Ulimboka adakwa kwa kutaka kumhonga Kado

Pia, kuna kesi ya Simba kumtumia aliyekuwa Mweka Hazina wake Jabir Shikamkono kutangulia Bukoba (mwaka nimeusahau) akiwa na fedha za kuwapa Kagera Stars ili waachie magoli na Simba wapate ubingwa. Ilikuwa mechi ya mwisho ambapo Simba ikishinda au droo basi anakuwa bingwa. Walichezea uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Yanga alikuwa Kirumba Mwanza akicheza na Pamba ambapo Yanga alihitaji kushinda na Simba ifungwe ili Yanga awe bingwa.

Jabir Shikamkono alipofika Bukoba akaficha zile fedha na akawadanganya viongozi wenzake kuwa ameshawapa Kagera Stars.

Mchezo ulipoanza, dakika ya 16 tu Simba wakapewa penalti na wakajua ndio ule mpango. Hussein Masha akafunga na kuongoza. Dakika ya 76 Mkama Ntare akaisawazishia Kagera na dakika ya 84 Fulgence Novatus akaifungia Kagera goli la pili. Hadi mwisho wa mchezo Kagera Stars 2 - 1 Simba.

Vurugu kubwa zilizuka ambacho viongozi na wachezaji wa Simba waliwashambulia wale wa Kagera kwa kuwataka warudishe pesa zao. Walikamatwa na kupelekwa polisi kulala huko. Baada ya mahojiano Jabir Shikamkono akakiri kuwa hakuwapatia pesa Kagera Stars ila alizificha akiamini Simba ingeshinda tu na pesa kuwa zake. Huo ndio ukawa mwisho wa Jabir Shikamkono ndani ya Simba.

Wakati huo huo, kona iliyochongwa na Kenneth Pius Mkapa ilijaa moja kwa moja wavuni na kuipa Yanga ushindi na kuibuka kuwa Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Hivyo, Simba haikuanza kuhonga jana. Ndio asili ya klabu yao.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi wa zamani, enzi za wapwa. Vijana wa siku hizi humu hawakujua uwapo wa groups ndani ya JF
 
Dah watu mna kumbukumbu. Hii mwenye kujua ni mwaka gani atuambje tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…