JF Toons
Digital Art by JF
- Feb 19, 2024
- 33
- 73
Katika harakati za kupambana na maisha, tunakutana na chanamoto hapa na pale ambazo wakati fulani unaweza kuona dunia imeisha na hakuna pakutokea, lakini amini kwamba hayo magumu unayopitia yana mlango wa mafanikio, usikate tamaa sababu kuna siku utapata ufumbuzi na magumu yote yabaki kama historia na funzo kwako.
Wahenga walisema mvumilivu hula mbivu, lakini pia mchumia juani hulia kivulini.
Ulifanyaje kukabiliana na jambo gumu la kukukatisha tamaa mpaka ukalishinda?