Ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA??

Duh umenikumbusha mbali nakumbuka enzi hizo nilikuwa mdogo natumwa kukaa nje kusubiri gari la sukari likisimama niwastue ndani gari ina mlango nyuma ina mifuko ya kilo moja moja ya kaki na huruhusiwi kununia zaidi ya mfuko mmoja.
 

National Radio Cassette Memory Q, Viatu ilikuwa ni Bora peke yake tena kwa mgao. Jamaa wa RTC walikuwa kama Miungu watu miaka hiyo. Mitumba ilikuwa ikiiitwa kafa ulaya.
 

Hakuna kitu tangible alichofanya Nyerere zaidi ya kumaliza akiba ya Taifa lenu kwa kujijengea hishma ya kisiasa kuwa yupo mstari wa mbele katika ukombozi wa Afrika na kuuwa uchumi wenu kabisa.

Nchi alipewa ikiwa na akiba kubwa ya fedha, haikuwa na njaa hata kidogo, uchumi wake ulikuwa mzuri, hakukuwa na ulanguzi wala mwendo wa kuruka na kila kitu kilipatikana madukani. Yeye ndie muasisi wa Rushwa na Ulanguzi huko Tgk.

 
Kweli watu wametoka mbali. Nakumbuka kaka yangu alivunjika mkono wakti akigombea katika foleni kutaka kununua sababu ya mbuni pale mtaa wa Aggrey kariakoo.

Nakumbuka ilikuwa mkiwa mnakwenda kuswali alfajr tunaweka mawe katika duka la kaya pale Aggrey na ukitoka msikitini tunapangiana zamu kulinda jiwe letu maana mkiondoka tu watu wanalitupa. Na gari la Ugawaji linakuja saa sabaa au nane alasiri.

Kila mtu alikuwa lazima amjue Mkurugenzi mkuu wa NMC mzee Mollel au Mkurugenzi wake wa utawala Mz Uwesu msumi kwa ajili ya kupata kibali cha kununua vitu kwa wingi.

Kweli kila watu na zama zao.
 

Wee acha tu ndugu yangu enzi hizo!!! Ukimsimulia kijana wa dot com hawezi kuelewa mambo yalikuwaje.
 
Na mwisho akakimbia kwa staili ya kung'atuka.
 
National Radio Cassette Memory Q, Viatu ilikuwa ni Bora peke yake tena kwa mgao. Jamaa wa RTC walikuwa kama Miungu watu miaka hiyo. Mitumba ilikuwa ikiiitwa kafa ulaya.
Duh unanikumbusha raba za pua ya ng'ombe. Mgambo wakikukuta na raba za mtumba wanakuvua.
 

Duh! Mkuu unajua kutia chumvi kama mahindi ya kuchoma ya kileo? Pombe watu walikua wanapiga ila wanawahi kama sanduku mbili mnanunua mnaweka chini ya meza mkiogopa zisiishe. Na pia magari ya Serikali yalikua siku za Jumapili kutembea mwisho saa 8 na hii ilifanywa ili watu wasitumie magari ya serikali kwa starehe zao na ilikua gari la Serikali halitakiwi kuonekana limepaki Bar ukionekana unakamatwa na Polisi ilikua ni suala la maadili sio kama sasa .
 

Ndio ujamaa huo
 
[FONT=comic sans

Kila mtu alikuwa lazima amjue Mkurugenzi mkuu wa NMC mzee Mollel au Mkurugenzi wake wa utawala Mz Uwesu msumi

FONT]
Hspo ni Dar. Kwa wakazi WA Dodoma tunamkumbuka Shekifu. Na huo ndo ulikuwa mwanzo wake kung'ara hadi alipo sasa.
 
Yaani nimecheka sana! Enzi hizo wajumbe wa nyumba kumi walikuwa wa maana sana maana wao ndiyo walikuwa wanapanga ration!!!! Ukikuta foleni unasimama tu bila kuuliza na unauliza wa mbele yako anakuambai hata yeye hajui ameikuta akasimama tu!! Duh!! Mungu apishilie mablai hali hiyo!!!
 
Duh! Enzi hizo ilikuwa unaponunua sukari lazima ununue majani ya chai na unga wa UKURA au wa Yanga.
 

Weka mfano wa hivyo vitu kuandika tu vitu "tangible" ni so vague.

Nilikuwepo wakati huo, kabla ya huo na Alhamdulillah nipo sasa. Tusiandikie mate na wino upo.
 
Kikwete na familia yake wameteseka vipi? Wanatajirika kwa kuuza madini na ardhi yetu kwa wazungu. Kawaulize.

Kikwete na mkapa nani kauza madini? Na nyerere na mwadui hebu tueleze ilikuaje?. Wee ni mtu mzima hebu weka ukatoliki wako kando useme ukweli
 
Kikwete na mkapa nani kauza madini? Na nyerere na mwadui hebu tueleze ilikuaje?. Wee ni mtu mzima hebu weka ukatoliki wako kando useme ukweli

Soma hotuba aliyoitoa Kikwete Afrika Kusini 2007 kuhusu vile alivyokata mbuga kuwatafuta akina Sinclair ndio uulize swali lako. Mwadui ilikuwepo enzi za ukoloni na usitake kuniambia kuwa Nyerere ndiye aliyeleta ukoloni.
Mimi si Mkatoliki. Ni Methodist.
 

Mwadui ilikuwepo Toka enzi za ukoloni kwa hiyo nyerere asingeweza kufanya kitu.asingeweza kufanya kitu?..hustuki?..we unashtushwa na hotuba ya 2007?...Hii suppott yenu hata kwenye upuuzi uliofanywa na nyerere na mkapa ndio unaotufanya tuamini kuwa chuki dhidi ya kikwete inaanzia kanisani
 
Khaaa wewe nakukubali,yote hayo na bado unamkubali mwalimu!!?,we mwenzangu japo mi sikula hiyo Yanga wala Burga
 
Mshukuruni Mwinyi na team yake.

Duka la kaya huchezi mbali na mjumbe.

Kidaftari lazima kitiwe tick sehemu husika.

Bada utalijua tu hata kama kwenu hamli.

Na ugali wa Yanga juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…