Ulishawahi Kuonewa utotoni au Ujanani??Tuambie ilikuaje na ulifanyaje??

Ngareroo

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2019
Posts
2,123
Reaction score
2,449
Aslaa Aleykum ndugu zanguni,,Eid Mubarack kwa wana JF ila ukini'PM au ukinitext kuhusu nikualike unione kimya jua nakufikiria...

(MBILI 3 ZA MZAMBULI)
MZAMBULI:Koh! Koh!..duuh ya Leo wakurungwa mmeitolea kwa pusha gani?hii sio ya Haji machalii zangu.

MIMI:Iyo niaje tumeidakia fas ya pale downika kwa Bob kill anavitu viko lit kisoro hanaga famba yule mkushi.

MZAMBULI:sasa skieni wajuba,hivi mnajua siku tukitimba Mbinguni kwa Sir God,God atatutenga makundi mawili,moja la wale waliokua wanasali sana church na msikitini ila hawachomi cha ukucha,,Alaf kundi la pili ni letu sisi wajuba wachoma kaya ambao hata church hatujawahi timba,umeona ile pale?!

MIMI:Ushaanza story zako za ki'whack kikosi wangu.

MZAMBULI:Ngareroo skiliza nikuelekeze acha perepete buddah.

MZAMBULI:Baada ya kututenga makundi mawili Mungu atawaambie wale waliokua wanasali ila hawali weeda.

SISI:Atawaambiaje sasa,teh.

MZAMBULI:Atawaambia kwa upole kuwa"Nyie mlikua mnasali sawa,ila sasa mlikosea kitu kimoja muhimu sana,,Hamkula dawa(hamkuvuta Bangi)",alaf sisi wahuni tunaenda Peponi wao Motoni.

SISI:Hahahah mzambuli we ni ****.

(TARGETED STORY)
Utotoni miaka kama12 au 13 hivi mwaka2011 nilitimba kijijini kwa Babu Monduli,mzee alikua na Ng'ombe wa kuzidi fas zile,,bas nikawa namsindikiza mchungaji kuwachunga wale wanyama daily tunasololoa mokomoko kwa ngoko...

Sasa machungani kulikua na chalii flani ivi li'maasai limepanda hewani linaitwa Molell likorofi alaf libabe kiquma,lilikua linachimba viazi alaf tunavichoma,ila kuvila viazi hadi mpigane kwanza,ukimpiga mwenzio ndo unakula kiazi alaf ukidundwa unakula maganda kubabake sio poa ani...

Jamaa lenyewe si ndo linatubonda wote so likawa linachagua kila mtu na wake mnakiwasha fas duas pale eeh wiuwiu bablai,lenyewe ndo linacheki game coz tulikua wa4 lenyewe la5...

Unaambiwa sikuwahi kula viazi yaani daily ni maganda2 alaf bora yangekua ya viazi vibichi ni matamu,maganda ya viazi vya kuchomwa sawa na unakula majivu au mkaa chaliangu..lilikua linaniita Msomali au macho kutokana na asili yangu ya usomali,utaskia linasema apo baada ya mpambano kuisha"Oyaa Davie chukua kiazi alaf menya maganda umpe Msomali,msomali gani wewe huwezi vita Eroo?kesho uje na mabomu ya Mogadishu utulipue ule viazi fala wewe"...

Daah ilikuaga ni kisangalai washkaji zangu,,tuambie nawewe kisanga chako cha kuonewa utotoni ilikuaje?


@NgarenaroBoy.
 
Duuh mhuni umetumia lugha ngumu 😂😂
Ngareroo Slangs iyo Chaliangu,,njoo Ngalimi,Ngarenaro,Daraja mbili,Kijenge Juu ujifunze coz muda so mrefu itaidhinshwa na BAKITA itumike rasmi Afrika tumeongea na mzee Oni Mafegi kasema yechu.
 
Nishakusoma Aptii (Mogadishu) fasi ya Kijiji balaa arifu.. uongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…