Ulishawahi kudanganywa kwenye mahusiano?

Ulishawahi kudanganywa kwenye mahusiano?

Dollar hermees

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
517
Reaction score
1,045
Habari wana JF leo nina bonge moja la tukio ambalo sijawahi kulipitia maisha yangu yote.

Mahusiano ni moja ya kitu chenye changamoto sana katika maisha yetu haswa sisi wanaume. Kutokana na asili ya wanaume tulivyo basi kuingia katika mahusiano ni committment na sio mazaha kwa sababu unajua zile mechi za nnje zina kuwa kando kidogo au kama zitakuwepo basi zinafanyika kwa ustadi wa hali ya juu.

Tuishukuru sana technology kwa sababu imerahisisha sana kwetu sisi wanaume katika suala zima la kutongoza. Wengi wetu tunajua kabisa demu akisha kupa namba basi uhakika wa kumpata huyo demu ni zaidi ya 70%, kiufupi ni suala la mda tu.

Wengine wanachukua mzigo siku hiyo hiyo na wengine wiki miezi mpaka mwaka ila lengo lisha timia.

Sasa hivi vijana wengi mademu wengi tuna wapata kupitia mitandaoni kwa maana ya social medias kama Snapchat, Facebook, Twitter na Instagram mkubwa wao. Japo watu wanayapinga mahusiano ya mitandaoni na kuyaona ni fake na uigizaji tu.

Niseme tu kweli na wala sikatai ila watu wanashindwa kuelewa huyo demu ale kutana nae au huyo mkaka, Je wana malengo sawa? Wengine kweli wanajuana kupitia mitandao na wana owana alafu fresh tu maisha yanaendelea mapaka wanakuwa na watoto.

Lakini kwa upande wapili sio hivo watu wanatumia mtandao kufanya utapeli, wengine umalaya wakina siye hapa, wengine kufanya biashara, wengine kuelimisha jamii na wengine hata kufikia hatua ya kutengeneza connection na watu wakubwa kabisa kama wasanii na kadhalika.

Sasa twende kwenye mada kuu ya kudanyanganya kwenye mahusiano. Nifuate...

Mwaka jana mwishoni, December nilijitoa rasmi kuingia kwenye mahusiano na mwanadada mmoja mzuri sana kupitia mtandao mmoja wa kijamii jina kapuni.

Huyu dada nilizoeana naye sana kufikia hatua ya kuzoeana naye na kuanza stori za hapa na pale mwishowe tuka anza mahusiano.

Mi najua wahuni mtasema mahusiano mpaka ule mzigo lakini sio hvo bana, unaweza date na demu hata mwaka lakini nguo huja mvua lakini huo ni ufala.

Point yangu ni kwamba alikuwa demu wangu sema tu bado hatuja onana. Demu aliniambia ana kaa mitaa ya Tabata hivo basi hii stori inahusu mazingira ya Dar es Salaam.

Demu ni mtu wa Singida kwahyo akaniambia atasafiri hivi karibuni kwenda kwa kaka yake kusimamia ujenzi wa nyumba huko Singida, yote hiyo ni December mwishoni.

Urafiki na yeye ulianza mda mrefu ila uhusiano rasmi ulianza December. Toka January mtoto yupo Singida kwa bro anasimamia ujenzi me hapo mda wote tunachat kupitia hiyo social network baadae akanigea namba yake fresh nikawa nachat naye WHATSAPP LAKINI SIO VIDEO CALL WHATSAPP.

Akanishauri ni download app ya IMO MESSENGER ili tuweze kupiga mavideo call mzee baba. Muhuni kama kawaida chap tu unajituma si unajua mzigo nitakula tu.

Tumeenda tumeenda Ramadhani inakaribi namuuliza demu unakuja lini wakati huo nilikuwa na ile pisi kali yazenji stori yake nisha wapea tayari nilivo mla kimasiahara kwa siku moja.

Mpaka nikagombana na yule dem wa zenji kisa huyu wa Singida bado ana niambia anakuja tu. Asema tusubiri Ramadhani ishe ndo atakuja, muhuni nikasema haina noma kwani siku ngap 30 tu.

Hizo apo zimekata demu bado ana nipiga fix. kipindi hicho Corona everywhere kwahyo demu akatumia hicho kama kigezo.

Nikamwambia sawa wacha tusubiri usafiri ukae sawa hapo demu aniambia atapanda ndege basi hapandi, nikasema sawa wakishua.

Mzee Magu akaruhusu ndege kuingia na kutoka hapo nadhani ni mwezi wa 5 tayari ndo akaruhu ndege za International kuingia bongo.

Niki muuliza demu vipi mbona huji ana niambia kuna mzigo ana usubiria. Me najiuliza huyu demu nita mtafuna lini wakati kwenye video call huko, tuna nyegeshana kila uchwao alafu napigwa tarehe. Hili jambo lina tuumiza sana wahuni.Ni kama vile demu anasema anakuja alafu hatokei.

Demu ana nipiga fix tu mara kuna mzigo kaagiza anausibiria ndo aniletee. Mara demu kaenda kwa shangazi kuna msiba, Mara demu kaenda kutembea KIOMBIO HOTEL.

