Ukweli ni kuwa Kikwete aliwekwa madarakani na kundi dogo sana lenye nguvu kubwa sana kifedha, na kundi hili ndilo Kikwete amekuwa akilitumikia na kuwajibika kwalo. Kinachofanyika sasa hivi ni namna ya kurudisha fedha ya hawa waheshimiwa waliomweka ikulu kabla ya uchaguzi wa 2010. Kama unafikiri vinginevyo subiri mwaka wezi wa EPA watakaopelekwa mahakamani. Tumesikia jana kuwa kwa kuwa EPA ni suala la miaka zaidi ya 20, na lilihamia BOT toka NBC kipindi ambacho hata kompyuta hazikuwepo hivyo kupotea kwa nyaraka nyingi muhimu. If this is what the president is telling our esteemed MPs, mwananchi wa kawaida atakuwa na matumaini gani? We are simply lost.