Uliowaambia njia ipi utapita ndio wametangulia kuweka miiba ili ukwame

Uliowaambia njia ipi utapita ndio wametangulia kuweka miiba ili ukwame

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Kuna sehemu unafika kirahisi kwa sababu ulipunguza watu wakujua njia ipi utapita na tena hata kuwafanya wakuone tayari umefika

Sio kwa ubaya ila kwa manufaa yako mapana ni kheri upunguze kuropoka hovyo kwa sababu sio wote watafurahia kusikia jinsi utavyokuwa mbeleni hivyo wako tayari kwa gharama kubwa wazuie michakato ya wewe kufika huko.

Iwe makazini ukiwa mtu wa kuropoka hovyo mazuri yako usishangae ukanyimwa hata ruhusu ya kuondoka au ukasumbuliwa kuipata hiyo ruhusa kwa sababu wanajua unaenda kufanya ambayo wao hawana au mazuri wasiyotaka uyapate.

Ni kweli binaadamu tunatamani watu wajue mazuri yetu ya sasa au ya kesho lakini inatakiwa utulivu na umakini wa juu wa kujua nani ajue na nani ashitukie ukiwa juu tayari.

Tupo kwenye harakati ila ndani ya hizo harakati kuna kuwindana , wewe ukiwaza kufanya zuri kuna mwingine anawaza namna ipi akuharibie.

#Fikia Ndoto Zako
#Mwanasayansi Saul kalivubha
 
Better still wewe fanya yako wala usiangalie watu wanasemaje au kutumia muda wako kutafuta uchawi...

Mara nyingi unaweza ukajishitukia kwamba fulani wanakuonea wivu / hawakupendi / wanakukwamisha kumbe wala haupo kwenye mawazo yao.... i.e. unapigana vita mwenyewe...

Huenda perception yangu ikawa tofauti ila its coming from a man who believes in building bridges rather than walls...
 
✍️
 
Natumaini kizazi cha tiktok, insta na fesibuku wamekusikia
 
Back
Top Bottom