Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

jiwekuu770

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
2,246
Reaction score
1,645
Habari jf

Katka kupambana na maisha kuna malengo tunajiwekea Shida ni changamoto ya kuyafikia. Mwanzo mwa mwaka 2016 nilijiwekea target kufikisha milion 3.

Kwangu ilikuwa hela nyingi coz nilikua nasoma na hela ambazo nilikuwa nashika ni laki laki mwisho laki 5 balance ya akiba laki moja!!... Lakini baadae nilipataga kazi kwahiyo kushika milion 3 ikawa siyo kazi but siyo akiba!! Unakuta hiyo milioni tatu ndio ufanye kila kitu akiba au saving ndio laki 3 au 5.

Najaribu kupambana nifike milioni 10 wapi!!

Kila ikifika milioni 3 au 4 napata shida natumia. Sasa nilitaka tubadilishane experience na wanajf wenzangu ambao mmeshavuka huko au mna idea.

NB: Hapa naongelea saving, hela unayoisave baada ya kufanya mambo mengine.

Je, wewe ulifikishaje milioni 10 yako ya mwanzo?
 
Nilikuwa Naishi Kasulu Hapo Kitambo Kidogo Miaka Ya Nyuma Maisha Rahisi Nikajibana Mpaka Nikawa Na Millions 8. Kipindi Hicho Sumry Ya Dar es Salaam Kwenda Kigoma Kupitia Nyakanazi, Kakonko, Kibondo, Kasulu, Hadi Kigoma
NMB Ilikuwa Mwisho Wa Mwaka Kuna Pesa Wanakuwekea Sijui Ilikuwa Bonus Ama....
 
Jiunge kikoba au Sacco's pia michezo ya Kila siku.

Nipo kwenye mchezo naweka 20,500 Kila siku sometimes nacheza majina hata 3.

Siku nikipokea hela napeleka kikoba.

Tumevunja juzi piga hesabu.

Mwaka huu mwendo ni ule ule namuomba Mungu sana ila najua inawezekana tu kwake in five years to come niwe na m 50 hivi
 
Pindi nipo chuo bodi waliniingizia 1.2 M Kwenye accnt yangu. Daah nilijiona bonge la tajiri, aisee ile pesa haikudumu hata mwezi.

Hapo ndio nikajua millioni ni pesa ya mboga tu. Sasa hivi nina ndoto za kushika billion na kuendelea.
 
Jiunge kikoba au Sacco's pia michezo ya Kila siku
Nipo kwenye mchezo naweka 20,500 Kila siku sometimes nacheza majina hata 3
Siku nikipokea hela napeleka kikoba
Tumevunja juzi piga hesabu
Mwaka huu mwendo ni ule ule namuomba Mungu sana ila najua inawezekana tu kwake in five years to come niwe na m 50 hivi
VICOBA = Village Commercial Bank...
Nakushauri bora pesa yako ukainvest sehemu au uingie partnership au ununulie hata shares kama una knowledge na hivyo vitu kuliko uko Kwenye VICOBA na masaccos, uko ujanja mwingi watu wanacheza na % tu..
 
VICOBA = Village Commercial Bank...
Nakushauri bora pesa yako ukainvest sehemu au uingie partnership au ununulie ata shares kama una knowledge na hivyo vitu kuliko uko Kwenye VICOBA na masaccos,uko ujanja mwingi watu wanacheza na % tu..
King ni hivi Sacco's zipo za maana hazina shida usisikilize maneno ya chadema mkuu
 
Nilifungua account maalum ya savings ambayo sitoi.

Nikaweka standing order ya kukata kiasi fulani kila mwezi kwny akaunti ya kawaida.

Nikawa naishi kwa bajeti na napeleka any extra cash huko.

Haikuchukua muda lengo lilifikiwa.

Na bonus ishakua tabia...kuweka akiba.
 
Jiunge kikoba au Sacco's pia michezo ya Kila siku
Nipo kwenye mchezo naweka 20,500 Kila siku sometimes nacheza majina hata 3
Siku nikipokea hela napeleka kikoba
Tumevunja juzi piga hesabu
Mwaka huu mwendo ni ule ule namuomba Mungu sana ila najua inawezekana tu kwake in five years to come niwe na m 50 hivi
Kwanini usiweke bank?
 
Back
Top Bottom