Ulishawahi kukutana na kisanga wakati unapita/kukaa karibu na makaburi

Ulishawahi kukutana na kisanga wakati unapita/kukaa karibu na makaburi

Nshomile wa Muleba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
2,166
Reaction score
5,620
Kuna wakati ndugu(mjomba) yangu alinunua kiwanja maeneo ya Morogoro na akaanza kujenga guest house kwa haraka sana mpaka ikakamilika na wakati huo nimemaliza form 6.

Basi anko akasema kuwa niende nikasaidie kazi hapo guest na atakuwa ananilipa (usimamizi)

Banaaa kumbe ile guest ilijengwa juu ya makaburi ya miaka 1990 huko na watu walishayasahau na wakauza maeneo.

Visa vikaanza
Unakuta uko rum umelala unasikia watu wanacheka, mara sauti inakuambia “Tokeni kwenye nyumba yangu”

Ukiacha msosi unakuta umepotea ghafla, au ukienda toilet usiku taa zinazimika ghafla,

kuna ile moja iliniacha hoi, nikiwa nimekaa receiption nikaiitwa na mlinzi mara moja ili kurudi nakuta mikojo kama lita 10 receiption nzima imetapakaa chini

Kiufupi niliaga kwa mjomba kuwa naenda kujiandaa na chuo na wale wafanyakazi walikimbia ile kazi

Mpaka leo kaiita wachungaji na mashekhe ila pameshindikana nilisikia kapauuza.

——————————————

Nyingine nilipita makaubirini maeneo ya Tabata pale jioni mida ya saa 11

Niliona mwanamke amekaa juu ya makaburi afu alikuwa ananiiita, nilijua pengine ni mfiwa anahitaji msaada,

Nikaiitika wito ile namsogelea akapotea ghafla, sijawahi kukimbia kiasi kile maishani

Kiufupi niliishi kwa shida karibia miezi mi3 hv

Je? ni kisa gani ulishawahi kukutana nacho ulivyopita au wakat unakaa maeneno karibu na makaburi, shusha kisa hapa tusome



Nshomile

Kagera, Tanzania
 
Dirisha langu pale hom kwa mzee ni karibu na makaburi kabisa yaani nyumba yetu ya kwanza kutoka makaburini

Hamna Ajabu lolote nlilowahi kuona 😅😅 nmeishi pale zaidi ya miaka 10 ni siku moja tu wakati niko Form 4 niliamka kupiga msuli niliona moto huko ukiwaka ila tofauti na hapo sijawahi kushuhudia chochote.
 
Tuliwah kuishi karibu na makaburi lakin sikuwah kuona chochote cha ajabu,choo kilikuwa kipo karibu kabisa na makaburi na kuna wakati tulikuwa tunaenda kujisaidia usiku mkubwa lakin sikuwah kuona kitu

Ila kuna kitu niliwah kukiona makaburin siku moja hadi nilishangaa,niliona kijana na binti wamekaa juu ya kaburi wanapiga story,nilishindwa kuelewa ujasiri wa huyo binti aliwezaje
 
Iliwahi mtokea mtu wangu wa karibu .......mitaa 200 kabla ya kukaribia haya madude ......
.akawa anasikia watu wanaongea Kwa sauti....so akaanza kuwakimbilia Ili apate escort ya kupitia pale coz ilikuwa usiku

Kila anavyo anavyopiga hatua.....zile sauti zinadhidi kusogeza mbele Kila akikimbia pia sauti + vicheko vinasogea mbele .....lkn haoni watu

Baada ya kufika katikati upepo mzito ulivuma kukawa kimya .......mbio alizochomoka Sasa[emoji23][emoji23]
 
Dirisha langu pale hom kwa mzee ni karibu na makaburi kabisa yaani nyumba yetu ya kwanza kutoka makaburini

Hamna Ajabu lolote nlilowahi kuona [emoji28][emoji28] nmeishi pale zaidi ya miaka 10 ni siku moja tu wakati niko Form 4 niliamka kupiga msuli niliona moto huko ukiwaka ila tofauti na hapo sijawahi kushuhudia chochote.
Yah kiukweli kabisa hata mimi nimeishi nyumbani panatazama na makaburi nilichowahi kuona ni moto unawaka tu pia naimani ni binadamu wa kawaida walikuwa na ishu maalum tu pale kwasababu mara nyingi hata mida ya sa 2 usiku inaweza kuja gari ikapaki then watu wakafanya yao wakasepa.
 
Kuna wakati ndugu(mjomba) yangu alinunua kiwanja maeneo ya Morogoro na akaanza kujenga guest house kwa haraka sana mpaka ikakamilika na wakati huo nimemaliza form 6...
We jamaa ni muongo yani umalize form 6 tena uage ukasome pre form 5
 
Back
Top Bottom