SoC04 Ulinzi shirikishi iwe taasisi rasmi ya kijamii kwa ustawi wa ulinzi na usalama kwa jamii

Tanzania Tuitakayo competition threads

WAPEKEE_

Member
Joined
May 23, 2024
Posts
21
Reaction score
28
UTANGULIZI
Ili taifa lolote liendelee, suala la Ulinzi na Usalama ni moja ya jambo nyeti na muhimu sana , kwani limebeba dhana ya kimaendeleo kwa kuwalinda wananchi na mali zao pamoja na kudumisha Amani na utulivu katika jamii. Jukumu hili ni la Jeshi la polisi ndio hasa chombo kinachowajibika kwa ulinzi na usalama wa jamii.

Kwasababu ya kuongezeka idadi ya watu na ukubwa wa mazingira kijiografia, jeshi la polisi pekee bila ushiriki wa jamii katika masuala ya usalama haliwezi kusaidia jamii kwa wakati na weredi mkubwa.
Hapa ndipo dhana ya ulinzi shirikishi inakuja kwa kuishirikisha jamii kwenye masuala ya ulinzi , kama kiungo muhimu cha kulisaidia jeshi la polisi kwenye masala ya uhalifu na uvunjifu wa Amani.

SHERIA NA SERIKALI ZA MITAA.
Suala la Ulinzi na Usalama, kisheria linatambulika kuwa wanajamii wote tunawajibu kushiriki kwenye shughuli za mendeleo ikiwemo Ulinzi na Usalama. Mamlaka ya Serikali za mtaa , yanawapa fursa wananchi kujiunga kuwa kikundi na kupewa mafunzo mbalimbali ya kupambana na kuzuia uhalifu na kudumisha amani.
Dhana hii inasaidia wananchi kutokujichukulia sheria mkononi kwa wavunjifu wa amani , bali ni kuwakamata na kuwakabidhisha katika vituo vya polisi ili sasa sheria ichukue mkondo wake kwa kufata sheria na taratibu. Pia inasaidia upatikanaji wa taarifa muhimu za kiintelejensia kwenye usalama wa jamii.

ULINZI SHIRIKISHI ( POLISI JAMII ).
Kwa miaka 25 ijayo, masuala ya uhalifu ni moja ya changamoto kubwa hasa kwa kuzingatia kasi ya maendeleo na ongezeko la idadi ya yatu. Polisi jamii ni kiungo muhimu katika kuondoa changamoto na kero za kiuhalifu. Wahalifu kila siku wanakuja na mbinu mbadala za kihalifu hasa kwenye ulimwengu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, hivyo ushirikishwaji wa jamii ni muhimu sana katika masuala ya ulinzi na usalama wa jamii.

Polisi jamii ( Ulinzi Shirikishi ) unafaida kubwa katika kujenga imani kwa jeshi la polisi na raia pamoja na mbinu za kibunifu kwenye kupambana na wahalifu. Polisi jamii wananafasi kubwa ya kuwahi kwa wakati kwenye matukio ya kihalifu na kutoa huduma ya kwanza ya ulinzi na usalama kabla ya jeshi lenyewe kufika maeneo ya matukio.

DAWATI / IDARA YA ULINZI SHIRIKISHI KWENYE SERIKALI ZA MITAA.
Tafsiri ya Polisi Jamii kuwa Ulinzi Shirikishi imefanya watu kujiona moja kwa moja kuwa na wajibu wa kusaidia masuala ya ulinzi kwenye jamii. Muundo wake umekuwa wa vikundi ndani ya mtaa, kata na vijiji. Lakini muundo huu haujapewa hasa ile nguvu na umuhimu wa uwajibikaji kwa wanajamii wanaojitolea kwa hiari yao kuilinda jamii yao.

Uedeshwaji wake unategemea zaidi, uwepo wa posho ndogondogo zinazokusanywa katika kila nyumba na kusimamiwa na serikali za mitaa, lakini kwakweli haijawa chachu kubwa kwa wanajamii hawa , na kusababisha baadhi yao kujihusisha na uhalifu, kwasababu bado suala hili linaonekana kuwa ni kujitolea zaidi bila kuwa na maslahi yanayo ridhisha. Na kwasasa ulinzi shirikishi wanatazamwa zaidi usiku kuliko mchana, wakati ukweli ni kwamba uhalifu umekuwa mkubwa muda wote, mchana na usiku lakini ulinzi shirikishi umekuwa wa usiku tu na kufanya matukio ya uhalifu mchana kuwa mkubwa zaidi.

