Ulitumiaje Mshahara wako wa kwanza?

nilianza na mshahara wa 1.8Mil walahi Lechaz bar walinikomaaa...
 
Mshahara wangu wa kwanza ulikua m3.5 fund kampun moja hv ya mhind mkataba wa muda mwaka mmoja unusu alipata tenda Helios ya kufunga minara na kufanya marekebisho,m2 alichukua dalal m1 alichukua mganga wa kienyej aliyenipigia ndumba mpaka nikapata mchongo baada ya kusota miaka nane tangu nihitimu,laki tano nikaenda kuichoma baa na washkaj kumlaan shetan na kuingiza akili mpya.
 
Nililewa sana nusura nifukuzwe kazi. Ndani ya siku moja tu imeisha na madeni juu! Mbona niliisoma namba mzee baba?
 
Kodi ya miezi sita + nauli ya kumsafirisha wife + godoro nikabakiwa na 100k
 
Na Mimi wa mshahara wa laki 3 naruhusiwa Kusema chochote au nikae pembeni kwanza?
 
Hamna aliyetoa mzaliwa wa kwanza madhabahuni? wala fungu la kumi?

Ndugu zangu, mmekula hata yale mavuno ya kwanza tuliyokatazwa? Kwamba apaswa atolewe bwana?
Unatoaje fungu LA kumi ikiwa pesa yenyewe haitosh mahitaj muhimu
 
Hii mishahara ya humu mmh mbona najiona nipo nyuma sana😪😪 kuanza na take home ya 1. M? Duh
 
Nilienda kuutoa malimbuko kanisani
 
Mie niliishia kulipa madeni tu maana nilikuwa juu ya mawe kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…