Ulikuwa Hujui?? Basi haya ndio maajabu ya bia..!!

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Kila ukinywa bia 1 umekunywa tofali 2 za kujengea.

Bia 1 kwa bei ya kawaida ni Tsh.2500/= na tofali 1 la inch 6 kwa maeneo mengi ya nchi ni bei isiyozidi.

Tsh.1300/=. Kama unakunywa wastani wa bia 5 kwa siku (kipimo cha kawaida) it means unakunywa bia 1,825 kwa mwaka sawa na tofali 3,650.

Tofali 3,650 zinatosha kujenga nyumba 1 ya room 3 self contained ya kisasa. Hii inamaanisha kuwa kama wewe nimnywaji basi kila mwaka unakunywa angalau
nyumba 1 au 2.

Sasa hebu jiulize tangu umeanza bia hadi leo umeshakunywa nyumba ngapi?

Anyway.. tuache kufananisha nyumba na vitu vya maana. Muhudumu ongeza bia.
 
lakini kumbuka huwezi kununua tofari moja kila siku hila bia unaweza maana kwanza utaanzia wapi.

swissme
 
lakini kumbuka huwezi kununua tofari moja kila siku hila bia unaweza maana kwanza utaanzia wapi.

swissme
Ukiamua kuwekeza kwenye kiwanda cha tofali, kila mwezi unaletea mzigo... Hakuna kinachoshindikana mkuu
 
Shiiiiii!!Mkuu usiwashtue walevi.Acha wengine tuendelee kuitwa baba mwenye nyumba
 
Maajabu mengine mpaka unaandika hivi huna hata kibanda bado unepanga, huku hunywi,
Sijui wewe unazipeleka wapi hizo hela








Kama hujawahi simamia hata kanyumba kako ka vyumva hata vinne utajenga humu jf nakwambia
 
Nibora wanywa biere, wanajua hela ilipoishia kuliko wengine hata hawajui zimeishia wapi. halafu kujenga ni mipango na zama, siyo swala la ulevi. mleta mada una element za woga wa maisha, nahisi ukiwa bar pesa unahesabia chooni.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukiacha kula pia ndo utajenga hata kumi aisee!
 
Acha kutukata stimu kwanza ww unaonekana utumii, nyumba nyumba nawaliojenga zakupangisha watakula wapi?
Na kanchi kenu kataendeleaje tusipokula ngano? Em kua
 
Takwimu zinaonyesha watu wengi wanaokunywa bia ndo wamejenga, na wengi wasiokunywa bia ndo wamepanga hawajajenga, sijui kwann hapo..?
 
Takwimu zinaonyesha watu wengi wanaokunywa bia ndo wamejenga, na wengi wasiokunywa bia ndo wamepanga hawajajenga, sijui kwann hapo..?

Kwasababu wanywaji hawafuati mambo ya takwimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…