Ulianza kuendesha gari ukiwa na umri gani? Au mwaka gani?

Ulianza kuendesha gari ukiwa na umri gani? Au mwaka gani?

Behind the camera

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
315
Reaction score
756
Aisee.

Mimi mpaka sasa ni miaka 29 imeshanipotea katika umri wangu na sijui kuendesha sio gari tu hata pikipiki siwezi. Kwetu hatukuwa/hatuna gari labda baiskeli ya matairi mawili (Phoenix) Sikuwa na rafiki, jamaa Wala ndugu ambaye alikuwa na kipando chombo cha moto miongoni mwa vyombo vya moto.

Kwasasa, naona kuna umuhimu wa kujifunza udereva kwasababu naona nina uhitaji/umuhimu wa chombo cha moto (sio birika la kahawa lakini). Najua wewe /huyo/yule ni mtoto wa kishua gari ilikuwa home kwao (kwenu)

Swali: Ulijua/ulianza kuendesha gari ukiwa na umri gani na wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa na miaka 14, (Vya mwaka gani achana navyo kwanza)..........................
 
Ndio natafuta hela ya kwenda VETA pale kujifunza.

#Bagwell
 
Aisee.

Mi mpaka sasa Ni miaka 29 imeshanipotea katika umri wangu na sijui kuendesha sio gari tu hata piki piki siwezi.

Kwetu hatukuwa/hatuna gari labda baiskeli ya matairi mawili (Phoenix)

Sikuwa na rafiki, jamaa Wala ndugu ambaye alikuwa na kipando chombo cha Moto miongoni mwa vyombo vya moto.

Kwasasa

Naona Kuna umuhimu wa kujifunza udereva kwasababu naona Nina uhitaji/umuhimu wa chombo cha moto (sio birika la kahawa lakini)

Najua wewe /huyo/yule Ni mtoto wa kishua gari ilikuwa home kwao (kwenu)

Swali!

Ulijua/ulianza kuendesha gari ukiwa na umri gani na wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilianza kuendesha nikiwa na miaka 20.

Now nna 25

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa na miaka 14 baada kumaliza darasa la 7 mwaka 2004, kwa sasa nina miaka 29. Ila unaweza kuanza kujifunza basics kupitia mtandao wa YouTube kwa kuanzia kuna watu wengi sana wame-share ujuzi wao.

Just type how to drive a stick shift or automatic transmission car on YouTube. It's easier to learn how to drive a car than riding a bicycle.
 
Miaka 17 nikapata na leseni kabisa baada ya kuongea miaka miwili, nilipewa class D kipindi kile maleseni ya kitabu, ukitaka unaongea vizuri na mkuu wa askari wa barabarani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka 18.

Napendekeza leseni za udereva zitolewe kwa Watanzania wenye elimu ya kuanzia Diploma sababu kazi ya uendeshaji wa gari Barabarani unahitaji maamuzi ya haraka pale panapotokea chamgamoto.

Matusi hayaruhusiwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sijui hadi sasa mie ni chopa mwanzo mwisho (pikipiki) namiliki kibao cha mbuzi natamba nacho sana hahahaha?
 
Back
Top Bottom