Hivyo napendekeza kwa dhati kuwa ulinzi shirikishi Ufanywe kuwa taasisi rasmi ya kijamii kwenye ngazi ya serikali za mitaa na vijiji, kwa wanajamii hawa kupewa mafunzo na jeshi la polisi, kupewa vitendea kazi kama virungu vya kutosha, mavazi ( Sare ), viatu na vifaa vya mawasiliano , lakini pia kupewa uhakika wa maslahi yao kifedha , kwa kufanya makusanyo vizuri ya michango na kuwafikia walengwa na sio wachache kama hali ilivyo sasa.

ULINZI SHIRIKISHI KATIKA CHAGUZI ZA KISIASA.
Katika vipindi vya chaguzi za kisiasa , mfano sasa uchaguzi wa serikali za mitaa na baadae uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na raisi, ni muhimu sana Taifa kuwekeza kwenye ulinzi shirikishi kwa usalama wa raia na mali zao. Maana kipindi hilki ndio matukio Mengi ya uhalifu, mauaji, uvamizi, na uporaji huongezeka maradufu, hivyo kuwekeza kwenye polisi jamii ( Ulinzi shirikishi ) itatoa uhakika kwa usalama wa wananchi kwa utoaji wa taarifa za kihalifu na kufika moja kwa moja kwenye matukio yanayotishia amani ya jamii.

ULINZI SHIRIKISHI KUWA AJIRA RASMI.
Kwa kutambua uzito na unyeti wa masuala ya kiusalama katika jamii, Kuwe na utaratibu maalumu wa maombi ya kazi za ulinzi shirikishi kwenye ofisi za serikali za mitaa, na hata hapo baadae tutambue kuwa ajira rasmi kwa wananchi.

Mfano SUMAJKT, Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa, lina miradi ya uzalishaji mali ikiwemo masuala ya Ulinzi kwenye makampuni, makazi ya watu, viwanda na kwengineko.

Basi iko haja ya kuruhusu serikali za mitaa zitoe fusa za kuwaajiri vijana rasmi kwenye shughuli za ulinzi ili kuwa na ufanisi mkubwa kwenye masuala ya ulinzi wa jamii.

Tutaongeza ajira kwa wananchi, uzalendo, amani, utulivu na umoja katika jamii zetu kwa mustakabari mzima wa taifa letu, na kwa miaka 25 ijayo tutakuwa na taifa lenye usalama wa keli huku kukiwa na umoja, imani na ushirikiano mkubwa kati ya Jeshi la polisi na wananchi lakini pia serikali na wananchi kwa ujumla wake.

HITIMISHO
Napendekeza kuipa nguvu dhana ya ULINZI SHIRIKISHI, kuwa na mfumo wa kitaasisi wenye uwajibikaji, uendeshwaji wa kisasa na kisomi zaidi pamoja na maslahi bora kwa watumishi wake ambao kwasasa wanajitolea na sio kazi rasmi. Wenu katika kulijenga Taifa letu Tanzania , WAPEKEE KEPHAS YOHANA.
 
Upvote 7
View attachment 3023407

Napendekeza kuipa nguvu dhana ya ULINZI SHIRIKISHI, kuwa na mfumo wa kitaasisi wenye uwajibikaji, uendeshwaji wa kisasa na kisomi zaidi pamoja na maslahi bora kwa watumishi wake ambao kwasasa wanajitolea na sio kazi rasmi.
Wenu katika kulijenga Taifa letu Tanzania , WAPEKEE KEPHAS YOHANA.
Polisi Jamii ambao wanahusika katikà suala zima la Ulinzi Shirikishi wengi wao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya Uhalifu hususani nyakati za usiku wakati wanapotekeleza hiyo dhana ya ulinzi shirikishi.
Kwa Maoni yangu ni kwamba Suala hili la Ulinzi Shirikishi lisitishwe kwanza kwa sasa hadi hapo utakapoandaliwa utaratibu mwingine ulio mzuri kwa kazi hiyo.

Aidha, Polisi Jamii wengi wamekuwa Mawakala wa Uhalifu kwa kuwawekea au kuwapandikizia Watu (Raia wema) vitu vya magendo kama vile madawa ya kulevya(e.g. cocaine, bangi, heroin, silaha za Moto, n.k) kwa nia ovu ya kuwalazimisha wahusika (wahanga) kutoa rushwa ili kuepuka kushitakiwa Mahakamani na kufunguliwa Kesi mbaya za jinai. Polisi Jamii pia wamekuwa Mawakala wa kukusanya rushwa mitaani na kuwapelekea baadhi ya Askari Polisi wahalifu waliopo ndani ya Jeshi la Polisi ambao 'wamefunga ndoa' na wahalifu mbalimbali kama vile majambazi, waporaji, wezi, n.k.
 
