Ulianzaje kusoma vitabu?

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari zenu wakuu,

Kama ilivyo kwa wa Tanzania wengine swala la kusoma vitabu ni gumu sana kwetu hasa vijana na mara nyingi wazee ndo wamekuwa na utaratibu huo.

Leo nataka ku share na nyinyi my love story iliyonipelekea kuanza kusoma vitabu.

Nilikuwa kwenye mahusiano na binti mmoja niliyefahamiana nae kipindi nipo chuo Ila Mimi nilimtangulia mwaka mmoja mbele alikuwa darasa la nyuma yangu

Nilimpenda na yeye alinipenda pia na tulishirikiana kwenye shida na matatizo kwa nyakati tofauti pindi mmoja wetu anapohitaji msaada wa haraka.

Nilifanikiwa kumaliza chuo huku yeye nikimuacha bado akiendelea kwani tulipishana mwaka mmoja Kama nilivyoelezea hapo awali,
Sasa balaa ndo lilianzia hapo baada ya kumaliza maana bado tulikuwa tuna mawasiliano mazuri tu na tulikuwa tumefika level ya kushirikishana hata Mambo yanayohusu familia zetu na kushauriana baadhi ya Mambo mbali mbali.

Mambo hayakuwa mazuri kiupande wangu baada ya kumaliza chuo kwani changamoto ya ajira ni janga la taifa kwa Sasa , Basi tukawa tunaendelea kuwasiliana na Yule mwanamke Ila alianza kubadilika ghafla Tena kwa mda mfupi sana ikawa nikiongea naye nikimuuliza kitu ana nijibu anachotaka hata kuonana kukawa kwa masharti magumu Sana ikafika mda mpaka ananiambia we utanisaidia Nini katika maisha yangu Bora kila mtu afanye mambo yake tu .

Basi kwa kuwa tulipendana sana na mabadiliko yalikuwa kwa mda mfupi ikabidi nitafute sababu zilizo mfanya abadilike vile, Basi baada ya uchunguzi wa mda mrefu nikaja kugundua jamaa mmoja wa TRA ndo anakula mzigo na ana mhudumia kwa kila kitu maana huyo jamaa alikuwa ame-post wako pamoja beach katika pozi za kimahaba aisee niliumia Sana kwa kweli kwani Yule jamaa ilikuwa anagharamia kweli kweli na mara ya mwisho huyo demu alifanya field hapo TRA nadhani ndo walikutana hapo.

Stress za kutoswa na msoto wa ajira na kupigiwa na jua Kali nikaangukia kwenye usomaji wa vitabu ili kupunguza machungu japo kidogo, na kitabu changu Cha Kwanza kusoma kilikuwa kinaitwa "UNDERSTAND THE PURPOSE AND POWER OF MEN" by Dr Myles Munroe baadae nikawa nasoma vitabu mbalimbali kama THINK AND GROW RICH-RICH DAD POOR DAD -HOW TO WIN FRIEND'S AND INFLUENCE PEOPLE na vingine vingi na mpaka sasa bado naendelea na utaratibu huo kwa Sasa nasoma "THE 100 START UP" but now I'm good mungu anasaidia kidogo si haba na tunaendelea kupambana na life japo ilinichukua mda kidogo kukaa sawa.

Wewe je ulianzaje zoezi hili gumu kwa watanzania wengi ? Karibuni wadau tujifunze wote .
 
Kuna mtu nilimuona anasoma kitabu Cha Robin Sharma kile Cha yule bwana mwanasheria nikakipenda tangu hapo nimekuwa msomaji
 
Nilienda kukaa kijijini hakuna umeme na sikuwa na marafiki maana kutafuta marafiki nami mgumu sana!.. najua na Wala sioni kama ni tatizo I now understand it kindly..
So option iliyokuwepo ni kusoma vitu na siwezi soma vitu vya darasani tu maana ndo nilikuwa secondary shuleni nisome na skani!!.. kutafuta vitabu vilikuwepo but vyengine vina kiingeleza kigumu siviwezi maana sielewi..😂
Nikaona isiwe tabu nikashika biblia ilikuwa biblia ya habari njema inavitabu vya agano la kale na vitabu vya deuterokanoni pamoja agano jipya.. nikaanza kabisa kile kitabu cha Mwanzo taratibu nikawa navutiwa zaidi na zaidi stori za wafalme,Mose,kina Ezekiel,elia n.k ilikuwa ndo dozi yangu kila siku lzm nisome especially siku za weekend mpk macho yalikuwa yananiuma!.. lkn nimo tu hata kutumwa nilikuwa naona nongwa! Maana kichwa kilikuwa kinatulia mpk raha you are only focus on one thing..
Mpk nikaja nikaimaliza!.. hapo ndo ikawa mwanzo wa kupenda kuanza kusoma na nikajua kuwa nahitaji kukua ktk lugha ya kiingeleza ili niweze kusoma pia vitabu vya kiingeleza so nikaanza ku focus kwenye ngeli mpk nikaweza.. hata vile nilivyovikimbia nikavichakaza na kuvielewa..

