Ulijiepusha Vipi na Urafiki Mbaya? Niliponzwa na Urafiki na Wabaya

Ndio marafiki Wa mashaka wana gharimu sana
Nadhani wewe ni wale watu ambao hutaki kumwingiza mwenzako kwenye matatizo, lakini upo radhi kuingizwa kwenye matatizo, na ukakaa kimya ili uonekane mwana.

Japo ni zamani, lakini kuwa namsimamo wako wewe kama wewe ni vizuri.

Rafiki yako anatakiwa ajue msimamo wako kiasi kwamba hata kukusingizia atashindwa aanzie wapi.

Nakumbuka mzee wangu aliombwa hati ya nyumba na rafiki yake ili akachukue mkopo. Mzee alimkatalia kiroho safi japo yule mzee alimind sana.

Kuna mzee mmoja upande wa shemeji yangu, alimpa rafiki yake hati ili akachukue mkopo. Bahati mbaya yule mzee akafariki dunia. Aliyepewa hati anasema hadaiwi kitu na hajui kuhusu hati. Mzee wa watu alimpa rafiki yake hati kienyeji na sasa familia nzima inapata shida.

Kuwa na msimamo ndiyo jibu pekee. Ukiona rafiki haeleweki, songa mbele.
 
Jamaa yangu tulilipoti mapema Sana shule kuanza form one. Hapo ndipo ulipo anza Urafiki.. Saivi nipo makini sana
 
Kweli mkuu nimejifunza mengi Sana hadi sasa.. Rafiki Wa mpumbavu ataumia
 
Ndege wafananao huruka pamoja..ni vizuri kurafuta unayefanana nae..hawa wengine ni matatizo tu.
 
sitasahau naanza form V boarding
niliwahi kuwasili basi nikachagua kitanda kizur cha juu nikakutana na mchz deka zetu zimeungana wote tupo juu baada ya story akasema twende tukazunguke tukaijue shule hapo shule walikua wamebaki form four peke yao so kama ndo walitupokea form five

tukajikuta darasa la washkaji wamejifungia wanakaredio chao wanachana free style kumbe mchz niliekuwa nae pia anapenda kuchana baada ya mda akawaambia mm mzuka umekata mpaka nishtue dah mamaee kumbe wanadiscus bangi kweli waarabu wanajuana kwa vilemba mm sikuelewa wao wakaelewana fresh wakamwambia twende hv
mm sielew nawafuata tu kuja kustuka watu wanatoa bangi wanavuta dah nilichoka wakaanza kuniforce nivute ili nisiwe snitch ikabd nitunge ka story io bangi mm nilivuta sana sema nikapata kifua kikuu ndo nikaacha
washkaji wakanielewa wao wakaendelea kuvuta uzur mm ni muongeaji tu mzuri na unafki nauweza basi nikawa na wapump na wadanganya na vistory vya kihuni wakanikubali mno walivomaliza tukasepa hapo mm natetemeka mda wote nikikamatwa hapa sijui ntamueleza nn baba yangu shule yenyewe prv8 alafu nifukuzwe siku ya kwanza kwa kosa la bangi dah
uzur walimaliza bila kukamatwa mm nilivopata chance tu ya kuchomoka mazoea na mshkaji ndo nikakata ingawa kuna siku walikua wananipitia class nikavute nashukuru bangi haijawah kunishawishi aisee nilikua nawapa sababu mpaka wakakata tamaa za kunivutisha
 
Hongera mkuu... Ujanja ulikusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…