Polisi Jamii ambao wanahusika katikà suala zima la Ulinzi Shirikishi wengi wao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya Uhalifu hususani nyakati za usiku wakati wanapotekeleza hiyo dhana ya ulinzi shirikishi.
Kwa Maoni yangu ni kwamba Suala hili la Ulinzi Shirikishi lisitishwe kwanza kwa sasa hadi hapo utakapoandaliwa utaratibu mwingine ulio mzuri kwa kazi hiyo.
Na wanafanya hivyo pale tu unapokua mkaidi kulipa hela ya ulinzi shirikishi wanaamua kukuonyesha mfano. Me maoni yangu serikali ibebe jukumu la kuwalipa ulinzi shirikishi ikiwa wamedhamiria kuisaidia jamii
 
Dhana ya ulinzi shirikishi ivunjwe na ikomeshwe kabisa hapa nchini. Jeshi la Polisi litekeleze jukumu lake la Ulinzi wa Raia na Mali zao kwani hilo ndilo lengo Kuu la kuanzisha Jeshi la Polisi hapa Tanzania. Watanzania wanalipa Kodi ili zitumike kuwalipa watumishi wa umma wakiwamo hao Askari Polisi, kwa hiyo ni wajibu wao kutekeleza hukumu hilo la ulinzi wa Raia na Mali zao.
 
Tukiwa shule tuliambiwa kuna masomo ya ziada hivyo mwalimu hawezi kufundisha akiwa kachoka inabidi tumlipe hela. Zingatia hicho nilichokiandika mkuu
 
UTANGULIZI
Ili taifa lolote liendelee, suala la Ulinzi na Usalama ni moja ya jambo nyeti na muhimu sana , kwani limebeba dhana ya kimaendeleo kwa kuwalinda wananchi na mali zao pamoja na kudumisha Amani na utulivu katika jamii. Jukumu hili ni la Jeshi la polisi ndio hasa chombo kinachowajibika kwa ulinzi na usalama wa jamii.

Kwasababu ya kuongezeka idadi ya watu na ukubwa wa mazingira kijiografia, jeshi la polisi pekee bila ushiriki wa jamii katika masuala ya usalama haliwezi kusaidia jamii kwa wakati na weredi mkubwa.
Hapa ndipo dhana ya ulinzi shirikishi inakuja kwa kuishirikisha jamii kwenye masuala ya ulinzi , kama kiungo muhimu cha kulisaidia jeshi la polisi kwenye masala ya uhalifu na uvunjifu wa Amani.

SHERIA NA SERIKALI ZA MITAA.
Suala la Ulinzi na Usalama, kisheria linatambulika kuwa wanajamii wote tunawajibu kushiriki kwenye shughuli za mendeleo ikiwemo Ulinzi na Usalama. Mamlaka ya Serikali za mtaa , yanawapa fursa wananchi kujiunga kuwa kikundi na kupewa mafunzo mbalimbali ya kupambana na kuzuia uhalifu na kudumisha amani.
Dhana hii inasaidia wananchi kutokujichukulia sheria mkononi kwa wavunjifu wa amani , bali ni kuwakamata na kuwakabidhisha katika vituo vya polisi ili sasa sheria ichukue mkondo wake kwa kufata sheria na taratibu. Pia inasaidia upatikanaji wa taarifa muhimu za kiintelejensia kwenye usalama wa jamii.

ULINZI SHIRIKISHI ( POLISI JAMII ).
Kwa miaka 25 ijayo, masuala ya uhalifu ni moja ya changamoto kubwa hasa kwa kuzingatia kasi ya maendeleo na ongezeko la idadi ya yatu. Polisi jamii ni kiungo muhimu katika kuondoa changamoto na kero za kiuhalifu. Wahalifu kila siku wanakuja na mbinu mbadala za kihalifu hasa kwenye ulimwengu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, hivyo ushirikishwaji wa jamii ni muhimu sana katika masuala ya ulinzi na usalama wa jamii.

Polisi jamii ( Ulinzi Shirikishi ) unafaida kubwa katika kujenga imani kwa jeshi la polisi na raia pamoja na mbinu za kibunifu kwenye kupambana na wahalifu. Polisi jamii wananafasi kubwa ya kuwahi kwa wakati kwenye matukio ya kihalifu na kutoa huduma ya kwanza ya ulinzi na usalama kabla ya jeshi lenyewe kufika maeneo ya matukio.

