwa nafanya mazoezi pia.

Nikaona inawezekana, nikamuuliza muuzaji bei akaniambia anauza laki mbili na ishirini, nikaomba punguzo tutakubaliana laki mbili nikamlipa nikaondoka na usafiri wangu. Hivyo tu.
 
Jamaa yangu alipata tatizo kubwa na la ghafla ikabidi aniuzie kwa bei ya kutupa kabisa.
Nikachomoa amount kwenye mtaji nikavuta chuma.
Simple 😂
 
Kwa wale wenye usafiri mtupe mbinu, je mlianza anzaje kumiliki chombo chako cha usafiri?

Siku ya kwanza kumiliki ulijisikiaje?
Unaanza kuwa na hela ya kutosha kununua ndio unaimiliki. Vinginevyo uhongwe au urithi.
 
NASHUKURU SANA KWA MUUMBA WA VYOTE MUNGU BABA KWA KUNIPATIA MIGUU HII BURE KABISA NA WALA SILIPII,ASHUKURIWE SANA
 
Picha ya hiyo baiskel tafadhari
 
Safi sana
 
Kiukweli bado sijamiliki, ila sijui kwa uoga huu kama ntaweza kudrive tena barabara za Dar hizi mambo mengi🤔 vipi siku nikinunua ndinga would you be my driver Zero IQ ?😂 joke
 
Siku yakwanza nilinunua tairi nikadunduliza hadi nikapata vitu vyote kasoro chassis nikaaa kama mwaka kumbe bwana bite haina chassis nilijichelewesha bure basi nikafunga vyombo huyo posta mpya!
 
Msema kweli mpenzi wa Mungu [emoji3][emoji3]
Hakika sitaki kusema namiliki ndinga kali wakati hata baiskeli sijawahi kumiliki, sina gari ila pia hata siku nikinunua naogopa kudrive😂 vipi wewe my Hommie una gari ngapi?🤪
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…