YonDu Udonta
JF-Expert Member
- Aug 6, 2016
- 723
- 569
Wakuu, salama?
Kwanza niseme hivi. Usiku wa kuamkia leo kama ningekuwa na mguu wa kuku, basi ningemwaga ubongo wa mtu!
Ilikua hivi: Baada ya kuangalia mpira wa Simba na Mtibwa, ikabidi nihamishie channel pendwa ya mieleka lakini sikuweza kumaliza kipindi nikawa nimepitiwa na usingizi pale pale kwenye sofa.
Hamadi! Nafungua macho nakutana na mti unavuta kilongalonga changu. Aisee sikumbuki nilifikaje dirishani na zile speed lakini nilipiga ngumi dirisha yule mwizi aliruka kwa uoga akijua kuwa ngumi imempata ila kumbe nilikua nimepiga nondo; alivyoamka hapo alikimbia na speed 120 na mimi kubakiwa na mti wake.
Huu wizi hutumia technique ya kufunga kandambili iliyochongwa vizuri mbele ya mti na huipaka Super Glue ili wabebee simu yako kwa urahisi.
Je, wewe ushawahi kukutana na ghasia hii?