Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

Nashukuru sana mdau,Mimi nataka local za bongo tuu nyingine hapana,hivi wakibadir masafa hizi zinabadiri au mpaka ubadirishe mwenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru sana mdau,Mimi nataka local za bongo tuu nyingine hapana,hivi wakibadir masafa hizi zinabadiri au mpaka ubadirishe mwenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
Local za bongo unazipata bila shida kaka.

Kuhusu swali lako, wenye satellite wakibadili masafa inabidi na wewe ubadilishe uelekeo wa dish lako ama size ya dish, kutegemea mabadiliko husika. Mfano, Continental walikuwa wanarusha 75E, nasikia wamehamia 46E. Inabidi kubadilisha dish kutoka uelekeo wa 75 kuja uelekeo wa 46E.
 
Inabidi ili nipate kwa ubora nifunge cband au ku? Nipe ubora wa kila technology hapo Ku na cband ili nijue msaada kaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inabidi ili nipate kwa ubora nifunge cband au ku? Nipe ubora wa kila technology hapo Ku na cband ili nijue msaada kaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ubora hautegemei KU wala Cband. Zote KU na Cband zinarusha channels za HD na SD. Kikubwa ni mawimbi husika, iwapo yapo katika Ku an C band. Kama utadaka mawimbi ya Intelsat 906 @64.2E (dish kubwa la kuanzia futi 6), ambako ndio ziko local channels, mawimbi yake yapo ktk C band, kama utadaka Continental, @ 46E, mawimbi yapo katika Ku band (dish dogo la futi 3). Ni maamuzi yako sasa
 
Hivi hii satellite ipo mwelekeo ule wa Dstv ama East kama kawaida?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naaam fundi,je kuna local kwa bongo haipatikani kwa cband? Mimi nina dish kubwa fut 6 Kuband nyakati za mvua nasikia mzinguo broo leta utaalamu huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naaam fundi,je kuna local kwa bongo haipatikani kwa cband? Mimi nina dish kubwa fut 6 Kuband nyakati za mvua nasikia mzinguo broo leta utaalamu huo

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati wa mvua kubwa madish yote hayaoneshi channel kwa sababu mawimbi yanakuwa distorted. Local channels ziko katika KU na C band kwa satellite mbalimbali. Kuzipata zote uwe na madish matatu mpaka manne. Hebu pitia HAPA ujue naongelea nini, uzione na ufanye maamuzi sahihi ya channels unazotaka.
 
Ahsante mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari mtaalamu. Naomba nieleweshe hivi mfano mtu anataka kupata satelite fulani. Labda dish ilikuwa imesetiwa katika position ya kupatikana Intelsat 906 ila unataka kupata channel fulani iliyopo position ya BULGARIAsat 1.9E - 12380 H 30000 Tandberg. Je unatakiwa kugeuza dish au unatakiwa kuongeza vile vinavyodaka mawimbi ya satelite? Sijui vinaitwaje C band au Lnb au nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwa direction ya hizi satellite mbili ni tofauti, unageuza dish kabisa kufuata uelekeo huo wa 1.9E
 
Kwa kuwa direction ya hizi satellite mbili ni tofauti, unageuza dish kabisa kufuata uelekeo huo wa 1.9E
Sawa Asante, kwahiyo unaweza ukapata satellite yoyote ile kwa kutumia LNB hiyo hiyo moja uliyokuwa nayo kikubwa ni kubadilisha uelekeo kulingana na satellite unayoitaka ili kuipata channel husika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ITV imepotea kwenye satellite ya Intelsat 906.Nani anaipata kwenye satellite yao mpya maana nilijaribu juzi sikuipata.
 
Mii nauliza upatikanaji wa satellite za mbali inategemea na ukubwa wa dish
 
Kwa mfano watu waliopo tz wanaweza kupata sat za Europe kama astra na eutusalat
 
Hatimaye uzi umeibuka upya,hakika ITV ni super brand siku mbili kumekuchaa aiseeh
 
Mkuu nimejaribu pia kwa dish la ft8 hmna kitu ukifanikiwa naomba ni pm boss
Nimeipata vizuri tu ila signal sio kubwa kama ilivyokuwa kwenye sat ya zamani.Pia mfumo haujabadilika hata wenye Mediacom wanaweza kuzipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…