Ulijifunza jipya lipi 8 8?

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,598
Waungwana hamjambo!
Nane nane mwaka huu ilikuwa na mambo mengi ya kujifunza. Mimi niko pande za Mwanza hivyo nilihudhuria kwa siku tatu tofauti tofauti.
Siku ya kwanza nilijifunza kilimo cha mapapai ya kisasa ambapo nilikutana na mkulima aliyekuwa na mbegu anauza na kutoa maelekezo. Jipya kwa huyu mkulima ni kwamba aliweza kunijulisha ni mbegu zipi za mpapai ukizipanda hazitoi mazao au zinatoa vipapai vidogo ambapo wengi hudai kwamba ni mipapai dume.
Pili, nilijifunza namna ya kutengeneza mruda kwa ajili ya kulea vifaranga.

Tatu nilijifunza kwamba watanzania hawapendi kujifunza, watu wengi walikuwa kwenye mabanda ya Halotel, Tigo, Vidacom na Cocacola wakiangalia wanenguaji, Sehemu za watu kujifunza kulikuwa na watu wachache sana ukilinganisha na kwenye mabanda ya burudani.

Tubadilike jamani... wewe ulijifunza nini jipya?
 
sisi mkoa wetu hatukuwa na mambo ya nanenane ni vyema ukatumegea ulichonjifunza zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…