Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Tokea umejitambua je, ulishakaa chini na kujiuliza maswali haya? Kama ulishawahi kujiuliza. Je, ungependa kutushirikisha majibu uliyopata? Karibuni.
- Je, kuna tofauti yoyote kati ya mtu kuishi duniani na kuwepo duniani
- Kuna kitu chochote umekiweka moyoni mwako iwe kwa muda mfupi au mrefu ambacho usingependa kiendelee kuwepo?
- Je, unafurahia jinsi ulivyo? Unajikubali au ungependa kuwa kama mtu fulani?
- Mara nyingi tumezoea kusema mtu hujifunza kutokana na makosa. Kama tunajifunza kutokana na makosa kwanini tunaogopa kufanya makosa?
- Kama maisha ni mafupi kiasi tunachofikiri, kwanini wakati mwingine tunalazimika kufanya mambo au kazi tusizozipenda na kujikuta tunatamani mambo au kazi ambazo tunashia kutokuzifanya kabisa maishani mwetu?
- Endapo ungepewa uwezo wa kuangalia yaliyomo ndani ya moyo wa adui yako,unafikiri ungekuta nini ambacho ni tofauti na kilichomo ndani ya moyo wako ?
- Kwanini unafikiri kuishi kwako au kuwepo kwako duniani ni muhimu?
- Leo ingekuwa ndio siku yako ya mwisho kuwepo duniani, je, bado ungefanya kile ulichokuwa umekusudia kukifanya leo?
- Je, ni kitu gani unachofikiria kinakukwaza kufikia malengo uliyojiwekea katika maisha yako? Na unafanya jitihada gani kukiondoa?
- Kitu gani unachokijua sasa ambacho unajuta kwa kukijua katika maisha yako?