Ulinzi wa Sergio Ramos na Pepe ni ulinzi hatari zaidi kuwahi kutokea kwenye soka

kalisheshe

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
2,064
Reaction score
4,056
Hii ilikuwa ni partnership tishio na hatari zaidi kwa washambuliaji wengi.

Ilikuwa ni nadra kwa mechi ya Real Madrid kuisha bila red card kwa mmoja kati ya hawa walinzi.

Mhanga mkubwa wa partnership hii alikua ni LIONEL MESSI, siku nikibahatika kukutana nae nitamuuliza ni kipi kilikuwa kichwani mwake akijua kuna game na hawa jamaa.

Wachezaji mlenda mlenda kama wa zile (timu za Kariakoo) walikuwa hawawezi kufurukuta mbele ya hawa jamaa.

Tupia unachokikumbuka kuhusiana na Hawa jamaa.
 
Hawana lolote zaidi ya kucheza rafu kwa watu ambao wanawadharau,ushawahi kuona mechi walizokutana either wamkabe Ibrahimovic au Diego Costa? Hao majamaa hawana huruma wana rafu za chini chini kuna mechi Ramos alikuta a na Diego Costa kidogo ateme ulimi, anamfanyia rafu diego costa ila kwenye hiyo hiyo diego costa anapita naye mara kamkanyaga kichwa kama bahati mbaya na refa anapeta ,Ramos aliiva kweli.
 
Nakumbuka vizuri
 
Franco Baresi & Paolo Maldini ilikuwa bonge la patnership lakini kama hukufanikiwa kuwaona kuna miaka ya karibuni kuna John Terry & Ricardo Calvalho waliruhusu goli 15 tu msimu mzima wa EPL huku wakiwa na clean sheet 24 kwa msimu huo kwenye EPL tu...rekodi inayosimama mpaka leo
 
Hahahahahaaaa,Aisee umenikumbusha hii mechi mpaka Ramos alikuwa mpole
 
Maldini vs nesta
Terry vs calvaiho
Vidic vs Fred and
Stam vs Blanc
Cordoba vs marterazzi
Canavaro vs tarchnand
Yondani vs nyoso
Masatu vs magoso
Kimanda vs aswile
Patrick Viera na Roy Keane shughuli ilikua ni pevu sana.
 
Hapo wakiongea kama marafiki wakati mmoja wao ametoka kukanyagwa 😁😁
 

Hii ilikuwa ni teke la shingo, Ramos shughuli aliipata kweli siku hiyo.

Mwanaume vs Mwanaume
 

Messi akikutana na madrid anajipigia tu,,chelsea mliyokua mnasema hakuwahi na hataweza kuwafunga basi aliwafunga na kuwaziba midomo,, kwa buffon pia aliwaziba midomo, upande wa national team, timu kubwa alizowahi kuzifunga na ubora wa mabeki wao. Huyu ndie messi, mchezaji bora kuwahi kutokea.
 
Maldini vs nesta
Terry vs calvaiho
Vidic vs Fred and
Stam vs Blanc
Cordoba vs marterazzi
Canavaro vs tarchnand
Yondani vs nyoso
Masatu vs magoso
Kimanda vs aswile

Sorin and Samuel walter
Heinz and rio Ferdinand
Zanetti and Materazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…