Ulinzi na usalama wa Kimtandao

Ulinzi na usalama wa Kimtandao

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Ulinzi wa kimtandao humaanisha tabia anuwai na tahadhari za kujilinda anazofuata mtu wakati anatumia mtandao katika kuhakikisha kuwa habari nyeti za kibinafsi na za vifaa anavyotumia mtandaoni vinabaki kuwa salama.

Husaidia kupunguza uwezekano wa kushambuliwa au kupunguza madhara ya shambulio lililofanikiwa.

Ni budi kufahamu kwamba chochote unachotuma mtandaoni kinaweza kuwa chanzo au habari inayotumiwa na Wahalifu wa kimtandao kuzindua kashfa au shambulio la mtandao dhidi yako.

Kuwa makini katika kila hatua kutoka kuandaa mafaili kwenye vifaa vya kidijitali, kuendesha akaunti zako kwenye mitandao ya kijamii pamoja na kuanzisha programu au teknolojia mpya ili kurahisisha maisha ya kidijitali au kuyafanya yawe salama zaidi.

Tunaweza pia kuita unadhifu wa mtandao au usafi wa mtandao anga.


=====

Unadhifu wa kidijitali ni hitaji la wakati wote na ni kama mazoea au tabia zinazopaswa kuendelezwa ili kudumisha unadhifu katika ulimwengu wetu wa kidijitali.

Hii inajumuisha kila kitu kutoka kuandaa mafaili kwenye kompyuta yako, kusitisha akaunti zako za mitandao ya jamii, kuanzisha programu mpya au teknolojia ili kufanya maisha yako ya kidijitali yawe rahisi au salama zaidi.

Tunaweza kusikia hii ikiitwa unadhifu wa mtandao au usafi wa mtandao anga. Hizi zote zinamaanisha kitu kile kile.

Faida za Ulinzi wa Kidijitali
Kwa kulinda habari unayosafirisha mtandaoni na au kulinda vifaa vya dijitali unavyotumia, unapunguza uwezekano wa kushambuliwa au kupunguza madhara ya shambulio lililofanikiwa.

Ni budi kufahamu kwamba chochote unachotuma mkondoni kinaweza kuwa chanzo au habari inayotumiwa na maharamia wa mtandao kuzindua kashfa au shambulio la mtandao dhidi yako.

Hivyo kama mdau wa haki za kidijitali, kuzingatia tabia zinazohakikisha unadhifu wa matumizi ya mtandao ni muhimu sana katika kujipa ulinzi mtandaoni.

Kuna mambo kadhaa rahisi unayoweza kufanya bila kununua teknolojia ya gharama kubwa au kuwekeza muda mwingi katika kusanidi upya mtandao wako wa nyumbani kwa lengo la kufanya kompyuta yako unayotumia mtandaoni ipate ulinzi bora zaidi. Orodha hii hapa chini ni mahala pazuri pa kuanzia na inakuunganisha na maeneo mengine ya tovuti yetu kupata habari zaidi juu ya kila hatua ya usalama na kujilinda kimtandao.

Desturi za kudumisha ulinzi wa kidigitali
1. Weka mifumo yako na programu yako hai wakati wote.

2. Daima kuwa na programu ya kupambana na virusi iliyo hai wakati wote.

3. Epuka wizi wa hadaa au utapeli wa taarifa zako.

4. Tumia nywila ngumu au meneja wa nywila.

5. Kuwa mwangalifu unabofya nini; tovuti isiyo salama inaweza kukuunganisha na maharamia wa mtandao.

6. Kamwe usiache kompyuta au vifaa vyako vya dijitali wazi. Funga komyuta yako unapoelekea hata uani. Kuacha kompyuta wazi ni mwaliko wa wazi wa kushambuliwa kwa mafaili yako.

7. Weka namba ya siri kwa kifaa chako cha rununu, na usijaribu kamwe kukiacha wazi ukiwa ndani ya ndege

8. Linda taarifa zako

9. Kwa faili zote za kibinafsi, chelezo taarifa zako! Huwezi kujua ni lini kihifadhio (hard disk) chako cha kompyuta kitaharibika na pengine usipate taarifa zako tena. Chelezo kutumia huduma za mtandao wingu (cloud) au kihifadhio huru.

10. Unaponunua mtandaoni, au kutuma taarifa nyeti, hakikisha unatuma habari iliyosimbwa na utume kwenye tovuti zenye anuani zinazoanzia na “https” au ikoni ya kufuli kwenye mwambaa wa anuani yako.

11. Kuwa mwerevu juu ya kile unachowasilisha (au acha kuwasilisha) kwenye mitandao ya kijamii.

12. Katika ulimwengu wa muingiliano mkubwa wa watu, kuwa mwangalifu kwa ‘uhandisi wa kijamii’. Hii inaweza kuwa jaribio la mtu usiyemjua kukuvuta kijanja na kumpa habari kama siku yako ya kuzaliwa, wapi unapenda kwenda likizo, jina la mnyama unayemfuga nyumbani, Ukiulizwa na mtu jiulize je ni kweli anahitaji taarifa hizo? Ukimpatia majibu ya maswali kama haya yanaweza kusababisha akaunti yako kuibiwa na ushindwe kuwepo mtandaoni.

13. Hakikisha unafuatilia matukio yanayotia shaka yanayogusa akaunti zako za kifedha na za mitandao ya kijamii bila kuchoka ili ubakie salama siku zote.

Chanzo: AYETA , Kifaa cha Zana Cha Haki za Kidijitali
 
Back
Top Bottom