DAWATI / IDARA YA ULINZI SHIRIKISHI KWENYE SERIKALI ZA MITAA.
Tafsiri ya Polisi Jamii kuwa Ulinzi Shirikishi imefanya watu kujiona moja kwa moja kuwa na wajibu wa kusaidia masuala ya ulinzi kwenye jamii. Muundo wake umekuwa wa vikundi ndani ya mtaa, kata na vijiji. Lakini muundo huu haujapewa hasa ile nguvu na umuhimu wa uwajibikaji kwa wanajamii wanaojitolea kwa hiari yao kuilinda jamii yao.

Uedeshwaji wake unategemea zaidi, uwepo wa posho ndogondogo zinazokusanywa katika kila nyumba na kusimamiwa na serikali za mitaa, lakini kwakweli haijawa chachu kubwa kwa wanajamii hawa , na kusababisha baadhi yao kujihusisha na uhalifu, kwasababu bado suala hili linaonekana kuwa ni kujitolea zaidi bila kuwa na maslahi yanayo ridhisha. Na kwasasa ulinzi shirikishi wanatazamwa zaidi usiku kuliko mchana, wakati ukweli ni kwamba uhalifu umekuwa mkubwa muda wote, mchana na usiku lakini ulinzi shirikishi umekuwa wa usiku tu na kufanya matukio ya uhalifu mchana kuwa mkubwa zaidi.

Hivyo napendekeza kwa dhati kuwa ulinzi shirikishi Ufanywe kuwa taasisi rasmi ya kijamii kwenye ngazi ya serikali za mitaa na vijiji, kwa wanajamii hawa kupewa mafunzo na jeshi la polisi, kupewa vitendea kazi kama virungu vya kutosha, mavazi ( Sare ), viatu na vifaa vya mawasiliano , lakini pia kupewa uhakika wa maslahi yao kifedha , kwa kufanya makusanyo vizuri ya michango na kuwafikia walengwa na sio wachache kama hali ilivyo sasa.

ULINZI SHIRIKISHI KATIKA CHAGUZI ZA KISIASA.
Katika vipindi vya chaguzi za kisiasa , mfano sasa uchaguzi wa serikali za mitaa na baadae uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na raisi, ni muhimu sana Taifa kuwekeza kwenye ulinzi shirikishi kwa usalama wa raia na mali zao. Maana kipindi hilki ndio matukio Mengi ya uhalifu, mauaji, uvamizi, na uporaji huongezeka maradufu, hivyo kuwekeza kwenye polisi jamii ( Ulinzi shirikishi ) itatoa uhakika kwa usalama wa wananchi kwa utoaji wa taarifa za kihalifu na kufika moja kwa moja kwenye matukio yanayotishia amani ya jamii.

ULINZI SHIRIKISHI KUWA AJIRA RASMI.
Kwa kutambua uzito na unyeti wa masuala ya kiusalama katika jamii, Kuwe na utaratibu maalumu wa maombi ya kazi za ulinzi shirikishi kwenye ofisi za serikali za mitaa, na hata hapo baadae tutambue kuwa ajira rasmi kwa wananchi.

Mfano SUMAJKT, Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa, lina miradi ya uzalishaji mali ikiwemo masuala ya Ulinzi kwenye makampuni, makazi ya watu, viwanda na kwengineko.

Basi iko haja ya kuruhusu serikali za mitaa zitoe fusa za kuwaajiri vijana rasmi kwenye shughuli za ulinzi ili kuwa na ufanisi mkubwa kwenye masuala ya ulinzi wa jamii.

Tutaongeza ajira kwa wananchi, uzalendo, amani, utulivu na umoja katika jamii zetu kwa mustakabari mzima wa taifa letu, na kwa miaka 25 ijayo tutakuwa na taifa lenye usalama wa keli huku kukiwa na umoja, imani na ushirikiano mkubwa kati ya Jeshi la polisi na wananchi lakini pia serikali na wananchi kwa ujumla wake.

HITIMISHO
Napendekeza kuipa nguvu dhana ya ULINZI SHIRIKISHI, kuwa na mfumo wa kitaasisi wenye uwajibikaji, uendeshwaji wa kisasa na kisomi zaidi pamoja na maslahi bora kwa watumishi wake ambao kwasasa wanajitolea na sio kazi rasmi. Wenu katika kulijenga Taifa letu Tanzania , WAPEKEE KEPHAS YOHANA.
Asante sana
 
Back
Top Bottom