Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,346
Huwa baadhi ya watu wakiingia katika nafasi za uongozi kwa mara ya kwanza, wanakuwa na 'moto' fulani ambao baada ya muda hupoa. Tunashuhudia hayo sio kwa maraisi tu bali hata kwa viongozi wadogo kama wakuu wa wilaya, mikoa au hata wakuu wa vitengo na taasisi serikalini.
Pengine ni kutokana na ambitions kubwa wanazokuwa nazo na kwa viongozi wa nchi pale wanapokuwa na uzoefu mdogo kwenye mambo ya kidiplomasia ndipo athari zinakuwa dhahiri zaidi.
Tulishuhudia Joyce Banda alipoingia madarakani, akaja na "moto" fulani wa kutaka kufanya mageuzi ya kiuchumi na kimaisha kwa Wamalawi over night.. Moto wake huo ukasababisha hata mahusiano yake na Tz yakatatizika kwa muda kwa jambo ambalo ni la kihistoria, na historia hiyo haionyeshi uwezekano wa jambo hilo kutatuliwa miaka ya karibuni. Tumelizoea, tunaishi nalo na pengine watakiamua vizazi vyetu vijavyo huko.
Banda baada ya kukaa na maraisi wenzake na kupewa cheo huko sijui SADC, kajifunza diplomasia. Sasa hivi kama mpolee, hatumsikii tena akitoa matamko ya hovyo hovyo... Keshajifunza "table manner", jinsi ya kula na maraisi wenzake...
Baada ya Banda, kaja tena Uhuru. Nae kaja na moto ule ule, diplomasia sifuri. Nae amerukaruka na akina Mu7 na Kagame ambao wana "interests zao", lakini tunaona anamtuma Amina Mohamed, aje Tanzania kubembeleza. Baada ya ziara zake mbili tatu, Uhuru nae anaanza kujifunza Table manner.. Baada ya miezi miwili mitatu atajua nini maana ya diplomasia, na hizi sarakasi za northern corridor sijui na nini hatutazisikia tena...