Ulishawahi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti mliyeshibana sana?

A, tulikuwa mabest enzi zile hakuna Tv wala nini si vitabu kuazimana.SAsa yuko Bank moja hapo mjini boss.Ila hatuwasiliani kivile siku moja moja nazukaga ofcn kwakwe km mzuka tunacheka na kufurahi na lunch tukipat imeisha hoyo.
 
Habari zenu wakuu,

Nimemkumbuka kaka fulani tulikuwa marafiki sana tangu nikiwa secondary. Kwa miaka 10 alikuwa mtu wangu wa karibu sana, mshauri wangu kwenye kila Jambo.
Yes, I do have! Nina rafiki yangu ambaye tulikuwa pamoja. Wazazi wake waliletwa kufanya kazi ktk mji niliozaliwa bahati nzuri walipata nyumba ya pembeni yetu. Huyu dada tumezaliwa mwaka mmoja, kaka zake na dada zake walikuwa marafiki zangu sana.

Huyu dada, tulisoma na kucheza pamoja, alikuwa kama pacha wangu. Watu walituzushia kuwa ni wapenzi lakini haikuwa hivyo. Baada ya masomo ya msingi nilibahatika kwenda kusoma sekondari ktk mkoa wa Kilimanjaro yeye hakubahatika kuchaguliwa. Barua zake zilikuwa haziishi (enzi zetu hakukuwa na simu za mkononi). Yeye baadae alienda kuishi kwa dada yake Tabora ambaye alikuwa ni muuguzi. Baada ya kuhitimu kidato cha nne nilipangiwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita ktk shule moja Tabora. Ilikuwa nifuraha kubwa sana kwangu kwenda kukutana tena na huyu rafiki yangu kipenzi. Nilimkuta akichukua kozi ya UUGUZI MSAIDIZI. Urafiki wetu uliendelea.

Baada ya kumaliza masomo na kumaliza pia mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria nilipata bahati ya kwenda kusoma nje ya nchi kwa miaka kadhaa. Kwa muda wote huo mawasiliano yangu na huyu mdada hayakukoma. Nikiwa bado nje ya nchi kwa masomo, huyu dada alipata ajira ktk hospitali ya Mkoa ktk mji ule niliozaliwa. Alibahatika kuolewa na bwana mmoja mfanya biashara. Bahati mbaya, huyu rafiki yangu hakubahatika kushika mimba na hapo mateso, manyanyaso na vipigo vilianza. Ndoa yake ikaingia ktk mgogoro. Tuliendelea kuwasiliana na mara chache nilipopata nafasi nilimpigia simu.

Niliporudi nilimkuta bado yupo ktk ndoa yake lakini ilikuwa bado na mgogoro mkubwa. Mume wake tulikuwa tunafahamiana kwani tulisoma naye na kucheza naye mpira wa kikapu. Baada ya kurudi, huyu Bwana hakuniamini alidhani natembea na mke wake tokana na ukaribu wetu. Nilibahatika kupata kupata kazi mkoa tafauti na kisha kurudi tena masomoni nje ya nchi. Kutoka na mateso na manyanyaso rafiki yangu aliamua kubwaga manyanga, akaamua kuachana na mumewe. Aliomba uhamisho wa kurudi kufanya kazi ktk mkoa alikozaliwa!

Alikuwa ni mshauri wangu mkubwa katika masuala mbalimbali. Hadi leo bado ni mshauri wangu, juzi kati kaniitia nikanunue shamba huko kwao kwani lilikuwa linauzwa kwa bei kama ya bure.
 
Able man hukuonesha abilities zako akaamua akupotezee baada ya kukutana na wazee wa Kazi Bagamoyo.
 
I have a male friend

Urafiki wetu umepelekea hadi mke wake akawa rafiki yangu tena tumeshibana zaidi yake(rafiki). Tulianza urafiki kabla hajaoa...tukashirikiana kutafuta mchumba...nikamsindikiza kutoa mahari...tukaoa...walichelewa kupata mtoto tukafunga na kuomba pamoja...tukahangaika hosp pamoja...wakapata mtoto wa kike...wakamwita jina langu


Tunalia wote...tunacheka wote
Hajawahi kunikosea adabu
Ananipenda
Nikikosea ananikanya kama rafiki kwa upendo

Urafiki wa kike na wa kiume is very possible

Mungu akubariki my friend.

Mungu akubariki rafiki yangu
 
mimi washkaji wa kiume hawahesabiki, wa kike nna wawili tu
 
Yes nimekukumbuka sana asee huyu mke naona nimuache tuyajenge old friend
 
Nilikutana nae Sjut-dom tuliishi kwa upendo na kushare mengi,tulishauriana mengi kuhusu masomo tulipeana moyo pale tulipofeli maana ilikuwa kufeli tunafeli pamoja,alikuwa mrembo sana na sikuwahi kumuomba tunda japo wengi walipotuona walijua tunakulana.
Nilikuja kupata mpenzi chuoni akanionya kuhusu ukaribu na yule rafiki yangu wa kike sikumsikiliza nilimuelewesha kuwa yule ni rafiki tu hakuna cha zaidi wakawa wanaitana wifi lakini mpenzi wangu alikuwa anavuta mdomo hapendi hata kuitwa wifi.Siku moja tulienda cape town usiku tukala pombe yule rafiki yangu akajichanganya akamix pombe nyagi yangu na wine na hajazoea alitaka tu kuona je itampelekesha maana alikuwa anajisifu anaziweza pombe.Alilewa sana kiasi cha kumshika na kumsapotu huku akitembea akiwa amefunga macho nilimpeleka hadi kwake nikamuingiza ndani,ilikuwa ni saa 7 usiku nikawaza naendaje kwangu sasa na bajaji tuliyokodi ilishaondoka nikaamua nalala pale kwake,nilikula tunda usiku ule na vibe la nyagi,asubuhi mapema niliamka zangu nikasepa geto kwangu nilijua urafiki utaisha maana nimemla akiwa kalewa,nikaanza kumkwepa cha ajabu hakuwahi kuzungumzia lile swala na urafiki uliendelea japo nilikuwa namkwepa sana baadae tulimaliza chuo akaolewa ana watoto saa hizi na bado tuna kaurafiki.
 
Mkuu unabahati Sana Mke wake alikubali urafiki baada ya ndoa. Wengi wao kwenye uchumba anajifanya anakubali urafiki wenu, wakishafunga tu ndoa hataki uwe na mazoea na mume wake na urafiki wenu utafia hapo.
 

Tunategemea coments zako nyingi kwenye ule uzi.
 
Sjawai kuwa na rafik wa kike..hata niliokuwa nao niliishia kuomba ishu tu na kupewa na urafik kuishia hapo
 
Chukulia ww ndo mke wa rafiki wa binti fulani,unaweza kuruhusu mahusiano ya ukaribu wa namna hyo uendelee kuwepo?
Na unaweza kuona hata mtoa mada pamoja na kusema huyo mwamba alikuwa best tu ila unaweza kuona kuna ka nafasi amekaweka ka kumtunuku mwamba mbususu,hakuna mpenzi atayekubali mpenzi wake awe na urafiki na jinsia tofauti na yeye..
 

Nakukunda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…