Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WANANCHI WA LUDEWA KULIPWA FIDIA KUPISHA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia watanzania kuanza kwa utekelezaji wa miradi mikubwa wa Liganga na Mchuchuma Wilayani Ludewa Mkoani Njombe baada ya kuanza ulipaji fidia kwa wananchi.
Akizungumza kwa njia ya simu na wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi wa zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yenye madini hayo Mhe. Rais Samia amesema kuwa lazima wananchi wote walipwe fidia pamoja na kushughulikia changamoto zote zilizojitokeza ili miradi hiyo mikubwa ianze.
"Nataka niwaahidi fidia zote zitalipwa na kama kutakuwa wataalamu wamekosea, kuna watu wameachwa tutaliangalia lakini tunahakika tunalipa fidia ambayo tulishaifanyia kazi vizuri, ahadi yetu kwenu baada ya kulipa fidia mradi sasa utaendelea, Mchuchuma na Liganga sasa utakwenda kuchangamka,ajira zitakwenda kupatikana, kodi kwa halmashauri zitakwenda kupatikana kutokana na mradi kuwepo,kwa hiyo niwaombe wananchi tushirikiane katika utekekezaji. Katika malipo kila mtu achukuwe anachostahiki halafu kwa vema tuje kushirikana kwenye mradi" alisema Mhe Rais
Kwa upande wake Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ambae alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo ,amesema kuwa Wizara sasa inaanza kwa kasi kubwa kutekeleza mradi wa madini hayo baada ya Serikali kuwalipa wananchi fedha zao.
"Sisi sasa kama watendaji ndani ya wizara hii tuko tayari kukimbia na wawekezaji ili mradi wetu huu uanze kutekelezwa,mradi huu wa Liganga na Mchuchuma ni mradi ambao unahistoria ndefu na ya muda mrefu ni mradi unaojumuisha uchimbaji wa chuma cha Liganga pamoja na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma ambapo kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Serikali mradi huu unaumuhimu mkubwa kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yetu"alisema Dkt. Kijaji.
"Wizara tuko tayari kukimbia na wawekezaji ili kutekeleza Mradi wa Liganga na Mchuchuma wenye historia ndefu unaojumuisha uchimbaji wa chuma cha Liganga pamoja na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma wenye umuhimu mkubwa kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yetu" - Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji -WUVB
"Nataka niwaahidi fidia zote zitalipwa, tunahakika tunalipa fidia ambayo tulishaifanyia kazi vizuri, Mradi wa Mchuchuma na Liganga utaendelea, ajira zitapatikana, kodi kwa halmashauri zitapatikana. Wanachi tushirikiane katika utekelezaji" - Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mwaka 2013 Tafiti ya Makaa za Mawe pamoja na Chuma zilifanyika na kugundua kuna tani milioni 428 za Makaa ya mawe ambazo zinaweza kuchimbwa kwa miaka zaidi ya 140 na Chuma ni zaidi ya tani milioni 126 ambazo zinaweza kuchimbwa kwa miaka 58.DG - NDC Dkt. Nicolaus Shombe