Maelezo ya kwenye Red ndiyo maelezo ya Nyerere ninayemfahamu!!
Achana na Ribosome yeye tangu enzi zilee akiitwa vilee akisikia jina la Nyerere anaweweseka. Sisi wengine tumefikia mbali zaidi kuamini kwama Mandela umaarufu wake unakuzwa sana na watu wa Magharibi kwa malengo yao mahsusi baada ya kuwaona watu kama Kwame Nkumah na Nyerere walikuwa ni vikwazo kwao. Mandela hakuwa mwanafalsafa kama Nyerere.Kigarama,
Hata mimi. Nilikuwa namjibu Ribosome ambaye alitaka kutuaminisha kuwa Nyerere alikubali yaishe kimya kimya.
Siku hizi za mtandao huwezi hata kumdanganya mtoto mdogo. Utaumbulika.
Siku moja nakumbuka nilikimbizana na gari la ugawaji mchana wa jua kali kwa zaidi ya maduka kumi. Kufikia duka ambalo sukari ilikuwa inashushwa nikaambulia kilo moja,lakini kurudi nyumbani nilionekana bonge la shujaa!!Duka la kaya lilikuwa noma. Kabla vita vya nduli mambo yalikuwa mazuri. Wauzaji tulikuwa tunawaita mameneja. Baada ya vita ilibidi mtu uamke alfajiri kwenda kupanga jiwe au kiroba cha mchanga. La kwetu pale Nyakato sokoni tulikuwa tunapaita Iloganzala. Kila nikipîta pale huwa pananikumbusha sana ile foleni ya kipindi hicho, siku hizi pamevunjwa wakati wa ujenzi wa barabara ya mza-msm. Nyerere ulijaribu R.I.P!
Wewe unadhani mimi namlaumu Mwalimu? Mimi kati ya watu ambao ni watetezi wakubwa wa Mwalimu lakini sikuleta hii mada ili kumhukumu Mwalimu.
Mimi nilishiriki kuiishi hali hii, nilikula unga wa YANGA, nikabugia BURGA, nikaogea MAJANI YA MPAPAI,nimekunywa chai kwa kuchemsha sukari kwa ukosefu wa majani ya chai, nimeogea sabuni ya MAGADI. Huu ni uzowefu wangu wala sina uchungu na sera za Mwalimu!!
Waliomfuatia Mwalimu afadhali ya Mzee Ally Hassan Mwinyi. Yeye alikuwa dhaifu lakini hakuwa mhalifu kama wenziwe wawili waliomfuatia. Ingawa kuna lile doa la Mama Sitti Mwinyi la kuuza "Stella Atois". Biashara za Ikulu ni mama Maria Nyerere peke yake ndiye aliyesalimika!!Umenikumbusha sabuni za Kamanyola na Uniform za Marudufu, Jinja na Marekani. Nadhani vitambaa vilitengenezwa na Kiwanda cha Urafiki kabla hakijafa. Angalau wakati ule viwanda vilikuwa vinafanya kazi, japo chini ya kiwango kuliko alivyofanya Mkapa, kuviuza na kuvigeuza maghala.
Umaskini aliotutumbukiza Nyerere hauna mfano. Mpaka leo wengi wa Watanzania wanateseka kwa ajili yake.
mkuu mimi niliambulia kuona hayo maduka ya RTC sukari, vyombo kwa foleni, kijijini huko naenda na mama kupanga foleni ya kununua robo kilo ya sukari, daftari niliwahi kununua kwa senti 5 1986,Usisahau ili kadi ambayo mjumbe wa shina anajaza resho yako. Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa single basi baba mwenye nyumba akawa nampa share yangu.
kwakuwa wee shabiki wa YANGA lazima uusifie, wenzio sik hizi wanasifia maandazi ya AZAM, ila bulga bana, na uji wa ngano ambayo haijasagwa, nakumbuka baba aliwahi kuja na maziwa ya unga tulitesa mtaani balaa,Mie nikiwa kitoto nilimkuta jirani mmoja anafukia mabati mapayaaaa ardhini. Nikawa namshangaa tuu. Akanipiga mkwara mzito nikimwonyesha mtu yoyote hapo nitakiona. Ila uji wa yanga ulikuwa mtamu acheni masihara. Ulikuwa ukikamulia malimao dah mtamu balaa. Wee acheni tuu.
duh! hilo la bia ni kali, ingekuwa asaiv ningeshafungwa,Mimi nakumbuka mgao wa bia, ambapo bia zilikuwa zinapatikana mwisho wa mwezi. Kila mtu alipangiwa kunywa bia 3 tu. wakati unakunywa bia USALAMA WA TAIFA wanaokata vizibo vya bia ulizokunywa. Ukimaliza magao wako wa bia 3 unakwenda nyumbani kulala. Ukijifanya mjanja ukahamia baa nyingine kuongeza, ukifika baa mhudumu anakunusa mdomo akikuta unanuka bia unakufukuzwa kwasababu atajua kwamba ulikotoka tayari utakuwa umeshakunywa mgao wako wa bia 3. Pia ninakumbuka MARUFUKU ya kutembeza gari la binafsi siku ya JUMAPILI baaada ya saa 7 mchana. Siku ya Jumapili mwisho wa kuendesha gari la binafsi ilikuwa saa 7 mchana, baada ya mda huo gari la binafsi likionekana barabarani linakamatwa na traffic na kupigwa heavy penalty. Mambo niliyoyaona kipindi hicho yalinifanya NIUCHUKUE UJAMAA HADI LEO, mimi huniambii kitu kuhusu SIASA YA UJAMAA!
duh! hilo la bia ni kali, ingekuwa asaiv ningeshafungwa,
Mzee inaonekana wewe ni mtu wa KIU KALI. Lakini kama ungekuwepo kipindi hicho kiu yako hiyo ingekatika yenyewe. Lakini pia hata pesa ya kununua hizo bia nayo ilikuwa haipo. Uzalishaji wa bia kipindi hicho ulikuwa mdogo sana. Na kwa kuwa UJAMAA ni kugawana UMASIKINI tulionao, ndio maana ukawekwa mgao wa bia angalau kila mtanzania aliyetaka kunywa bia anywe japo kidogo. Kwa wale wavutaji wa sigara, ilifika wakati sigara zikauzwa kwa pafu/fundo. Yaani wavutaji sigara wanajipanga foleni, halafu sigara inawashwa watu wanauziwa kwa pafu/fundo la moshi unaovuta. Wakati mvutaji anapiga pafu/fundo, muuzaji anakuwa amemshika koo, akizidisha pafu/fundo la moshi anamkaba koo.
Nakumbuka sisi tulipokuwa tunaishi bahati mbaya hatukupangiwa duka la kaya ilibidi tufanye urafiki na Wapemba waliokuwa na maduka ili angalau akuuzie nusu kilo ya sukari. Siku moja mimi namwenzangu rafiki yetu aliyekuwa anafanya kazi Game reserve alitutumia kopo la mafuta ya kula Supaghee kilo 2 kila mmoja, njiani watu walitushangaa sana tumeyapata wapi.