KUMBE NI UWONGO MTUPU. Mwezi huu wa saba ulivo ingia nikaona drama zimekua nyingi ngoja nimuelezee mshkaji wangu mmoja hili sakata. Vile nili kuwa namsimulia ndo akili ikafuguka kuhisi demu ni mzinguaji.

Nilianza kumbana kwa kumpiga maswali kuhusiana na kuhakiki line za simu kupitia majina yake ya NIDA.

Demu nikimwambia acheck kwa *106# anasema eti no network kumbe MUONGO. Nikimwambia a screenshot anitumie nione anasema simu ya Samsung Galaxy s7 kweli haina option ya screenshot.

Namalizia maana stori naona nikiandika hivi hasira zina zidi kunipanda. Siku za hivi karibuni nikamtumia message nika muuliza aniambie yeye ni nani? katumwa na nani na yuko wapi? Alafu nikapotea.

Majibu aliyo nipa nili shika kichwa. Kumbe mda wote huo toka January demu yupo Dubai kanificha na hakuwa Singida wala Dodoma. Mbaya zaidi nilivo kuwa nikimpigia video call always nakum kuta kwenye same place n environment yani chumbani kwake. Kwahyo bana wakulungwa wenzangu nimedanganywa miezi 7 consistently bila hata huruma mtoto watu na nika muuliza kwanini amefanya yote hayo eti kisa tumejuana mtandaoni ndo maana kanificha ,mara OOH nilitaka nikufanyie suprise, mara sikupanga nikwambie nilitaka nikuambie tukionana.

Yote hayo Corona ime muumbua. Wadau niseme kitu usione mwamba kamzibua mkewe ukaona ni mdhaifu mshakaji au laa.

Me mwenye huyu demu kama angekuwa bongo au nimeona naye uso kwa uso angechezea kipigo. Kama nilivo sema mwanzo wa stori wanaume tukiingia kwenye ndoa au mahusiano basi tuna sacrifice vitu vingi sana ndo maana tuki umziwa tunapagawa. ila kwa wanawake kwao ni advantage atahudumiwa, atatunzwa na atalindwa pia.

Ni uwongo gani uliwahi kudanganya na mpenzi wako huto usahau mpaka leo. Wangu mie ni huo hebu share nasi wakwako ilikuwaje. Ila tujifunze sio kila king'aacho ni dhahabu.

AHSANTE KWA KUSOMA UZI HUU NAIMANI UMEJIFUNZA KITU.
 
Dah umenikumbusha ,nilivyodate na demu messenger kwa mda wa miaka mitatu bila kujua ashaolewa na pia ana watoto wawili tayr, stori iko hivi, nikiwa form four ,nilitokea kupendwa sana na mrembo wa darasa mpaka tunamaliza ,ila mwenzangu baada ya kumaliza alienda India kusoma ,mda wote tuliendelea kudate ati akirudi tutaoana ,dah after three years nilikuja jua kuna wa kishua mmoja ashaweka ndani na mambo ya masomo ilishabaki story ,kila nikikumbuka uwa nasinzia
 
Sasa una uhakika gani kama hayo maelezo ya kuwa dubai ni ya kweli wakati siku zote unadanganywa?
 
Dah umenikumbusha ,nilivyodate na demu messenger kwa mda wa miaka mitatu bila kujua ashaolewa na pia ana watoto wawili tayr, stori iko hivi, nikiwa form four ,nilitokea kupendwa sana na mrembo wa darasa mpaka tunamaliza ,ila mwenzangu baada ya kumaliza alienda India kusoma ,mda wote tuliendelea kudate ati akirudi tutaoana ,dah after three years nilikuja jua kuna wa kishua mmoja ashaweka ndani na mambo ya masomo ilishabaki story ,kila nikikumbuka uwa nasinzia

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu uzuri umenifikirisha sana, pole mkuu
Umenikumbusha nyimbo ya Just a dream, Nelly
 
alinidanganya kuwa bikra kumbe bwawa na mm nikamdanganya kuwa siwez kuishi bila yeye, ila naishi hadi leo
 
Dah umenikumbusha ,nilivyodate na demu messenger kwa mda wa miaka mitatu bila kujua ashaolewa na pia ana watoto wawili tayr, stori iko hivi, nikiwa form four ,nilitokea kupendwa sana na mrembo wa darasa mpaka tunamaliza ,ila mwenzangu baada ya kumaliza alienda India kusoma ,mda wote tuliendelea kudate ati akirudi tutaoana ,dah after three years nilikuja jua kuna wa kishua mmoja ashaweka ndani na mambo ya masomo ilishabaki story ,kila nikikumbuka uwa nasinzia
dah sio poa kabisa. alafu kwao kudanganya wanaona simple sana
 
Hadi saa hii natype hapa kwenye uzi huu Nadanganywa yaani naambiwa uwongo kama wote. Halafu nishajua ukweli sema nimeamua kuzoea uwongo wake ili niendelee kuenjoy nae nampenda sana 😂😂😂😂
 
Hadi saa hii natype hapa kwenye uzi huu Nadanganywa yaani naambiwa uwongo kama wote. Halafu nishajua ukweli sema nimeamua kuzoea uwongo wake ili niendelee kuenjoy nae nampenda sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kama kweli umempenda basi komaa nae ipo siku atakwambia ukweli
 
Back
Top Bottom