SoC02 Ulimwengu wa Shamsa

SoC02 Ulimwengu wa Shamsa

Stories of Change - 2022 Competition

Jamie M

New Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1
Reaction score
0
ULIMWENGU WA SHAMSA

Mama! Mama! Ilisikika sauti huku akiwa anatembea kuelekea chumbani kwa Mama yake.
Inamaana Mama hajarudi mpaka sasa ivi tangu alivokwenda shamba asubuhi. Alianza kupata wasiwasi kwaji mda ulikuwa umekwenda. Akiwa anaendelea kutafakati huku akiwa amejawa na hofu taratibu alisikia mlango ukifunguliwa, alikuwa ni Mama yake Shamsa akiwa anarejea kutoka shamba

'vipi mwanangu mbona hujavua nguo za shule'

'Hapana Mama, shikamoo pole na uchovu wa shamba'

'Asante mwanangu, naomba ufanye haraka nmekuja na mihogo uandae chakula cha usiku. Leo nmechelwa sana mto ulijaa maji na nikalazimika kupita ile njia ya "msitu wa tembo" ndio sababu imenifanya nmechelewa sana leo'

'Mama ile njia umepita mwenyewe unesahau tumempoteza baba kwa kushambuliwa na tembo' kwa unyonge shamsa alinuambia Mama ake

'Hapana mwanangu huku akiwa ameweka mkono kichwani kwa Shamsa, mwanangu kuishia kwenye mdomo wa mamba au kuishia kwenye mdomo wa tembo ni maisha ambayo tumekuwa tukiyapitia tangu enzi na enzi na tumekuwa tukipoteza ndugu na jamaa zetu bila matumaini ila ipo siku yatakwisha na ufumbuzi wa haya utapatikana.

Kwa upole na macho yakiwa yamejaa machozi alimtazama Mama yake na kusema kimoyomoyo "ipo siku tutaishi maisha ya furaha" .

Baada ya kumaliza kjla chakula cha usiku Mama alienda kulala na mimi nilichukua vitabu vyangu na kuanza kujisomea, nilisoma kwa uchungu mno kwani nilitamani kumuona siku moja Mama yangu anafuraha mda wote

Siju moja Shamsa akiwa anamsuka Mama yake nyuma ya nyumba yaokwa mbali alimony rafiki ake Zakia akiwa mwenye uso wa furaha na tabasamu .

'Shamsa tumefaulu kwenda chuo kikuu'

Ilikuwa ni siku ya furaha sana katika maisha yangu nilitokwa na machozi ya furaha Mama alitukumbatia na kusema ' hongereni sana wanangu, hongereni sana naona mwanga gizani, naona ndoto zenu zinakwenda kutimia sasa. Naomba mpiganie ndoto zenu na kamwe msikubali kuishia njiani, sawa wanangu

Zakia na Shamsa walianza maisha mapya chuoni, maisha hayakuwa raisi kutokana na changamoto nyingi walizokutana nazo zaidi ikiwa ni ukosefu wa pesa ya matumizi, waliishia kutamani na kuona maisha mazuri kwa wanafunzi wengine

Baada ya miezi sita Zakia alipata rafiki na kuanza kubadilika, alianza kupendeza na kuvaa usasa huku akisahau ndoto zake. Baada ya matokeo kutoka Zakia alishindwa kuendelea na masomo kutokana na kufeli masomo yake yote Alilia kwa uchungu pale alipokumbuka ndoto zake zimeishia njiani.

Hakuweza kurudi nyumbani kwani alikuwa anawaza atawaambia nini wazazi wake mpaka kushindwa kuendelea na masomo hivyo aliamua kuanza maisha mengine mjini.

Shamsa alifanikiwa kumaliza masomo yake na kuhitimu vizuri kwa alama za juu sana, aliamua kurejea nyumbani ili aweze kumpa Mama ake ushindi alorudi nao, ghafla Mama ake zakia huku akikimbia na kwasauti alimuita Shamsa, shamsa! hujambo mwanangu mbona upo peke ako mwenzio tuko wapi? Shamsa alidanganya na kusema yeye atachelewa kidogo anakuja.

Shamsa alifika nyumbani na kumkuta Mama ake akiwa anasuka mkeka alimkumbatia kwa furaha na kumwambia Mama ake 'Mama mimi sasa ni dakatari' wote walifurahi kwa furaha
 
Upvote 0
Back
Top Bottom