Ulimbukeni wa akina Hasheem Thabit

Hii ni tabia tu ya mtu binafsi na wala sio kusahau. Watu tumechikichia States zaidi ya miongo miwili na bado tunatema kilugha cha kwetu na Kiswahili kama kawaida itakuwa hiyo miaka mitano, wacheni hizo nyie. Halafu hizo Mid Western States ulizozitaja, Iowa na Minnesota mbona wabongo wapo kibao tu, au unaongelea za wapi wewe!.
 

Minnessota wabongo wameanza kuja miaka hii, tell me about connecticut ambako hasheem amekaa muda mrefu, hata kama wapo ni mmoja mmoja uwez kufananisha na texas, arkansas, atlanta and so on as huko atleast waswahil mnakutana kwa muda kwenye vi party vya hapa na pale, I was in grinnel Iowa for almost a month mpaka nikawa namuuliza mwenyej wangu watz wenzangu nitawapata wap na yeye ni mtz aliyelowea muda mrefu akasema ni ngumu sana na mpaka narud sikuona mbongo yeyote,

Na mdau aliyesema mbona india hawasahau kiswahili, india wabongo ni wengi sana as kila mji wapo, now nipo hyderabdad south india. But wabongo walivyojaa kama nyumban kias kwamba hata nikikutana na mtu mweusi kwenye popote naanza na mambo as najiamin ni wa kwetu tu, na wengi inatiki he he he, sasa kiswahil utasahau vipi sehem mliopo wengi, states kama indiana,alabama,connecticut mtz utamtoa wapi? Tuwe wakweli jaman
 
kuna watu walikuja wakiwa 8yrs old States, sasa hivi wapo kwenye early twenties na wanaongea kiswahili, jamani tuache visingizio visivyokuwa na maana. Hiyo Minnesota toka miaka ya 80's tayari kulikuwa na wabongo.
 


Na huyo mtoto angekuwa na kiwango kama cha Kevin Durant, air Congo Sergre-Ibaka, James Hadden, Air south kamanda Thabo, Kobe, Amaar Stoudmare, chaunsey Bilaups, au tu angekuwa anapata nafasi ya kuanza ktk game za NBA basi watu tusingekunya na kuchamba...

Ukiwaangalia alioingia nao NBA wenzie wako mbaaaali na ni mastaa kwa sasa.
Lakini lenyewe ushuzi mtupu
 
hii hoja uliyokuja nayo inaweza kuonekana ni ya 'kitoto' kwa wengi wetu lakini ni ya msingi sana na hasa kwa Watanzania.

Tatizo kubwa likakuja kwenye uelewa wetu (tulio wengi) ambapo ukiongelea utamaduni tunadhani ni kucheza ngoma tu. Tanzania hatuna utamaduni na matokeo yake ndio haya kwa maana wanasema nchi/mtu bila utamaduni ni mkusanyiko wa watu wasioelewa wanakotoka na hivyo haitatokea hata siku moja wakaelewa wanakoelekea!

Pia kuna maswali megi katika kuifanya lugha ya Kiswahili kama sehemu ya utamaduni (lugha) wa Watanzania huku tukisahau makundi madogo madogo yanayoiunda nchi kwa ujumla wake kuwa wana lugha zao kwa hiyo kushindwa kuelewa ni wakati gani wa ku-promote lugha ipi kati ya hizo mbili.
Chukulia mfano wa Wanyarwanda, Waganda, Wakenya, Malawi nk, hata wengine wamezaliwa ulaya huko huko na wengine wamekaa zaidi ya miaka 25 lakini wakiongea Luganda, kijaluo nk, utadhani wamekulia hapo. Na wanaona fahali kweli japo sisi hapa tunaweza kuita "kuleta ukabila".

 
Hi kawaida eti kuonekana matawi ni lazma uongee lafudhi ya kimarekani, au uchanganye kingereza na kiswahili, si hashim tu hatahapa bongo kunavitoto vikienda shule za kimataifa huko mbezi vinarudi uswazi vikiongea kingereza cha kulazimisha na lafudhi ya kimarekani,. Kwa wataalam wa lugha mtu akifikisha umri wa mika 16 hawezi sahau lugha aliokulia na kubadilisha lafudhi mfano mzuri magufuli,ngeleja na wengineo wengi
 
Hawa nao mi mkuu wao nimekaa huko ambako wao wamekwenda juzi nimerudi natwanga bado kilingala achilia mbali kiswahili ndo wawe hawa wakuja?
 
Daaaah! Hii imetokea kwangu jana tu, jamaa yangu msukuma alienda znz mwaka jana mwanzoni kutafuta maisha,jana karudi fulu mpemba atiiiii! Nakumbuka jamaa alikuwa anakandamizia balaa, sasa hivi ulimi lainiii! Kwangu mm huu ni utumwa wa mawazo.
 
Msiseme tu watanzania eti mkikaa maulaya mwezi tu mnajifanya hamjui Kiswahili,wangapi tunawaona hapa mjini kila sentensi lazima atupie vimaneno vya kizungu kana kwamba hajui kwa Kiswahili yanatamkwaje! Na hao hao Ukute hawajatoka hata hapo nje ya Darisalama,ni ulimbukeni tu Na kukosa fikra kuhisi nikiongea vimaneno vya kizungu nitaonekana Wa maana Zaidi,haijalishi uko abroad,ulienda abroad au vyovyote vile! Asanteni kwa kunisoma!!
 