Kusoma raha sana.. ila unatakiwa ujue unasoma nini maana Kuna vitabu vya kukifunza na kukuelimisha na pia Kuna vitabu vya kukuburudisha..

Kusoma raha.. ..😜
 
1.Tangu nilipojua kusoma Baba alipenda kunipa magazeti nisome na nijaze crossword puzzles

2. Nilipokuwa Darasa la 4/9 yrs then.,ilikuwa ni lazima kusoma 'story books' fupi fupi japo mbili kila wiki....tangu hapo i read anything i lay my hands on.,
 
Vipo kuhusu huyo demu ? Story haijaisha
Mkuu mpaka leo kila mtu na maisha yake japo siku chache baada ya kuachana aliniambia yule hakuwa jamaa wake Ila alikuwa na ukaribu naye tu wa kikazi lakini sikurudi nyuma nilikuwa nampenda Sana Yule mwanamke sijui Kama nitakuja kupenda Kama vile maishani mwangu ila yote maisha mkuu japo ilinichukua mda ku accept the reality.
Kama bado Kuna kitu unataka kujua zaidi ya hapo be free mkuu kwa kuuliza Kama nimeelezea tofauti na ulichotaka kujua.
 
Sisi tusikilizao audiobooks, sijui bado tutaiwatwa wasomaji au tuko na category yetu separate.
 
Sisi tusikilizao audiobooks, sijui bado tutaiwatwa wasomaji au tuko na category yetu separate.
Ndo category moja mkuu hapo tofauti ni aina ya kupata taarifa tu Ila vyote ni vitabu mkuu tiririka
 
Asante mkuu pwilo kwa kuniruhusu kutiririka.


Mi nilianza 2018 tu hapo c mbali. Na niliamua tu nianze kusoma yani consciously niliamua mwenyewe. Hakukuwa na external factor yoyote iliyoni-drag in.

Before hapo nilikua na pdfs katika pc, ila kusoma page 5 mfurulizo ulikuwa tabu sana. Kwanza mazingira hayakuwa yanasupport. Ila baada yakugumia chaka ambalo liliniwezesha kupata Audiobooks tu, mambo yakawa mtelezo.

Kuanzia July 2018 to 2019 nilikua nmeshasoma vitabu zaidi ya 30 ( kwa mujibu wa mkuu pwilo).

So nikabadilika kdogo yani muda wote utanikuta nipo na earphones, Kwenye daladala, njiani nikitembea, pia hata nikiwa nimechill magetoni nakula zangu audiobooks.

Within few days kitabu Nilikuwa namaliza, vitabu vingi duration yake ni kuanzia 3hr na kuendelea. Kusikiliza 3hr straight haikuwa rahisi kulingana nashukuri ninazofanya. Hivyo kusikiliza 10mins to 1hr ndio ilikuwa ratiba.

Vitabu navyopenda ni
1.Business related books
2. Self-help books ila c sana
 
unatumia app gani kupata hzo audio books
 
Sawa mkuu which is your favorite book so far na ungependa kila mtu asome mi nashauri THINK AND GROW RICH one of the best book kwako MWALIMU kashasha
 
Baada ya kuangalia season Sanaa, nikaona huu ujinga. Yaani naangalia watu wanavyo pigana itanisaidia nini wakati hata pushapu zenyenye sipigi zaidi ya 2😃😃. Nikageugia vitabu.

Though nilikuwa napenda Sana kusoma tangu nikiwa mdogo, ila mapinduzi makubwa ni kipindi nikiwa chuo.

Jamani tusome vitabu vinasaidia hata kukabiliana na changamoto ndogondogo za kila siku.
 
Sawa mkuu which is your favorite book so far na ungependa kila mtu asome mi nashauri THINK AND GROW RICH one of the best book kwako MWALIMU kashasha

Kila kitabu nachopitia kwa kweli kwangu huwa ni favourite. Kwa sababu kila kimoja uwa na madini yake unique kabisa.

Ila na-recommend

1. How to win friends and influence people.
2. The Airbnb Story
3. Dark Psychology
4. Zero to One
5. 10X Rule
6. Men are from mars and women are from venus
7. Falling Forward
Ase ni vingi sana, natamani watu wasome
VINGI MNO.
 
Kwenye vitabu kuna vitu vingi sana vimefichwa ambavyo tunakabiliana navyo katika maisha ya kila siku na jamii inayo tuzunguka
 
Upo vizuri mkuu naamini wadau na wapenzi wa vitabu wamepata kitu kutoka kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…