JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Simu yako inapofanya kazi taratibu kupita kawaida ni dalili moja wapo ya simu yako kuwa imeathiriwa na virusi. Kila Mtu anatarajia simu yake nifanye kazi sawa sawa na kwa haraka
Simu yako inaposimamisha utendaji (Stucking) mara kwa mara ni dalili nyingine ya kuonesha kuwa simu yako imeingiliwa na virusi.
Betri ya Simu kuisha kwa haraka hata bila ya simu kufanya kazi kwa muda mrefu. Virusi kuendelea kufanya kazi bila ya ruhusa ya mmiliki wa simu. Hii inasabanisha betri kuwa na kazi kubwa na kuisha haraka
Kila ukifungua 'Browser' yako unakutana na matangazo mengi ya biashara hata ambayo hakuwahi kufuatilia. Virusi vinaweza kutumika kifanya matangazo ya biashara
Simu kuwa na Application ambazo hujawahi kuzipakua (Download) ni dalili nyingine kuwa simu yako imeingiliwa na virusi
Simu kuwa na matumizi makubwa ya Vifurushi vya Intaneti, pia ni dalili ya simu kuwa na virusi. Watu wengi hulalamika Vifurushi kuisha bila ya kutumika sawasawa, wakati mwingine ni kwasababu ya virusi
Jinsi ya kuondoa 'Virus' kwenye Simu ya Android
Ondoa 'application' usiyoitambua katika simu yako: Kama simu yako ina application ambayo huitambui tafadhali iondoe yawezekana imeletwa na kirusi au yenyewe ni kirusi
Tumia 'Antivirus' kuondoa virusi kwenye simu yako: zipo Antivirus nyingi sana lakini unashauriwa kutumia Antivirus zifuatazo Kaspersky, Avast, Norton na AVG. Tafuta moja kati ya hizo kwenye Play Store kisha itumie kujisafisha simu yako. Tumia Antivirus moja usiweke mbili
'Reset Factory' kwenye simu yako: kabla kutumia njia hii, hakikisha umehifadhi taarifa zako (picha, nyimbo na vitu vingine) kwa lugha rahisi Hakikisha umefanya backup ya taarifa zako. Reset Factory kwa hatua zifuatazo;
Settings > System > Advanced > Reset options > Erase all data. Utaondoka kila takataka kwenye simu yako na itaanza upya kama simu mpya
-
Endelea kujilinda: kila ukitaka kupakua application mpya hakikisha umeipata Playstore au kwenye chanzo kingine cha kuaminika. Hakikisha umeujua undani wa App husika kabla ya kupakua

Upvote
1