Huku niliko Nina Zaidi ya 10 years,lakini kudadadeki nikiongea dk 2 tu unanijua Kama sijazaliwa mtimbwilimbwi basi nimeshuka sasa hivi toka mahuta,Na ninaona sifa sanaaa tu! Sasa mtu ajichanganye aniongelee kizungu chake Na nijue kaingia hapa wiki iliyopita ninampa za uso hapohapo kuwa Ndugu tafadhali,ili twende sawa toa maneno ya kizungu!!
 
tajibeba babuuuu..mwenzako leo ndo anasign deal ya 2bn kw amiaka miwili.....ulisema ukistaafu kiinua mgongo chako ni 18m?? hahahaaaaaaaaaaaaaaaa nicheke mie
 
Wivu wa kike....wivu wa kijinga.....wivu wamaendeleo............wivu wivu wivu utakuua!!Au wewe ujui kama Hashmu ni Superstar?? celebrity??

nini!? supastaa!. Unamjua jack chan,jet lee wale nao wasemaje..mbna wao wanaongea lugha yao ijapokuwa wanafanya kazi huko marekani..huo ni unyonge tunaojiwekea wa africa..mi nina ndgu yangu ameishi huko miaka 12 bila kurudrudi tz ila sasa hivi amerudi na anakichapa kisw kama kawa tena mpaka maneno ya kihuni.
 
inferiority complex! inawezekana ndo inayomsababishia ashindwe kufanya vizuri! aonane na washauri nasihi wamsaidie!
 

Bora ulivyompa ukwelia wake maana kuna mijitu mingine haijui hata kuficha miwivu na chuki zao.
 
Mbona niko muda mrefu wa maisha yangu na mke wangu, bint zangu, bibi yao pia bosi wangu, demu coleague wangu wengi kazini mademu na nawapenda mademu mbona siongei kidemu demu?
 
...Kuna family friend ambao baba yao aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Sweden mwaka 1975 na waliondoka hapa wakiwa between 12 na 18 years of age.waliishi Sweden kwa karibuni miaka 15 mfululizo ma baada ya Baba yao kustaafu na kurudi nyumbani wengie walibaki hapo hapo Stockholm na wengine waliunganisha marekani ambako wanaishi mpaka sasa. Hivi karibuni mmoja aliyekuwa school mate alirudi kwa likizo after more than 16 years in Sweden na tulipokutana alikuwa akiongeza kiswahili fasaha kiasi cha mimi kumtania kwa kumuuliza kama alikuwa akiishi Sweden kweli! NI mindset tu na Infiriolity Complex kujifanya umesahau lugha uliyozaliwa nayo baada ya miaka mitano huku kila mwaka ukirudi nyumbani kwa likizo.
Na ndio maana hata watetezi wanatoka jasho sana kutetea hili...!
 
Nilikuwa najaribu kufuatilia ushabiki huu kwa Hashim. Inashangaza!!!

Hashim hajafanikiwa kuliko Yi Jianlian. Mbona kichina kinapanda kama kawaida? Nadhani kweli kuna umuhimu wa kuogeza shule yake kwanza ndo ahangaike na mpira wa mikono. Nahisi ana upungufu.

Sasa kuna kundi linasema ni wivu. Nani kamuonea wivu? Kwa kusahau Kiswahili?

Nani kauliza kipato chake? Nani kasema arudi Tanzania? Nani kasema haishi masaki? Nani kasema US alitakiwa aongee Kiswahili? Tunachojiuliza ni jinsi gani mtu aliye na akili zilizoenea asahau lugha aliyojifunza tangu akinyonya hadi Sekondari? Eti ana pesa! Eti amewazidi wa-tz vijana wenzake! Sasa ndo nini. Hayo ndo yamtoe akili?

Tusiingize ya wivu kama nyimbo za harusi zinazoimbwa kwa hisia tu! Hashim tumemsikia anavyoongea na kwa mwenye akili hakika utafahamu Siyo kwamba kasahau ila anataka ionekane hivyo. Akiwa US yeye aendelee kuiga lakini siyo hapa. eti anahojiwa mbele ya kamera yeye anajidai ulimi unagoma. Mara anapojisahau utasikia matamshi ya Kariakoo, akikumbuka anajishaulisha. Hatumuonei ila alazimishe kuwa na busara, isije kuwa hata kwa mzazi anamuhangaisha kuwasiliana naye.

Hata Mwinga Mwanjala naye ametolewa mfano wa kujidai kusahau Kiswahili wakati amekuwa mwanariadha hapa nchini mpaka alipochuja. Kaja Dar naye kuhojiwa eti Kiswahili kimeharibika tayari.

Vijana wengi walimaliza form 6 wakapelekwa USSR kusoma medicine kwa miaka 7 pamoja na kulazimika kutumia lugha ya huko, bado wamerudi wako fit na English yao ya Form 6 na Kiswahili chao na nahau zao. Hata hivyo najiuliza mbona mafanikio yake ktk spoti yanakuja polepole sana ukilinganisha na wenzake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…